DPP kukata rufaa kupinga dhamana ya Lwakatare Mahakama Kuu

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) amezidi kumng’ang’ania Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare (pichani) baada ya kuanza mchakato wa kupinga dhamana yake.

Lwakatare, ambaye anakabiliwa na kesi ya jinai pamoja na mwenzake Ludovick Joseph Rwezaura katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, aliachiwa huru kwa dhamana Juni 11, mwaka huu, baada ya kusota rumande kwa miezi miwili na siku 23.

Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Aloyce Katema anayesikiliza kesi hiyo,alimwachia huru kwa dhamana Lwakatare, baada ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam kuwafutia mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakiwabili.

Hata hivyo DPP amewasilisha katika Mahakama ya Kisutu taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama Kuu, kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kumpa dhamana. Mbali na taarifa hiyo ya kusudio la kukata rufaa kupinga dhamana yake, DPP pia tayari ameshawasilisha katika Mahakama ya Rufani, maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia mashtaka ya ugaidi.

Katika maombi hayo, DPP anaiomba mahakama hiyo iitishe majalada ya kesi hiyo na kuchunguza uhalali wa uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotolewa na Jaji Lawrence Kaduri, kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya ugaidi soma mwananchi 4details
 
DPP anataka CDM kiwe chama cha kigaidi au kusudio hili lina mana gani?
 
Tunaanza na Mungu tutamaliza na Mungu, tena awahi siyo kutishia nyau, mbuzi. Huyo
 
Kina Kinana siyo wanasheria ila wanawapelekesha puta mpaka mnaharibu dhana nzima ya mashitaka. DPP tumia taaluma yako kufanya kazi, usifate shinikizo la maelekezo.
 
DPP anakuwa na chama sijawahi ona,naomba katiba mpya ije mapema hatuwezi kuwa uonzo kama huu
 
Hivi kweli huyu Feleshi (DPP) tunayemjua siku zote naye amekubali kuingia kwenye mkumbo wa kutumiwa kama tambara la kudekia na kulamba miguu ya watawala na wajinga wengine kama nape na mwigulu.
 
DPP ni cheo cha mezani au competition job? tukishajua hilo tunaweza endelea na mada.
 
DPP anakuwa na chama sijawahi ona,naomba katiba mpya ije mapema hatuwezi kuwa uonzo kama huu

Dr. Feleshi ni mwadilifu na mchaji wa Mungu sana, hana chama, anajua anachokifanya tumwache maadam hatujui kilichomfikia mezani huenda anajua anachokifanya.
 
Sasa ofisi ya mwanasheria imekuwa ofisi ya kukata rufaa.Dhamana imetolewa na mahakama na dhamana siyo mwisho wa kesi kama wanaona mahakama haikutenda haki si wakamchukuwe Lwakatare wakamfunge kabisa ili ijulikane kuwa wao ndiyo wenye uwezo wa kuamuwa kila jambo.
 
Back
Top Bottom