Dpp ..mkurugenzi wa mashitaka.. Elieza feleshi.. Laivu..dk.45>>itv | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dpp ..mkurugenzi wa mashitaka.. Elieza feleshi.. Laivu..dk.45>>itv

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Jun 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkurugenzi ma mashtaka hapa nchini.. Ameelezea na kuainisha utendaji wa kazi na uwajibikaji kisheria.. Ameeleza ulazima wa mwanasheria kujiunga na school of law, uendeshaji wa mashtaka unavyo fanyika kwa umma na jamii.. Jinsi kesi na mashtaka yanavyopokelewa Kwa mapolisi, wanasheria,,
  ameeleza kuhusu uharamia na udhibiti wake katika karne hii ya utandawazi.. Makosa ya kwenye hifadhi yanavyoangaliwa.. Na msimamo wake yeye na watendaji kazi wake katika kusimamia na kurekebisha hiizi changamoto ktk legal sector.. ameeleza mchango wa sheria na umuhim wake katika kuendeleza uchumi kupitia kuondoa utata kwenye mikataba na sera nzuri kupitia nyanja ya sheria..
  haki za msingi za mshtakiwa na mshitaki ameeleza.. Mashiko yake kupitia tuhuma, mazingira ya kesi, mashahd, ushaid, vielelezo.. Kulingana na hivo mahakama husema mtu anayo kes ya kujib au la? Na amri na uamuzi wa mahakama kulingana na kesi husika, na kuna vipimo vinavyo angaliwa mpaka kesi kufikishwa mahakamani.. Na mtu hukata rufaa kama amerizika na maamuz au la? kulingana ngazi ya mahakama ambapo maamuz yametolewa! na jukum la kikosi chake cha kuongoza mashtaka ni lazima kumlinda shahidi..na kumuongoza shahd kulingana na mujibu na mipaka ya sheria Na shahid anapewa fursa zote kueleza ushahid na mazingira na kulindwa..
   
 2. B

  Bob G JF Bronze Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Takukuru wanailalamikia ofisi yake kwamba inachelewesha maamuzi na inafuta kesi nyingi za rushwa, mi nataka angeulizwa kama Takukuru wanaamini zinzushahidi wa kutosha DPP anatupilia mbali
   
 3. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ameongeza kuwa kesi zote ambazo ziko mahakamani wanazisimamia na kuhakisha kuwa haki inapatikana na wenye hatia wana wekwa kitimoto! Na AMEOMBA JAMII NA UMMA UIAMINI OFISI YAKE NA KWAMBA WAMEJIPANGA.. KUWASHUHURIKIA WANAO HUJUM UCHUMI NA KUVUNJA..
   
 4. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  amewaonya waandishi wa habari kuandika habari nusu nusu bila kupeleleza. . Na amesema kuwa WITO WAKE ANAWAPENDA SANA WADAU.. NA AMEOMBA USHIRIKIANO NA WATENDAJI WENGINE SERIKAKINI NA KWENYE MASHRIKA BINAFSI..
   
 5. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  amesema kuwa pesa si kinga ya kuepuka hukumu na NA KUWA PESA HAIWEZI KUNUNUA HAKI...NA HAKUNA MTENDAJI ALIYEJUU YA SHERIA NA AMESEMA KUWA WANANCHI WAKIAMUA KUTAFUTA HAKI WATAIPATA.. NA TUENDELEE KUBORESHA MAZINGIRA YA HAKI.. NA UPATIKANAJ WAKE KWA WATANZANIA WOTE.. KWA UJUMLA.
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Eliezer Feleshi, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), aache kudanganya watu kwa sababu ni moja kati ya vigogo wanaotuhumiwa katika kashfa ya kuingilia kesi ya mauaji ya watu wanne waliouawa katika Kijiji cha Tegeruka Wilaya ya Musoma Vijijini Aprili, 2009 wakidaiwa kuwalinda watuhumiwa hao ambao ni viongozi wa chama tawala CCM.

  Habari za uhakika zinaeleza kuwa kutokana na shinikizo la vigogo hao akiwamo ofisa wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DPP), wamesababisha kesi iliyokuwa ikiwakabili watu hao ambao pia ni madiwani watatu na Mwenyekiti wa CCM wa Kata, kufutwa na DPP Eliezer Felishi.

  Februari, 15 mwaka huu, Feleshi alifuta kesi hiyo iliyokuwa Mahakama Kuu mjini Musoma kwa madai kwamba kuna utata katika kesi hiyo, hivyo anarudisha jalada polisi ili waanze kulifanyia uchunguzi upya. Mtuhumiwa moja ambaye ni diwani inasemekana ni ndugu wa ofisa wa ngazi za juu katika ofisi ya DPP.

  Kwa habari zaidi soma hapa;

  CCM imekuwa kimbilio la wahalifu wakiwemo wezi, wauaji na mafisadi kwa sababu watu kama Eliezer Feleshi wameamua kusaliti taaluma zao kwa sababu ya ulafi, unafiki na tamaa ya mali, shame on him!
   
 7. p

  plawala JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuna ofisi iliyosaidia sana kukua na kushamiri rushwa kubwakubwa ni ya DPP chini ya Feleshi
   
 8. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alivaa KOTI la mtoto wake kama ndiye alikuwa anahojiwa kwenye kipindi hicho.
   
 9. m

  mamajack JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mie simwamini,maana kesi zinachukua mda mrefu sana,nahisi kuna rushwa iliyokisiri kwenye office hii.
   
Loading...