Dr. A.Meru(EPZA):Kubadilisha Majina ya kampuni hakuambatani na ukwepaji kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. A.Meru(EPZA):Kubadilisha Majina ya kampuni hakuambatani na ukwepaji kodi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by TUJITEGEMEE, Apr 28, 2012.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,681
  Trophy Points: 280
  Dr. A. Meru, Mkurugenzi mkuu wa Export Processing Zone Authority (EPZA), amesema utaratibu unaotumiwa na makampuni kubadilisha majina: mfano Sheraton kuwa MovenPick, Airtel kuwa Zain, Mobitel kuwa Tigo, n.k., hauambatani na ukwepaji wa kulipa kodi. Amesema ukwepaji huo wa kodi haupo kwani mkataba unausisha mradi (project) wala sio jina la kampuni. Pia alisema utaratibu wa kubadilisha majina ni wa kawaida kwa makampuni mengi duniani wala hili halifanyiki Tanzania tu. Aliongeza kuwa EPZA inatoa likizo ya kutolipa kodi (tax holiday) ya miaka kumi. Muda huo ukiisha lazima kampuni ilipe kodi bila kujali ilibadilisha jina ama la.

  Dr. Meru aliyasema haya wakati wa Mhadhara wa wazi kwa Umma (Public Lecture) uliondaliwa na Engineers Registration Board (ERB) na kufanyika Luther House (Dar-es-Salaam) jana huku yeye akiwa mzungumzaji mkuu.

  Source: ERB


  WanaJF mnasemaji kuhusu maelezo haya ya Mkurugenzi mkuu wa EPZA?
   
 2. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama amesoma MBA mwambieni aka review upya topic inayoitwa TRANSFER PRICING! aone huo ujinga anao utetea wa TAX HOLIDAY ya miaka 10! labda watu wanaiogopa hiyo PHD yake! Unaweza kuwa PHD holder bado ukawa kiazi wa kutoa mawazo kama Dr Benson Bana wa UDSM!!!!:shut-mouth:
   
 3. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,681
  Trophy Points: 280
  Professionally ni Mechanical Engineer.
   
 4. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  viongozi wa namna hii
  ni mzigo kwa walipakodi
  ni vema tukatoa mawazo kwenye katiba
  mpya bunge lipewe meno
  baada ya kiongozi wa shirika la uma pamoja na Mkuu wa jeshi la polisi, magereza na uhamiaji

  majina yao yapelekwe bungeni, yajadiliwa na ikionekana aanafaa ndio aidhinishwe kuwa MD

  hii itasaidia saana kuwawajibisha hawa ma MB mbumbumbu

  angekuwa china angepewa zawadi ya kunyongwa
   
 5. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,681
  Trophy Points: 280
  Akitetea uwamuzi wa EPZA kutoa tax holiday ya miaka kumi kwa kampuni zinazotaka kuwekeza katika SEZ(special economic zone) na EPZ(expert Processing zone) alisema miaka 10 wanaanza kuihesabu pale tu kampuni inapopewa leseni wakati kampuni hiyo kabla hajaijapata eneo la kufanyia kazi, kujenga kiwanda n.k.

  Alongeza kuwa ni vigumu kwa kampuni kuanza kupata faida (Break Even) ndani ya muda huo kwa maeneo hayo ya SEZ na EPZ.

  Kwa maelezo zaidi namna scheme za EPZ na SEZ zinavyofanya kazi soma hapa>>>http://www.epza.co.tz/About-EPZ-Program.html
   
 6. S

  Speculator Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu na mm ngoja niitafute hiyo topic TRANSFER PRICING je itakuwa kwenye Accounting or Corporate Finance ?
   
 7. S

  Speculator Member

  #7
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu tayari nimejaribu kupitia TRANSFER PRICING naona kama inahusika Product Transfer Pricing Policy/methodology In Multinational Corporation among branches na sio Ownership Transfering Labda utusaidie kuelewa mahusino yake na tax in transfering ownership ? kwa nia nzuri na sisi tuelewe
   
Loading...