Dr A. Bashiri avitananga vyama vya siasa visivyo kuwa tawala

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Leo katika kipindi cha asubuhi za Radio One Nipashe kilikuwa kinamuhoji Dr. Bashiri Ally (Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam – Kitivo cha Siasa) kuhusiana na lengo kuu la vyama vya siasa. Katika majibu yake alisema kuwa, Lengo cha tawala ni kuendelea kutawala na kushika dola, ila lengo la vyama vingine (ambavyo sio tawala) ni kuhamasisha umma kujiletea maendelea yao mengine.

My take : Kama ndivyo hivyo basi ina maana vyama vingine visivyo kuwa tawala havijui lengo lao kuu ni nini? Kwani kila siku tunasikia wakisema lengo lao ni kushika dola kumbe sivyo kabisa.
 
Amezungumza vizuri na ikitokea vikashika dola kwakuwa sii lengo la kutawala naamini vitajikita kwenye lengo lao kuu la kujiletea maendeleo
 
Kwa hiyo umemsikiliza huyo kama vile unavyomsikiliza Imamu nini?

Sasa wewe unataka kila kitu nikumalizie, ww humu jf upo kwa ajili ya nn? JF sio sehemu ya vilaza ni sehemu ya watu wanatoa thread na wengine wanachambua.usitake niamini kuwa ulikuwa hata darasani unaibia majibu ya wenzako kwa kutojishughulisha na kichwa chako
 
Dr Bashiri ni CCM damu,aliwahi kuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana tawi la Kanazi.
 
Leo katika kipindi cha asubuhi za Radio One Nipashe kilikuwa kinamuhoji Dr. Bashiri Ally (Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam – Kitivo cha Siasa) kuhusiana na lengo kuu la vyama vya siasa. Katika majibu yake alisema kuwa, Lengo cha tawala ni kuendelea kutawala na kushika dola, ila lengo la vyama vingine (ambavyo sio tawala) ni kuhamasisha umma kujiletea maendelea yao mengine.

My take : Kama ndivyo hivyo basi ina maana vyama vingine visivyo kuwa tawala havijui lengo lao kuu ni nini? Kwani kila siku tunasikia wakisema lengo lao ni kushika dola kumbe sivyo kabisa.

Siamini kama huyu ndiyo yule Bashir Ally aliwahi gombea urais wa Daruso akashindwa, Bashiri Ally aliyekuwa kampeni manager wa Sebastian Kinyondo (RIP) aliyeshinda na kumpatia zawadi ya kukaa bure katika nyumba yake ya pale Mabibo external kama anaweza kusema haya.

Nadhani alikuwa na maana kuwa 'Lengo la chama chochote tawala ni kuhakikisha kuwa kinaendelea kutawala kwa kuwaletea wananchi maendeleo yao ili kuwashawishi waendelee kuwachagua na lengo la vyama vya upinzani ni kuonesha mapungufu ya chama tawala kwa kuwashawishi wananchi kuwa kiki chaguliwa kitafanya tofauti na yanayofanywa na chama tawala na kuwapaisha zaidi'

Nafikiri hii ndiyo statement ambayo atakuwa ameitoa Dr Bashiri Ally, ila kama kaongea hayo kwenye thread yako basi sishangai maana maisha yamekuwa magumu na njaa zimekuwa kali sana miongoni mwa wasomi wetu hasa katika maeneo ambayo hayalipi kama haya ya kuwa mhadhiri wa siasa, na watu wengi wanajaribu kujifanya watumwa wa watawala ili angalau watupiwe masalia.
 
Back
Top Bottom