Dpp Kuridhia Mashtaka Dhidi Ya Vigogo Kesi Za Pccb?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
29,374
52,531
SOURCE: www.raiamwema.co.tz

Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

Mwandishi Wetu Machi 26, 2008

SERIKALI inakamilisha taratibu za kuwashitaki mawaziri wa zamani wawili wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Raia Mwema imefahamishwa.

Habari za uhakika zilizopatikana na kuthibitishwa na maofisa waandamizi wa Serikali zinaeleza kwamba mawaziri hao (majina tunayo) walihojiwa na vyombo vya dola kwa mara kadhaa na sasa mchakato wa kuwashitaki uko katika hatua za mwisho.

Wote wawili walipata kuongoza Wizara ya Fedha, chini ya utawala wa Rais Benjamin Mkapa na mmoja aliteuliwa katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete kabla ya kuachwa katika mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni.

Kwa mujibu wa habari hizo, mmoja amekuwa akichunguzwa kufanya maamuzi kadhaa yenye utata, ikiwamo kutoa misamaha ya kodi ambayo kisheria hakuwa na mamlaka nayo akiwa anatuhumiwa kuvuka mipaka ya mamlaka yake katika kutoa misamaha.

Mwingine anaelezwa kuchunguzwa kuhusika na maamuzi kadhaa akiwa Waziri katika Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, lakini haikuweza kufahamika mara moja ni eneo gani hasa ambalo mwanasiasa huyo mstaafu amechunguzwa.

Mawaziri wote wawili wanatajwa sana kuwa karibu na Mkapa katika masuala kadhaa ya kiutendaji na hata katika masuala kadhaa binafsi na inaelezwa kwamba baadhi ya mambo yaliyochunguzwa yanaweza kumgusa moja kwa moja Rais huyo mstaafu.

Mkapa anatajwa kuhusika moja kwa moja na mradi mkubwa wa mkaa wa mawe wa Kiwira, akiwa na maslahi binafsi katika kampuni ya Tanpower Resources, ambayo iliuziwa hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Limited iliyokuwa ikimilikiwa na serikali kabla ya ubinafsishaji.

Pamoja na Mkapa kutajwa katika maeneo mengi, bado kumekuwa na maelezo ya kutaka “aachwe apumzike”, huku baadhi wakitumia kinga ya kikatiba ambayo rais mstaafu anakuwa nayo pamoja na kupingwa na baadhi ya wanasheria.

Haikuweza kufahamika mara moja mawaziri hao walichunguzwa katika maeneo gani mengine zaidi lakini kuna uhakika kwamba uchunguzi huo uligusa pia misamaha ya kodi iliyofanywa katika kipindi mawaziri hao wakiwa madarakani.

Miongoni mwa mambo ambayo yaliguswa ni mkataba kati ya Serikali na wakaguzi wa Alex Stewarts waliokuwa wakifanya ukaguzi wa mapato katika sekta ya madini.

Eneo jingine tata ambalo linatajwa kuguswa ni mkataba wa Serikali na kampuni ya Tanzania International ContainerTerminal (TICTS) wa kukodisha eneo la bandari ya Dar es Salaam, mkataba ambao hadi sasa umekuwa ukipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa sekta ya bandari.

Hata hivyo, mawaziri wote wawili walikuwa ama na mahusiano ya karibu na Mkapa kikazi na hata kibinafsi mambo ambayo yanazidi kuonyesha ni jinsi gani Serikali italazimika kumtaja ama kumgusa rais huyo mstaafu katika uchunguzi na hatimaye mashitaka.

Ikiwa wanasiasa hao watafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Kikwete kuwashitaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, akituhumiwa kuiibia Serikali Sh bilioni 2 kutokana na ununuzi wa jengo la ubalozi, Rome.

Hata hivyo, kiu kubwa ya Watanzania kwa sasa iko kwa watu wanaotajwa kuhusika katika upotevu wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika na mradi tata wa umeme wa dharura wa Richmond Development LLC.

Pamoja na Rais Kikwete kuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, kulikuwa na kazi iliyokwisha kuanza kufanywa na vyombo hivyo ndani ya BoT na maeneo mengine nyeti kiuchumi.
 
Well,

Naona hii movie imeanza mapema sana. Asante Jokakuu kwa story hii ya raia mwema. Niliiona juzi kwenye wire nikadhani haitachapishwa. This is too good to be true.... mzee wa nyasi akiwekwa ndani basi itakuwa bonge la move!
 
Mwafrika wa Kike,

..this is a very interesting development. lakini watamshitaki vipi Daniel Yona na kumuacha Ben Nkapa "akipumzika??"
 
ni dakika ya 75 ndugu msikilizaji naona timu ya "Muungwana" inaanza kufanya mambo yake hapa!. kocha mchezaji "Muungwana" naona ameanza kuichachafya ngome ya mafisadi. kama hali ikiendelea namna hii Watanzania tunaweza kusawazisha hili bao.
ila mpaka sasa mafisadi moja waungwana bila. hebu kwanza twende kwa wadhamini wetu.....
 
Mwafrika wa Kike,

..this is a very interesting development. lakini watamshitaki vipi Daniel Yona na kumuacha Ben Nkapa "akipumzika??"

That's why I said kuwa hii movie itakuwa bonge la hit na kuna uwezekano mkubwa ikaongozwa kwenye box office this weekend. Ukishamkamata Yona basi ni lazima Mkapa naye afuate au utoe maelezo kuwa ni kwa nini unamwacha Mkapa!

Tik tak tik tak tik tak ......kamata pop corn na mbege for this one!
 
Mramba na Yona bila Mkapa ni zip zero.

Inaonekana kama danganya toto vile, halafu juu chini nyingi, kukosekana ushahidi na technicalities, mwisho watu wanakuwa absolved.

Kama kweli wako serious wamshitaki na Mkapa naye.
 
That's why I said kuwa hii movie itakuwa bonge la hit na kuna uwezekano mkubwa ikaongozwa kwenye box office this weekend. Ukishamkamata Yona basi ni lazima Mkapa naye afuate au utoe maelezo kuwa ni kwa nini unamwacha Mkapa!

Tik tak tik tak tik tak ......kamata pop corn na mbege for this one!

....presidential immunity!
 
Kwa wanao cite kutomshitaki Mkapa kwa sababu ya presidential immunity.

Presidential immunity ina apply kwa vitu vilivyofanywa katika presidential capacities, siyo personal capacities.

Kwa hiyo presidential immunity ina apply kwa Mkapa kama mtu atataka kumshitaki juu ya mauaji ya January 27 kule Zanzibar, kwa sababu alitoa order kama rais wa Jamhuri ya muungano citing some national security issues.

Lakini kama alichukua Kiwira Mines, in his personal capacity kama Benjamin William Mkapa wakati akiwa rais, presidential immunity hai apply kwa sababu aliyechukua Kiwira pale si President of The United Republic of Tanzania, bali ni Benjamin William Mkapa.

Kwa hiyo katika kumshtaki Mkapa kuhusu ufisadi binafsi hakuna issue ya Presidential immunity.
 
I agree with you 100%. Kama Mkapa angejiandikisha Kiwira kama "The President of United Republic of Tanzania" then angejiepusha na madai haya, in the way that angeweza ku-apply presidential immunity kwenye issue aliyoitenda kwenye capacity kama President of the United Republic.

Kama kweli tuko-serious na suala hili basi Mkapa inabidi awe suspect (mshtakiwa) number one. Yeye kama Rais alienda kinyume na kiapo chake kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.. kwamba atalitumikia Taifa kwa UADILIFU... The thing that he never did... He should pay for his actions!!! Hakuna msamaha kwenye hili.. Jizi ni jizi tuu..
 
Hii haina nguvu kama alifanya ufisadi na ushahidi uko bwelele kwamba jamaa alikuwa busy kuwafisadi Watanzania.

..Bubu, Naungana na wewe. Biashara alizofanya Ben ikulu hazikuwa ni sehemu ya majukumu ya raisi wa nchi. Alifanya biashara hizo kama Ben. Ushahidi upo, hiyo Benk ya ANBEN siyo ya serikali. Ni mali yake binafsi. Kikwete anatakiwa kuanza na Ben wakati wengine wanapaka sabuni kichwani, ili kurahisisha kazi ya perma sharp.
 
Hii stori ni nzuri lakini sidhani kama serikali itakuwa na "balls" za kuwafungulia mashtaka hao waliotajwa. Kama issue ya kurudisha pesa za BoT tu na kuwataja owners wa hizo kampuni linakuwa suala la kiini macho, sembuse kuwafungulia mashtaka watu wa mkono wa kuume wa Mkapa. I doubt it. Najua serikali ya JK iko under intense pressure kutoka kwa donors kuwachukulia hatua wote wale waliohusika na ubadhirifu ma ma-bilioni ya shilingi otherwise donors watasitisha mchango wao kwenye budget yetu.
Tatizo la serikali ya mh. Kikwete ni kwamba japokuwa wanawajua wabadhirifu na mafisadi, hawana nguvu za kwenda kuwakamata na kuwafungulia mashitaka kwa vile ukiangalia sana...hata wenyewe sio wasafi sana. This is just my personal opinion.
 
Mimi sijui kabisa sheria za nchi na katiba zinasemaje, labda niwasiliane na Mh Mchungaji Mtikila kuona kama kuna uwezekano wa kumfungulia keshi Ben Mkapa kuvunja katiba kwa kufanya ikulu ni nyumba ya biashara, je raisi mtaafu anaweza simama kizimbani, nipeni ufafanuzi JF
 
Hii issue mbona ilishajidiliwa siku nyingi. Katiba inatoa "immunity" kwa raisi anapofanya makosa katika maamuzi yanayohusu majukumu ya utawala. Sasa biashara si sehemu ya majukumu ya raisi. Katiba ya nchi haina kipengele kinachomruhusu raisi kuanzisha benki anapokuwa ikulu. Kwa hivi, Ben Anabanwa na hicho kipengele. Na hata Mh Kikwete anafahamu hilo. Ndio maana akasema mwacheni mzee wa watu apumzike.
 
Hivi Bob Makani si alisema atamburuza Mkapa kortini? Amefanya chochote kuhusu hili au ndo alikuwa anamtishia mtu mzima nyau?
 
Hii issue mbona ilishajidiliwa siku nyingi. Katiba inatoa "immunity" kwa raisi anapofanya makosa katika maamuzi yanayohusu majukumu ya utawala. Sasa biashara si sehemu ya majukumu ya raisi. Katiba ya nchi haina kipengele kinachomruhusu raisi kuanzisha benki anapokuwa ikulu. Kwa hivi, Ben Anabanwa na hicho kipengele. Na hata Mh Kikwete anafahamu hilo. Ndio maana akasema mwacheni mzee wa watu apumzike.

Wabeja sana Nsumba Ntale, Nadhani ni wakati sasa umefika kuwa na mwamko, wa kuwafungulia viongozi wazembe na wavunja sheria ili kutoruhusu abuse of power wanakuwa nayo...
 
SOURCE: www.raiamwema.co.tz

Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

Mwandishi Wetu Machi 26, 2008
Hata hivyo, mawaziri wote wawili walikuwa ama na mahusiano ya karibu na Mkapa kikazi na hata kibinafsi mambo ambayo yanazidi kuonyesha ni jinsi gani Serikali italazimika kumtaja ama kumgusa rais huyo mstaafu katika uchunguzi na hatimaye mashitaka.

Ikiwa wanasiasa hao watafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Kikwete kuwashitaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, akituhumiwa kuiibia Serikali Sh bilioni 2 kutokana na ununuzi wa jengo la ubalozi, Rome.

6.jpg
 
Wabeja sana Nsumba Ntale, Nadhani ni wakati sasa umefika kuwa na mwamko, wa kuwafungulia viongozi wazembe na wavunja sheria ili kutoruhusu abuse of power wanakuwa nayo...

mkatubyolelage miso tulibana ba tanzania habise yaya batulija tulebana ba tanzania, yeah, tatizo linakuja ni kwamba katika hizi issue zote CCM inahusika kwa namna moja au nyingine, if any action has to be taken should come from outsiders, lakini ndani ya ccm msitegemee kitu, sisi kama watanzania tutafute namna ya kumshitaki mkapa na wenzake.
 
immunity ipo kama ulifanya kosa kwa lengo la kulinufaisha taifa au kama ulifanya kosa ukiwa kwenye harakati za kufanya jambo linalohusu taifa. Hakuna immunity kama akifanya kosa la wizi wa mali za umma, au kama aliabuse ofisi kwa manufaa yake binafsi, yasioy na connection hata kidogo na maslahi ya taifa. Kuna msingi mzuri tu wa kumshikisha adabu BWM, lakini timing siio nzuri!
Akinyonyolewa Mramba, Chenge, na wengine wengine then unaweza ukakamata Ben. Lakini hata hivyo tukumbuke kuwa Ben sio mwizi aliabuse ofisi, hakuiba hela zetu ila aliitumia Ikulu kufanya biashara, hapa kuna tofauti kidogo. We can put him aside for a while!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom