Dr. Bashiru Ally anakagua bandari huko ziwa Victoria na kutoa maelekezo, huku wapinzani hata mikutano ya ndani tu wanazuiwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,786
2,000
Wakati tunasoma na kusikia kuwa, wapinzani wanazuiwa kufanya hata mikutano ya ndani,huko kanda ya ziwa kupitia tv(TBC 1), namuona Katibu Mkuu wa CCM ,Dr.Bashiru Ally akitembelea bandari katika ziwa victoria na kutoa maaelekezo kwa watendaji.

Maoni yangu:
Wapinzani wasilaumiwe kwa uamuzi wowote watakaochukua maama hio ndio njia pekee iliyobaki kwa sasa.

Nia wanayo,sababu wanayo,uwezo wanao ila muda wa kupoteza zaidi ndio hawana-siwezi kuwalamu kwa lolote.

Jambo lingine,nimejifunza ni bora wapagani wasio na dini kuliko sisi wengine wanafiki tunaojifanya kumjua Mungu na kumtaja kila mara.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
46,215
2,000
Jipya lipi kwenye siasa? Kazi ya upinzani ni kuikosoa Serikali unataka mapya yapi? Wakati Wapinzani wote mmewabambikia kesi? Endelea kufanya makosa mapya utaona upinzani upya pia ingawa mnatumia udikteta kuwaziba midomo Wapinzani.
Upinzani aujafika Tanzania MKUUU pengine unapatakale karuzuku nakuhakikishia mpwa CCM aitoki Leo wala keshokutwa pale wamebakià wachumia ttumbo basiiii
 

Aikambee

JF-Expert Member
Sep 27, 2017
4,058
2,000
Bado unakwepa hoja ya msingi...vyama vingine ndio visiendelee na shughuli za kisiasa kwasababu tu CCM imeunda serikali? Kama hivyo ndivyo, hiyo haki imetolewa kwenye katiba gani ya nchi yetu? Hii ni mara ya mwisho nakuuliza, na ukiendelea kuleta ujanja ujanja wako wa kiccm, nakuacha ili uendelee kula matango pori peke yako.
Shughuli za kisiasa zinaruhuziwa, ila kama kuna sababu za msingi za kuzuia, zinazuiliwa. Mfano, chadema kutaka maandamano wakati watu wanataka maendeleo siyo sawa.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,523
2,000
Acha ufala wewe kipenzi cha wengi wa wapi? Kipenzi cha wengi angehangaiks kiminya demokrasia? Kwanza 2015 hakuchaguliwa bali uchakachuaji ndiyo ulimpeleka ikulu? Huko 2020 labda muibe kura kwa kuwatumia Polisiccm na Tumeccm ndipo arejee ikulu lakini kura za Ukweli hakuna wa kuwapa.
Hata hao mnaosema watamsaidia kurudi ikulu, basi ndio hao hao wengi kwa kuwa, mmeshindwa kumzuia
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
92,750
2,000
Wakati tunasoma na kusikia kuwa, wapinzani wanazuiwa kufanya hata mikutano ya ndani,huko kanda ya ziwa kupitia tv(TBC 1), namuona Katibu Mkuu wa CCM ,Dr.Bashiru Ally akitembelea bandari katika ziwa victoria na kutoa maaelekezo kwa watendaji.

Maoni yangu:
Wapinzani wasilaumiwe kwa uamuzi wowote watakaochukua maama hio ndio njia pekee iliyobaki kwa sasa.

Nia wanayo,sababu wanayo,uwezo wanao ila muda wa kupoteza zaidi ndio hawana-siwezi kuwalamu kwa lolote.

Jambo lingine,nimejifunza ni bora wapagani wasio na dini kuliko sisi wengine wanafiki tunaojifanya kumjua Mungu na kumtaja kila mara.
Huo ndiyo ushenzi wa ccm huyo Bashiru anakagua kwa ujuzi upi kama siyo kufanya siasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
12,270
2,000
Evolution Africa haijawahi kufika mwisho.
Mfano wa muendelezo wa evolution ni uzi huu wa kwako, unashindwa kuelewa kuwa katibu mkuu wa chama kilicho madarakani ni mmoja wa wasimamiaji wakuu wa sera zinazoongoza nchi.

Analo jukumu la kuwafuatilia wabunge wa chama chake, pia analo jukumu la kuangalia muendelezo mzima wa sera.
 

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
6,134
2,000
Muogope sana mtu anayejifanya kumtajataja Mungu kila mara na wale walio mstari wa mbele kwenda kwenye nyumba za ibada.

Waogope sana hao watu hata Yesu aliwaona na akasema sio wale waniitao bwana bwana watakaouona ufalme wa Mungu, (Mathayo 7:21).
 

demulikuy

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
944
1,000
Huyu ni kiongozi wa serikali!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly ? Ni wazi sasa Dr hayaelewi madaraka yake. Baada ya CCM kunadi sera zake "zikakubaliwa' ni jukumu la Serikali ya CCM kutekeleza ilani hiyo na kutoa "FEEDBACK" kuhusu utekelezaji wake kupitia VIKAO RASMI VYA CHAMA. Na kama kuna ulazima Serikali kupitia waziri husika huitwa makao makuu ya CHAMA kutoa ufafanuzi.
"Secretariat" ya CHAMA haipaswi kuchukua majukumu ya serikali kama vile kukagua utendaji wa bandari. Hili la kupunguza vikao vya chama CCM, waliangalie upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masinki Nyansarari

Senior Member
Nov 24, 2018
142
225
Katibu mkuu ana wajibu wa kuangalia utekelezaji wa ilani ya chama ili kuikumbusha serikali pale inaposhindwa kutekeleza kwa wakati
Anyway ccm ni serikali na serikali ni ccm
 

senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,454
2,000
Katibu mkuu wa ccm ni namba nyingine.Hao ndio walopewa ridhaa ya kuongoza.Akifanyacho ni sahihi kabisa.Wala usije ukamlinganisha wadhifa wake na ukatibu mkuu wa
akina VISHETI MASIZI
 

alitosis

Member
Apr 30, 2017
92
125
Wewe ni zwazwa yaani hata majukumu ya chama hujui kwa serikali hujui yaani hata hujui ni nani alipaswa kukagua au kusimamia hiyo ilani tena ni bora ingetekelezwa Bora.....pumbavu ndo maana kuna mawaziri wapo ambao ni wanapaswa kuwa wanachama wa chama tawala.hawa sasa wanapaswa kufanya hivyo na anayejiita katibu anapaswa kutoa maelekezo kwa mawaziri na si kwa watumishi wa uma moja kwa mojamoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 

dumuzi

JF-Expert Member
Mar 16, 2007
966
1,000
Kwani Katiba ya Tanzania inapotaja neno "tawala" ina maanisha kwamba yenyewe ni katiba ya kidikteta?

Kwa Tanzania, neno "tawala" lina maana ya kuwa madarakani au kuongoza.

Hayo uliyoyawaza kinyume na hapo ni ya kwako tu.

Kwanza democracy ya nchi moja haifanani na nchi nyingine.

Mfano, Kenya rais bora kwao ni yule anayetokana na kabila kubwa aidha Mkikuyu, Luhya, au Kalenji.

Kwa Tanzania rais bora ni yule anayetokana na CCM maana CCM ndicho chama kilichosheheni viongozi bora kabisa walioandaliwa kwa muda mrefu na wana ujuzi na uzoefu katika uongozi.

Hivyo vyama vingine hakuna kitu, zaidi sana kuna makapi yaliyochekechwa na kutemwa na mfumo was CCM
Mkuu nitajie kwanza hiyo ibara kwenye katiba unayoizungumzia. Pili katiba iliyopo ilitungwa kipindi cha udikteta wa chama kimoja ndio maana dhana ya chama tawala iko vichwani mwenu. Mkuu usidhihaki nchi ya Kenya wana upeo mikubwa wa kidemokrasia kuliko bongo. Majaji waliweza tengua ushindi wa raisi ingekuwa bongo wangetekwa na kupotezwa kama Ben Saanane ama wangemiminiwa risasi kama Tundu Lisu. Halafu cha kushangaza mkuu hao unaowaita makapi walikuwa ni viongozi wa juu wa ccm na kwenye serekali ya ccm. Kama unajinasibu ccm in viongozi bora walioandaliwa ilikuweje hawa makapi washike nafasi hizo za juu? Kama makapi waliweza kushika nafasi hizo waliokuwepo inaonekana ni makapi zaidi. Inaelekea chama kina makapi kikao kuliko viogozi bora.
 

Nangere

Member
Jun 2, 2018
95
125
We ndiye hujiitambui sasa kwa taarifa yako.

Kwa hiyo unataka kusema nini?

Kwamba kwa kuwa Mimi ni Mchagga, sipaswi kuiunga serikali ya CCM mkono???

Na kwamba kwa kabila langu basi niwe mfuasi wa chadema?

Tuseme tu ukweli, hakuna chama chenye uwezo wa kuongoza Tanzania zaidi ya CCM.

Kama wapinzani wanalalamika kuibiwa kura na hawaji na ushahid wala suluhisho, je, wataweza kusimamia fedha za nchi achilia mbali taasisi za umma?

Wameshindwa kuongoza vyama vyao, je wataweza kuongoza nchi yenye raia milion 50+?
Naona kwa namna ya uandishi wa hoja zako mfilisi na mtiririko wa mfumo wako wa kufikiri, huna uwezo wa kuelewa wala hustahili kueleweshwa jambo. Nitajitahidi kidogo kukuelimisha kwa kifupi ifuatavyo:
Mwl J K Nyerere aliwahi kusema kuwa "kukimbilia dini, ukabila, na /au ukanda ni kufilisika kisiasa."
Nilichokisema ni kuwa jiana lako la Aikambee limebeba "usanii". Mchaga ni mtanzania. Mgoni naye ana haki kikatiba ya kujiunga na chama chochote cha siasa bila kuvunja katiba na sheria za nchi. Unarukia "uchaga" na "uccm"!
Unatumia nguvu kubwa na hoja zisizokuwa na mpangilio kutetea mambo yaliyo sivyo ndivyo. CCM inaelekeza na kusimamia nn serikali yake ifanye kwa mujibu ya ilani yake iliyoiweka madarakani; siyo haki na sahihi kusimama badala ya serikali.
Mantiki yake yako wapi? Chama chochote tawala ni chama cha upinzani mtarajiwa bila kujali muda wake wa kushika na kuiongoza. Kuasisi na kustawisha utamaduni wa akina Bashiru kunamaanisha kuwa chama cha upinzani xy kitakapokamata madaraka kitafanya hivyo hivyo.
Utawala bora unaozingatia sheria za nchi unataka kuwepo mgawanyo wa kazi na mipaka ya utendaji kitaasisi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom