G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
DPP wa Tanzania amepora uhuru wa mahakama, mahakama nayo imeridhia.
Ni jambo la aibu kuwa DPP anamkamata mtu anamfungulia mashtaka yasiyo na dhamana kisha kila mshtakiwa akipelekwa mahakamani DPP anaiambia mahakama kuwa upelelezi haujakamilika. Aibu yako kubwa wewe DPP usiye hata na chembe ya utu.
Binadamu wa kitanzania anaona ameshateseka vya kutosha kutokana na nguvu uliyonayo juu yake anaamua kukubali yaishe. DPP kuna kupanda na kushuka. Ole wako! Unamkamataje mtu unamfungulia mashtaka hayo yasiyo na dhamana kisha kila uchwao unasema upelelezi bado? Iko wapi nguvu ya mahakama kutetea uhuru wake?
Mahakama ya Tanzania imegeuka kuwa msikilizaji wa anayosema na kuamua DPP, kama nchi tuna tatizo kubwa la udikteta. Narudia kusema tena na tena, huu utawala kuna watu wataandikwa kwenye vitabu maalum ili waje walipie wanayoyafanya kwa sasa! Nasema ole!
Kwa haya yanayoendelea ni bora Tundu Lissu asirudi kwa sasa. Haki ya wakosoaji nchi hii ipo katika mashaka makubwa.