Dr Augustino Lyatonga Mrema aliwezaje kuimudu Wizara ya Mambo ya Ndani inayowashinda Mawaziri wengi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,667
Dr Mrema aliweza kutimiza majukumu yake kiufanisi hadi kupandishwa cheo na kuwa Naibu Waziri mkuu.

Ni mbinu gani alizitumia mangi huyu katika kutimiza majukumu yake kwa ufanisi ambazo mawaziri wa zama hizi hawajazing'amua.

Waliofeli ni pamoja na Mwapachu, Lau Masha, Dr Nchimbi, Dr Kitwanga, Dr Nchemba na Lugola.

Maendeleo hayana vyama!
 
1. Hakuwa Mnafiki, Mwongo na Mfitini
2. Alijiamini na Kutoogopa lolote
3. Alijua vyema Majukumu na Mipaka yake.
4. Alitaka Kuaminiwa na Kutoingiliwa na alithaminiwa kwa hilo na Wakubwa zake.
5. Alikuwa ni Mbunifu hasa kwa Masuala mazima ya Uhalifu na Usalama.
6. Alipita katika Misingi mizuri ya Kiusalama ( Kiujasusi ) ndani na nje ya nchi.
7. Hakukubali Kutumika, Kumuonea Mtu au Kujipendekeza ila aliruhusu Taaluma yake na Maadili vifanye Kazi.
 
Aliiweza wapi? Ingekuwa ni kipindi cha JPM mbona angetumbuliwa asubuhi? Msilinganishe utawala huu na zilizopita!
Kwani kipindi hiki....tena juzi tu Dr Augustino Lyatonga Mrema hajateuliwa na Rais Magufuli kutimiza majukumu katika wizara ya mambo ya ndani?

Acha kukariri bwashee!
 
A.L.Mrema amekuwa Waziri katika utawala wa chama kimoja kwa hiyo ni mazingira tofauti na ya sasa,Mr.Mrema alikuwa waziri wa wizara hii wakati average ya umri wa watanzania was 40+ means wengi walikuwa waoga etc etc.

Sasa kuna generations mpya yenye damu zinazochemka,mitandao imekuwa mengi inayosaidia habari kusambaa kwa haraka, Mr.Mrema hakuwa waziri aliyefanikiwa sana ,yeye pia alipenda utawala wa amri,mashurutisho na bila kufuata utawala wa kisheria alianzisha na kulazimisha ulinzi wa sungusungu bila ya kwanza kuutungia sharia(Adv.Lamwai aliweza kuutoboa mfumo huu wa sungusungu mbele ya mahakama,kuwa haukuwa wa kisheria).

Na hiki cheo cha unaibu waziri mkuu HAKIPO KIKATIBA,ni press tu ndio walijipendekeza na kuamua kumwita kwa cheo hicho.Mh.A.H.Mwinyi kwangu ndiye aliyeimudu wizara hii and he resign kwa kuwajibika.hii wizara ni kubwa mno vunja na zilwe wizara mbili,POLISI NA MAMBO YA NDANI(hawa only wahusike na uraia,uhamiaji)na Polisi wao usalama na ulinzi wa raia.
 
johnthebaptist,
Wakati huo kupiga ilikuwa ruksa, siku hizi hapana.

Kuna waziri unamfahamu alitumbuliwa wakati huo kwa kupiga? Mbona wote walidumu si Mrema peke yake
 
Back
Top Bottom