assadsyria3
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 6,904
- 4,050
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amezidi kumngangania Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare (pichani) baada ya kuanza mchakato wa kupinga dhamana yake.
Lwakatare, ambaye anakabiliwa na kesi ya jinai pamoja na mwenzake Ludovick Joseph Rwezaura katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, aliachiwa huru kwa dhamana Juni 11, mwaka huu, baada ya kusota rumande kwa miezi miwili na siku 23.
Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Aloyce Katema anayesikiliza kesi hiyo,alimwachia huru kwa dhamana Lwakatare, baada ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam kuwafutia mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakiwabili.
Hata hivyo DPP amewasilisha katika Mahakama ya Kisutu taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama Kuu, kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kumpa dhamana. Mbali na taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa kupinga dhamana yake, DPP pia tayari ameshawasilisha katika Mahakama ya Rufani, maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia mashtaka ya ugaidi.
Katika maombi hayo, DPP anaiomba mahakama hiyo iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotolewa na Jaji Lawrence Kaduri, kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya ugaidi soma mwananchi 4details