Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,988
Sio tuu mimi na wewe hatuwezi kumbana DPP, bali hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumbana, hata rais hawezi!.
Mzee MMKJJ, yote uliyosema kuhusu DPP ni kweli, lakini pia kwa mujibu ya sheria iliyounda ofisi ya DPP, havunji sheria yoyote kwa kutofanya uchunguzi wowote kwa vile hayo ndio mamlaka yake ambayo kisheria, anayatumia at his discretion as he pleases at his pleasure na sheria inamlinda.
Kwa maoni yangu, tatizo sio DPP, tatizo ni mamlaka ya ajabu yaliyochini ya DPP.
Niliwahi kuchangia mahali nikaainisha sheria yetu iliyounda ofisi ya DPP, amepewa mamlaka makubwa yac ajabu, na hayo aliyoyaainisha MMKJJ ni dibaji tuu, nguvu haswa za DPP ni pamoja na 'power to declare nolle proseque' yaani hakuna kesi ya kujibu. DPP huyu anauwezo wa kuingilia kesi yoyote ya jinai, ikiwa mahakama yoyote na ikiwa katika hatua yoyote kabla ya hukumu, kuisimamisha, kingilia, ama kuifuta bila kulazimika kutoa sababu zozote wala maelezo yoyote.
Sheria ya DPP inamtaka kutimiza wajibu wake bila shinikizo lolote kutoka popote na hata akiletewa kesi yoyote ni discretion yake aprosecute ama asiprosecute na hakuna chombo chochote ndani ya JMT chenye mamlaka ya kumuuliza lolote DPP, hata rais hana mamlaka hayo, sembuse MMKJJ?.
Naungana na WoS sisi mwisho wetu ni kupiga tuu kelele, japo za mlango, siku moja moja mwenye nyumba atakosa usingizi kwa sababu nyingine na atazisikia hizi kelele za mlango na ama ataamka na kuubana mlango, ama atautia kizuizi ili usiendelee kupiga kelele.
Enzi za Mwalimu kulikuwa na sheria ya 'Presidential Preventive Detention Orders' iliyompa rais mamlaka ya kumuweka mtu yoyote kizuizini kwa kipindi chochote bila kutoa sababu yoyote. Mwalimu Nyerere aliitumia kipindi chote cha utawala wake. Kipindi cha Mwinyi, wanasheria wa chuo kikuu wakiongozwa na Shivji na Mgongo Fimbo, waliichalenge sheria hii kwa 'court review' na mahakama ikatamka its a bad law, hivyo ikamlazimisha rais, kila akisaini 'preventive detention order' lazima atoe sababu. kuna detention moja ya Mwinyi ilipigwa chini na mtuhumiwa kuachiwa huru.
Kama wanasheria wetu, waliweza kufanya hivi dhidi ya mamlaka ya rais, wanashindwa nini kwenye mamlaka ya DPP?.
Kwa mawazo yangu, 'Tatizo sio Feleshi as DPP, ni mamlaka yake makubwa mno anayatumia atakavyo bila kuvunja sheria. Tazizo ni the institutional of the DPP.
watu wengi wanachanganya sheria ya Prevention and Detention ambayo bado ipo na sheria ya Emergency Powers za Rais. Sheria ya Prevention and Detention haimpi nguvu Rais kwa kiasi hicho ila ya Emergency Powers. Sijui kuhusu specific cases lakini ninafahamu sheria ambayo imewahi kutumiwa vibaya ni hiyo ya emergency powers ambayo ilidaiwa kutumika kwenye suala hili la EPA pia..
Unaweza kunisaidia review ya hiyo kesi ya kina Shivji juu ya Prevention and Detention?