Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
- Thread starter
- #21
KakaKiiza,
Nakushukuru sana. Lazima tuifikishe JF mahali inapotakiwa kuwepo. Kuelimishana na kukosoana huku tukiheshimiana itakuwa nguzo ya maendeleo yetu binafsi na taifa kwa ujumla.
Hatuwezi kuibadili nchi kwa kutukanana na kudharauliana. Hatutakuwa na tofauti na wabunge wanaozomea wenzao na kuwaita makondakta halafu wabunge wanaoona wamedharauliwa wanapoamua kurudi kwa wananchi kushtaki wanaambiwa wanavunja amani. Tatizo la sasa ni dharau na watu kujiona bora zaidi.
Nitasema wazi, CCM wanadharau upinzani. Wanajiona wao ni bora na wanamamlaka. Hoja ikipelekwa bungeni wanaangalia inawasaidia nini kama chama sio ina maslahi gani kwa nchi. As a result wanajikuta wanaongoza wananchama wao na sio wananchi. Inapofika hapo wanasema tatizo Chadema. Yote imeanzia kwenye dharau.
JF hatutadharauliana. Wachache wanaweza kudharau lakini wengi tuendelee kuelimishana na kukosoana kwa hoja. Hii nchi inatuhitaji sisi kuilinda, kuitetea na kuiendeleza. Haihitaji matusi, kejeli, dharau na jazba.
Nakushukuru sana ndugu. Tuijenge nchi yetu pamoja.