DPP wa Tanzania: Ni Kihiyo wa Sheria, Msanii au Mbabaishaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DPP wa Tanzania: Ni Kihiyo wa Sheria, Msanii au Mbabaishaji?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kapelwa, Apr 14, 2009.

 1. k

  kapelwa New Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: Sep 4, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Nimeshitushwa na kauli za mara kwa mara za DPP wetu kuhusu ugumu wa kuishitaki kampuni ya KAGODA. Nimeshitushwa zaidi na matamshi yake yaliyonukuliwa na gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Aprili 12, 2009 kuwa: wamiliki wa KAGODA watafunguliwa mashitaka ikiwa itathibitika kuwa kampuni hiyo haikupewa kazi ya kukusanya madeni na kampuni za nje! Hivyo basi, DPP wetu sasa hivi anahangaika kuzitafuta kampuni hizo huko nje!

  Kwa msimamo huo wa kichekesho, mimi najiuliza: DPP WETU NI KIHIYO WA SHERIA, MSANII AU MBABAISHAJI TU? Nashindwa kupata jibu sahihi, maana ushahidi wote wa kumfungulia mashtaka Rostam Aziz na washirika wake upo!!! Kazi aliyojipa DPP wetu si yake ni ya mawakili wa utetezi kuleta ushahidi kuwa KAGODA ilikuwa imetumwa na kampuni fulani ya nje ambayo itaitwa kutoa ushahidi! Anayoyafanya DPP wetu ni upuuzi na mchezo wa kitoto unaotia kichefuchefu, unaowageuza Watanzania wapumbavu wa mwisho duniani. Hivi, nauliza, wamiliki wa makampuni mengine wako mahakamani kutokana na kwamba DPP ana uthibitisho wa makampuni yote kutoka nje? Aliyemwambia DPP wetu kuwa ONUS OF PROOF katika kesi za jinai inamwangukia yeye, ni nani? Huyu kasoma kweli shule, mbabaishaji au msanii ambaye amewekwa hapo kuwahadaa Watanzania?

  Katika kesi ya Herniman dhidi ya Smith ya mwaka 1938 ambayo iliamuliwa na Mahakama ya Juu ya Uingereza (House of Lords) na uamuzi wake ukapokewa baadaye na Mahakama Kuu ya Tanganyika kama mwongozo katika kesi ya Ali Mohamed Osman dhidi ya DC Hill, msimamo wa kisheria ni kwamba si wajibu wa upande wa mashtaka kuhakiki kila kipengele cha ushahidi kabla ya kuchukua hatua za kushitaki. Nanukuu:
  "... It is not required of any prosecutor that he must have tested every possible relevant fact before he takers action. His duty is not to ascertain whether there is reasonable and probable cause for prosecution. ... there is no obligation to call on the cheat and ask for an explanation in as much as to ask for this may only have the effect of causing material evidence to disappear or to be manufactured ..."

  Na kweli kabisa, anachofanya DPP ni kumruhusu Rostam kutengeneza ushahidi na makampuni ya nje! Kwa sisi wazee tuliokaa ndani ya taaluma ya sheria kwa zaidi ya miaka 50 sasa, tunachokiona ni KIOJA! Ili kumfikisha mtu mahakamani, DPP hahitaji kujiridhisha na ushahidi wote, anachohitaji ni ushahidi kiasi unaojenga "reasonable and probable cause to prosecute". Ushahidi wa aina hiyo, tayari DPP Elieza Feleshi anao!

  Tanganyika Law Society mko wapi? Wanasheria wa Tanzania mko wapi kuiokoa taaluma yenu ambayo sasa inabakwa? Tofauti yenu na laymen iko wapi?
   
 2. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hili la kuchanganya taaluma na siasa tabu sana! Nilishawahi kusema hapo nyuma kwamba baadhi ya hizi office zinaitaji kufanyiwa 'vetting' na Bunge kabla ya kushika hizi nyadhifa. Na tena ziwe kwa mikataba let say miaka 5 then unarudi kupimwa through vetting ...mbona waganda wameweza sisi tunashindwa nini?
   
 3. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Duh, mimi ndio maana sipendi jukwaa la siasa na ninalichukia. Nimesoma hii post najikuta nikianza kupandwa na Moli. Wao wafanye wanavyotaka na kama sisi watu wakawaida ni wajinga hatujui kitu ni kwanini watu wamataifa mengine unakuta wana akili sana, mfano hawa Jewish kwanini? Nakama viongozi wataenda kinyume na sheria na sisi raia wema hatujui sheria tutafanya nini zaidi ya kuangalia?
   
 4. F

  Fataki Senior Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Lakini Mzee Kapelwa, naelewa unaandika kwa abstraction ya juu mno. Naomba suala moja liwe wazi kwa wana JF. Kisheria, onus of proof katika criminal matters iko kwa DPP, lakini si katika stage ambayo Mzee Kapelwa unaielezea na kunukuu authorities, yaani stage ya kuamua whether to prosecute or not. Hapo DPP hana wajibu kabisa wa kuthibitisha, kinachohitajika ni "reasonable and probable cause to prosecute", yaani msingi au sababu za kuridhisha tu kumshitaki mtu, ambazo na mimi nakubali kuwa DPP wetu anazo siku nyingi!
  Vilevile hii ni changamoto kwa wanasdheria wote. Msiangalie tu mambo yanaharibika. Hivi hamwezi kuingilia kati kufanya private prosecution? Huyu ROSTAM mpaka aje kuomba kugombea Urais ndo mshituke?
   
 5. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135


  Jamani Nchi hii inawataalamu wengi mno wa sheria kwanini msitie maguu kwenye hiyo issue kama haiendi sawa?
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Naweza kusema Tanzania hatuna wanasheria wenye kuzijua sheria na kama wapo basi nao ni mafisadi tu!!!
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sheria inapindishwa makusudi kwa baadhi ya watuhumiwa kwa maslahi ya kisiasa ila siku ipo tutaulizana kilichokuwa kinatokea.
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  DPP wa Tanzania si kihiyo wa sheria, bali ni msanii, mbabaishaji, fisadi, mvivu wa kufikiri, hana professional ethics na hana hofu ya Mungu ndani yake
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hebu tusome hizi doc, kama kweli hakuna ushahidi katika Kagoda. Haya yote yalianikwa humu JF...

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wenzako walishakamilisha hilo (quoted in red) ndio maana wanasema sasa hivi......otherwise wangekuambia......."No Comment"
   
 11. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Naomba mamlaka (kesi au sheria ya Bunge) inayosema mshitakiwa jinai ana hatia mpaka atakapojisafisha mahakamani, na yeye ndio ana mzigo kudhihirisha hana makosa, na kazi ya prosecutor ni kutuhumu lolote lile.
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi suala la Kagoda siku hizi watu hupata kigugumizi kujadili, mbona iko kazi mwaka huu!!!!???
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Humu kuna maswali mengi ambayo Bwana Feleshi anatakiwa kuyajibu si kutafuta watu wa nje wamsaidie kujibu. Atoe hoja kama zile alizotumia kuwashitaki kina Rajabu Maranda na Jeetu Patel. Tunajua mahusiano yake na Andrew Chenge na kundi lake na hivyo kuwa vigumu kwake kushughulikia Kagoda na rada, lakini kazi ndio muhimu udugu baadaye bwana Feleshi
   
 14. e

  eddy JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,369
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  Halisi, Chenge na Feleshi wapi na wapi?
   
 15. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Kagoda siyo Rostam, yeye ni chambo tafuteni kwa undani muijue Kagoda
  wakpo watu nyeti wakitajwa tutashangaa na kuona kuwa nchi hii imeisha yumba siku nyingi ndo kwa maana DPP anapata kigugumizi.Advocate Sanze na Benjamin Mwangonda mbona hawatusaidii maana hao ni mashahidi ukiangalia
  hati za usajili wameanguka sahihi zao hapo,ndugu zangu Kagoda ni sirikali.
   
 16. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huku sasa ni kuchanganya madawa kwa makusudi,... Ni nani aliyesema kuwa mtuhumiwa ana hatia mpaka atakapojisafisha mahakamani?... Nani aliyesema kazi ya prosecutor ni kutuhumu lolote lile.

  Kilichosemwa ni "DPP hahitaji kujiridhisha na ushahidi wote, anachohitaji ni ushahidi kiasi unaojenga "reasonable and probable cause to prosecute".

  Tusiharibu mijadala kwa spinning zisizojenga.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,231
  Trophy Points: 280
  Kutokana na hasira za watu dhidi ya ufisadi, wasiopenda utawala wa sheria, wanaona hata kesi za ufisadi ni kupoteza muda. Wangetaka hukumu moja kwa moja.
  Kwa upande wangu, naungana na DPP, anayatumia kikamilifu mamlaka yake aliyopewa na katiba!. Jee mnayajua mamlaka ya DPP?.

  Niliwahi kuandika mahali, kati ya watendaji wote wa serikali, ukimuondoa rais wa JMT kwa madaraka kwa mujibu wa katiba, DPP ndiye mtu wa pili mwenye mamlaka ya ajabu ambayo hata
  Rais hana uwezo wa kuyabeza.

  Ni DPP ndiye mwenye mamlaka ya kukubali kuwa hapa kuna kesi ama la. Na akiamua hakuna kesi, hakuna mamlaka yoyote ya kumuuliza kama rais akiamua kumteua yoyote kushika nafasi yoyote akiona anafaa, hakuna mamlaka ya kuuliza, ni utekelezaji tuu.

  Mamlaka ya DPP, hayaishii kwenye kuendesha mashitaka, bali ana mamlaka nyingine kubwa na ya ajabu inayoitwa 'Nolle Proseque'
  Hii ni mamlaka ya kusema hakuna kesi ya kujibu wawakati wowote kesi ikiwa hatua yoyote kabla ya hukumu, hata kama ushahidi wa hatia ni asilimia 100%. Mamlaka hiyo inatamka DPP akiamua 'nolle prosequi', hakuna mamlaka yoyote ya kumuuliza why, hata rais hawezi!.
  Mtu pekee mwenye mamlaka ya kuruhusu Private 'prosecuition ni huyo huyo DPP, na uamuzi wake ni wa mwisho.

  Angalau Prof.Shivji ameuthibitishia umma kuwa baadhi ya maamuzi ya serikali yanayoelezwa kuwa ni ya mwisho, yanaweza kuwa challenged before the court of law kesi ya Bawata, mbona ya DPP hayaguswi?!.

  Kagoda inajulikana ni nani, pesa zilikokwenda kunajulikana, kazi nzuri ya fedha hiyo inajulikana, na matokeo yapo wazi na yanajulikana. Anachofanya DPP ni kutimiza wajibu wake,anatumia mamlaka yake halali kusema 'No Case to Answer', kwa mujibu wa katiba, mnashangaa nini?. Amevunja sheria gani?.

  Mimi sio mwanasheria, ila tongotongo nimetoa, hawa wanasheria wetu waliobobea wanayajua mamlaka hayo na hawajawahi kuyachallenge, leo ndio wanashangaa?,
  Mbona haya ni ya Musa tuu, subirini ya Farao kwenye kesi ya Yona, Mramba na Mgonja!.
   
 18. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa Pasco. Kunamambo mengi yanahitajika ili kuikomboa Tanzania. Kama hatutaki mapinduzi
   
 19. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakuna cha Feleshi wala nini. Hiki kigugumizi ni kutoka juu! Unafikiri JK angetaka Rostam apelekwe mahakamani angekuwa uraiana hadi leo? Hapa sasa ndio JK atakapoiona nchi chungu. Yaani kawapeleka kundi la Mkapa - kina Mramba - mahakamani lakini hakuna hata mwanamtandao mmoja aliyeguswa! Anawapa watu ndani ya CCM cha kusema
   
 20. Nyemanze

  Nyemanze JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2016
  Joined: Sep 13, 2013
  Messages: 2,124
  Likes Received: 1,402
  Trophy Points: 280
  Aisee kumbe DPP Ana mamlaka makubwa mno
   
Loading...