Dr. Abbas: Tenda ya ujenzi wa reli ya SGR kutoka Mwanza-Isaka itatangazwa wakati wowote

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Shirika la Habari la Kimataifa la CNBC Africa tarehe 29 Februari, 2020 limerusha kwa zaidi ya nchi 100 duniani makala inayoeleza mafanikio ya Tanzania katika sekta mbalimbali

Ripoti ya RMB ya mwaka 2020 imeitaja Tanzania imekuwa ya 21 duniani, Afrika imekuwa ya 4 na Afrika Mashariki imekuwa ya Kwanza kwa kiwango cha biashara ndogondogo na uboreshaji wa shughuli za machinga

Haki za binadamu sio siasa, kama nchi tumeendelea kusisitiza na tutaendelea kuzienzi haki zote za binadamu

Ujenzi wa reli ya SGR kwa eneo la Dar-Moro umefikia zaidi ya 75% na Moro-Makutopora umefikia zaidi ya 28% ikijumuisha uwekaji wa nguzo na nyaya za umeme ambapo jumla ya fedha zilizotumika hadi sasa ni Trilioni 2.957

Tenda ya ujenzi wa reli ya SGR kutoka Mwanza-Isaka itatangazwa wakati wowote

Ujenzi wa Chelezo katika ziwa victoria umekamilika na inasubiriwa kujaribiwa kwa uzito uliosanifiwa wa tani 4000 na itaanza kutumika katikati mwa mwezi Machi, 2020

Ujenzi wa MV Victoria katika ziwa Victoria umefikia 89% na ukarabati wa MV Butiama umefikia 86%

Mradi umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) sehemu ya ujenzi wa eneo la kuchepusha maji ya mto limekamilika kwa 100%

Utendaji wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi umezidi kuimarika, jumla ya migogoro ya ardhi 10,000 imetatuliwa

Tunataka utawala bora katika vyama vyote vya michezo, sisi kama Serikali tunafuatilia, moja ya eneo ambalo nitalifuatilia kwa karibu katika sekta ya michezo ni vitendo vya rushwa

Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuwa Serikali ijenge uwanja wa Michezo Dodoma uliokuwa ujengwe na Morocco na tunategemea ujenzi wa uwanja huu uanze mwaka huu baada ya ramani kukamilika

Nampongeza sana Mbwana Samatta kwa mafanikio makubwa katika soka, tutaweka mikakati ya kuwa na vituo vya mafunzo vya michezo ‘academy’ ili kukuza na kuendeleza vipaji nchini

Haitatokea katika dunia hii, Serikali yoyote duniani kwa chochote inachokifanya isikosolewe, hata manabii walipingwa, Serikali ina nia na kila sababu ya kutokulala kuwapigania watanzania, sisi tupo kazini tunapiga kazi ili kupata maendeleo

Imeandaliwa na Idara ya Habari - MAELEZO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia nzima viongozi wanahangaika kuinua maisha ya watu pamoja na mambo mengine sisi kwetu tofauti sana

Nchi inajengwa na wakulima na wafanyakazi lakini sisi wafanyakazi hali zao ngumu madeni yanawakaba mishahara haiongezeki hata ndururu huku wakulima wakinyimwa ruzuku na mazao yote ya biashara yakiachwa yameanguka.

Biashara zimekuwa holela na wenyebiashara rasmi wanaangushwa na makodi pamoja na low purchasing power inayokabili wananchi. Tusidanganyane na maujenzi wakati wananchi ndiyo wamebanwa mbavu mpaka mwisho.
 
Huyu amekuwa kama yule msemaji Wa sadam Hussein, maneno meengi Na majigambo utadhani mhaya.
 
Leo hii mbunge wa Mbeya kazuiliwa kufanya mkutano na wananchi wake ambao kimsingi ndiyo walio mchagua
 
..ameharibu hapo alipodai " haki za binadamu siyo siasa..."

..alitakiwa atoe taarifa ya miradi na mafanikio ni siyo kurusha VIJEMBE na kuanzisha MALUMBANO.

Magufuli ndio huwa anasema hivyo, sasa yeye anawakilisha mitazamo ya boss wake.
 
Huyu amekuwa kama yule msemaji Wa sadam Hussein, maneno meengi Na majigambo utadhani mhaya.

Halafu sasa hivi wamekuja na utapeli wa kutaja mambo kwa Percentage na zote ni above 80. Utasikia elimu bure utekelezaji ni zaidi ya 90%, mapambano ya rushwa mafanikio ni zaidi ya 85%, miradi yote asilimia huwa ni zaidi ya 80%. Uchunguzi wa takukuru ni 99%. Ukifuatilia vizuri huu utapeli ni wa jiwe toka akiwa waziri alikuwa anatoa taarifa za kupika na alikuwa anatumia mtindo wa hadaa kwa kipimo cha asilimia. Sasa hivi kawa mkulu ndio kawaambukiza wote huo uongo wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom