Dr. Asha-Rose Migiro does better interview than JK?

Mzuvendi,

JK was asked about ECOMONIC CRISIS akajiuma jiuma kujibu.
The point is huyu mama so clear,to the point and articulate.

Mstahiki
 
Hebu mpumzisheni JK...hivi mshasikiliza interview za AMINA SALUM ALI aliyoko kule UN?

That woman is so useless kabisa
 
Kuwa na interview nzuri haina maana kwamba unajua au unaamini kile unachokisema. Nyerere alikuwa mzungumzaji mzuri, interview nzuri, lakini alikuwa haamini kile alichokuwa anakisema. Pamoja na speech zake nzuri, alishindwa kuwasaidia WTZ kimaendeleo, elimu nk. Kwa hiyo, kuwa na interview nzuri, Si kigezo cha kuwa na knowledge ya kuongoza, bali ni kipaji tu cha kuzungumza.
 
I was really impressed with Dr Mingiro interview,She is so clear,to the point and articulate.She way better that JK.What do you think?
....Aisee,sijui kwanini huwa tuna tabia ya kulinganisha visivyo linganishika!! sasa kwa lugha ya sebuleni ni kwamba:Kitandani kwa The-Migiros hupumzika Digrii saba!! sijui kwa huyo mwenzangu na miye zaidi ya miguu minne kunani??....sijui!!!....
 
Kuna vitu Mama Migiro amesema ambavyo ningeshukuru kupata ufafanuzi.

Akiongelea madhara ya global financial crisis kwa wanawake wa Tanzania na Africa, amesema, wanawake ndio wanafanya kazi kubwa shambani, na ndio wanaofanya "petty trade," na hivyo, kutokana na hii credit crunch, na mfumuko wa bei za vyakula, basi vyovyote ambavyo wanawake wamekuwa wakifanya vitadhurika.

Ningependa kuelewa, jee, credit crunch inamwathiri vipi msuka ukili na mchoma chapati na mponda kokoto (petty traders). Mpanda mihogo na mtama ataumia au atafaidika na mfumuko wa bei ya vyakula?

Kwa nchi zenye uchumi wa kuazimana, credit crunch inaathiri vitu kama mikopo ya mortgage, mikopo ya wanafunzi, mabenki, investments za makampuni, na mikopo ya ununuzi wa magari.

Kama sio tabia ya kugeza ya kwingineko, Global credit crunch inamuathiri vipi Mama Ntilie wa Gezaulole?
 
Wataathirika zaidi kwenye matibabu, kusomesha n.k.
Kwa upande mwingine, baadhi ya wanaume watazikimbia familia zao kukwepa jukumu la kuilea familia ambalo sasa linaendelea kuzidi kimo.
 
....Aisee,sijui kwanini huwa tuna tabia ya kulinganisha visivyo linganishika!! sasa kwa lugha ya sebuleni ni kwamba:Kitandani kwa The-Migiros hupumzika Digrii saba!! sijui kwa huyo mwenzangu na miye zaidi ya miguu minne kunani??....sijui!!!....

Mh? Makubwa!!!!!!
 
Bila kupoteza muda na kutaka kupoteza maana ya aliyetoa mada, Migiro is more bright and clear than the mzee wa ngoma. Hata kama wangekuwa kwenye topic moja au la, bado mama yuko juu sana. Dilunga unachosema inawezekana ni kweli au isiwe kweli pia, ki ufahamu wanawake ni watendaji wakuu na walezi wa familia, wanaume ni guider kwenye nyanja zote huku wamama tukisaidia implementation.

kama ameiga lakini point imeeleweka.
 
Ni JK huyuhuyu aliyesaidia kumfikisha huyu Mama hapo alipo sasa. Huyu Mama ni kati ya TEUZI nzuri alizowahi kufanya JK. Nasikia anaandaliwa kuwa RAIS 2015?
 
does JK our role-model for everything? usisahau Dr. Migiro ana PhD na uzoefu wa kutosha kwa mambo mengi, JK pamoja na uzoefu mzuri lakini bado hana kisomo cha juu kama Rose, ukichanganya na kipaji cha kupangilia points basi wanakuwa tofauti tu
 
Ni JK huyuhuyu aliyesaidia kumfikisha huyu Mama hapo alipo sasa. Huyu Mama ni kati ya TEUZI nzuri alizowahi kufanya JK. Nasikia anaandaliwa kuwa RAIS 2015?

I beg to differ, jamani huyu mama juhudi yake ya kazi ndio imemfanya afike hapo alipo! hiyo sio siasa ya tanzania ya kupeana viti vya ubunge!:rolleyes:
 
Kuna vitu Mama Migiro amesema ambavyo ningeshukuru kupata ufafanuzi.

Akiongelea madhara ya global financial crisis kwa wanawake wa Tanzania na Africa, amesema, wanawake ndio wanafanya kazi kubwa shambani, na ndio wanaofanya "petty trade," na hivyo, kutokana na hii credit crunch, na mfumuko wa bei za vyakula, basi vyovyote ambavyo wanawake wamekuwa wakifanya vitadhurika.

Ningependa kuelewa, jee, credit crunch inamwathiri vipi msuka ukili na mchoma chapati na mponda kokoto (petty traders). Mpanda mihogo na mtama ataumia au atafaidika na mfumuko wa bei ya vyakula?

Kwa nchi zenye uchumi wa kuazimana, credit crunch inaathiri vitu kama mikopo ya mortgage, mikopo ya wanafunzi, mabenki, investments za makampuni, na mikopo ya ununuzi wa magari.

Kama sio tabia ya kugeza ya kwingineko, Global credit crunch inamuathiri vipi Mama Ntilie wa Gezaulole?
hapo ni suala la kutunga sentensi tuu, uhalisia unakuja bdaee..

halafu western media zinaangalia jinsi unvyonyoosha sentensi na vibwagizoooo...

natumai dr migiro pale new york ameshapata orientation nzuri ya media mgt na public communication ambavyo viongozi wengi kwetu wanakosaa sanaaaa
 
I beg to differ, jamani huyu mama juhudi yake ya kazi ndio imemfanya afike hapo alipo! hiyo sio siasa ya tanzania ya kupeana viti vya ubunge!:rolleyes:
Naibu Katibu Mkuu wa UN ni cheo cha kisiasa zaidi. Uwaziri wake wa Mambo ya Nje aloopewa na JK umemsaidia sana kwenye uteuzi huu. Juhudi ipi ya kazi iloomfikisha hapo? Asingeingia kwenye siasa kwa mlango wa nyuma(viti maalum) asingefika huko!
 
I beg to differ, jamani huyu mama juhudi yake ya kazi ndio imemfanya afike hapo alipo! hiyo sio siasa ya tanzania ya kupeana viti vya ubunge!:rolleyes:

I agree with you. Asha is a capable indivudual, inteligent woman and hard working person. Kwenye ambayo ina patrichal system kama yetu, kwenda juu kwa wanawake kwenye siasa kunategemea kwa kiasi kikubwa ridhaa ya wanaume. Vilevile ikumbukwe uwezo wa urais hautokani na kufanya interviews nzuri, it is much much more than that.

Hata hivyo pamoja na kuwa Asha haziwezi siasa za ufisadi, majungu, fitan na vitu kama hivyo, lazima tukubali kuwa ana uwezo mkubwa mara nyingi kuliko muungwana. Sasa hivi rais anayetafutwa ni wa 2010 hatuhitaji wa 2015 kwa sababu tatizo sasa liko 2010. I wonder why some people are trying to talk about 2015 while 2010 is a bigger headache that 2015. Are you out of your mind?
 
Back
Top Bottom