DPP, IGP na polisi kwa ujumla mmelitengenezea sifa mbaya taifa kwa kesi ya Mbowe

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
309
1,000
Kwakweli toka moyo wangu na kwa haki ya Mungu, Polisi hii kesi imewaumbua vibaya sana mpaka hata polisi wengine walioko nje wanashangaa sana. Mashahidi upande wenu wamejichanganya kwa kila kitu, wametofautiana mpaka kuna mahali hata raia wa kawaida anajua kuna mambo ni ya uongo wa wazi.Hivi mlifikiri mkimtuhumu na kumfunga Mbowe ni kuiokoa CCM na serikali dhidi ya harakati zake Mbowe za kudai katiba mpya na kuua upinzani ? Au mliwaza kitu gani? Hamkua mkijipanga?

Mpaka sasa hata raia Mjinga akiasi gani anaelewa kabisa hukumu ya kesi hii hata ikiwa kinyume cha matarajio ya wengi, yaani kesi inayoitwa kua ni ya Ugaidi utafikiri ni kesi ya kawaida ya unyang'anyi. Na niwaambie siyo kwamba kesi ya Mbowe na wenzake 3 inatetewa na mawakili Mahiri sana au laah, au mawakili wa serikali ni Vilaza, big NO! Kesi hii haileweki iko miguu chini au juu yaani mpaka hata washtakiwa wana confidence na ndio maana mnaona Shahidi wa jana yule Komandoo Adamoo alijibu kwa kujiamini sana.

Kiukweli kabisa mlitakiwa kupima, Kwanza Mbowe chama chake ni kikubwa na cha pili kwa wingi wa wanachama Tz ambao ni milion 6.5 nyuma ya CCM yenye wanachama milion 8. Kiongozi wa Chama kikubwa huwezi kumshtaki kirahisi rahisi hivyo kwa jambo usilokua na uhakika nao,Chukueni mfano wa Raila Odinga wa Kenya alivyosumbuliwa na MOI na haikusaidia kitu , na isitoshe Mbowe alikua Kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani na hana record yeyote ya uhalifu.

DPP na Polisi nilitakiwa mpime kwanza kua Mbowe alikamatwa akiandaa Kongamano la kudai katiba mpya, neno "Katiba" liko kwenye vichwa vya watu wengi wanaojitambua, liko kwenye vichwa vya wanaharakati wote na pia lipo kwenye mataifa yenye taasisi kubwa za haki za binadamu. Msigetegee hili suala likakosa attention ya ndani na nje ya nchi. Kwakweli kama mlitagemea kulinda maslahi taifa kwa jambo hili mmeingia katika mkwamo kweli kweli hata mkililazimisha.

Etii, yaani kesi inakua na attention kubwa ya watanzania na walioko ndani na nje ya nchi kuliko hata safari ya Mama huko nje na hotuba yake? Kuna kitu hakipo sawa lazima tukubaliane hapa. Tukiendekeza siasa hizi siasa mbovu hivi nawaambieni CCM haina hata miaka 10 mbeleni na huenda hiyo ikawa mingi sana,na mtayakumbuka maneno haya.

USHAURI WANGU KWENU;
Lipeni hadhi taifa hili, futeni kesi hii mpaka hapa ilikofikia kwa ushahidi uliotolewa tayari ni kama imeisha. Ukiangalia hata mashahidi wa upande wa mashtaka kwa sasa hawana jipya zaidi ya kujikanganya tu na huenda wakaharibu zaidi mbeleni wakaendelea kuwakwaza Watanzania. Toeni onyo kiaina kama kuzuga tu lakini mtakuwa mmeshamaliza mchezo hamjachelewa.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
16,506
2,000
... in short hicho ndicho kinachoitwa matumizi mabaya ya madaraka! Mnatumia nafasi zenu za kimadaraka, mnatumia resources za nchi - fedha, mahakama, polisi, muda, mawakili, n.k. dhidi ya wapinzani wenu ambao wako kikatiba na kisheria ili mtawale bila bughudha wala uchafu wenu kuwekwa hadharani! Hapo ndipo CCM ilipofikia kwa sasa.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,554
2,000
Hawakujua. Imebakifaya
Na hawakutegemea kama ingekuja kuwa watu wana uwezo wa kurekodi mwenendo mzima wa kesi , hiyo ndio imewavua nguo kabisa kwani hata aliyeko nyumbani anajua nini kiliendelea mahakamani!!na hilo linatoa picha kuwa kesi nyingi sana watu wanabambikwa tu!!MI POLISI INARUKA NA KUKANYAGANA!!wakaona bora mashahidi waishie hao watatu tu kwani ndio waliokuwa wanawategemea na wamekula za uso je hao wengine si ndio wangezimia kizimbani?na jaji yuko fair kabisa, hadi sasa
 
Cathelin

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
1,209

Me nimefurahi Mbowe kupewa kesi,,hii itakuwa fundisho kwa polisi kuwasingizia wapinzani kesi za kubumbu,,yaan hii kesi imeback-fire kwa polisi kinoma
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
16,506
2,000
...
Kesi hii haileweki iko miguu chini au juu yaani mpaka hata washtakiwa wana confidence na ndio maana mnaona Shahidi wa jana yule Komandoo Adamoo alijibu kwa kujiamini sana.
...
Komandoo Adamoo kanyoonsha maelezo kama rula! Imagine mtu kaletwa kutoka mahabusu alimowekwa zaidi ya mwaka hana hili wala lile ghafla mahakamani Serikali inaondoa mashahidi wake waliosalia; ghafla mtuhumiwa anaieleza mahakama kwamba atajitetea mwenyewe tena wakati huo huo bila kutarajia wala maandalizi yoyote. On the spot anapanda kizimbani na kuanza kutiririka ushahidi wa tukio zima!

Imepata kuandikwa; waovu hukimbia wasipofuatwa na mtu ila wenye haki ni jasiri kama simba! Ndicho kilichotokea jana kwenye ushahidi wa Komandoo Adamoo na pengine kwa watuhumiwa wengine waliosalia mbele ya safari. Ukweli hauna maelezo ya ziada tofauti na uongo konakona nyingi.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,744
2,000
Me nimefurahi Mbowe kupewa kesi,,hii itakuwa fundisho kwa polisi kuwasingizia wapinzani kesi za kubumbu,,yaan hii kesi imeback-fire kwa polisi kinoma
Imeandikwa Katika Biblia takatifu, kitabu cha Mithali 14:34 nanukuu "Haki huinua Taifa na dhambi ni aibu ya watu wote" mwisho wa kunukuu.

Hapo ndipo tulipofika kama Taifa, yaani sielewi hawa Polisi, Wana akili gani??

Kwa kuwa hata Rais aliwapa onyo, kuhusu mtindo wao waliouzoea wa kuwabambikia kesi, raia wasio na hatia

Hata hivyo sikio la kufa, halisikii dawa!
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,554
2,000
Komandoo Adamoo kanyoonsha maelezo kama rula! Imagine mtu kaletwa kutoka mahabusu alimowekwa zaidi ya mwaka hana hili wala lile ghafla mahakamani Serikali inaondoa mashahidi wake waliosalia; ghafla mtuhumiwa anaieleza mahakama kwamba atajitetea mwenyewe tena wakati huo huo bila kutarajia wala maandalizi yoyote. On the spot anapanda kizimbani na kuanza kutiririka ushahidi wa tukio zima!

Imepata kuandikwa; waovu hukimbia wasipofuatwa na mtu ila wenye haki ni jasiri kama simba! Ndicho kilichotokea jana kwenye ushahidi wa Komandoo Adamoo na pengine kwa watuhumiwa wengine waliosalia mbele ya safari. Ukweli hauna maelezo ya ziada tofauti na uongo konakona nyingi.
Siku zote ukiwa muongo lazima uwe na kumbukumbu!!hao watesi walikuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu!!!?na hawakutegemea kama kesi ingekuwa wazi kiasi hicho!!!ki ukweli wamedharirika sana!!kama hata kitendea kazi chao kikubwa PGO, imeonekana hawana uelewa nayo bali wanafanya kazi ki mazoea tu.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
9,038
2,000
Kwakweli toka moyo wangu na kwa haki ya Mungu, Polisi hii kesi imewaumbua vibaya sana mpaka hata polisi wengine walioko nje wanashangaa sana. Mashahidi upande wenu wamejichanganya kwa kila kitu, wametofautiana mpaka kuna mahali hata raia wa kawaida anajua kuna mambo ni ya uongo wa wazi.Hivi mlifikiri mkimtuhumu na kumfunga Mbowe ni kuiokoa CCM na serikali dhidi ya harakati zake Mbowe za kudai katiba mpya na kuua upinzani ? Au mliwaza kitu gani? Hamkua mkijipanga?

Mpaka sasa hata raia Mjinga akiasi gani anaelewa kabisa hukumu ya kesi hii hata ikiwa kinyume cha matarajio ya wengi, yaani kesi inayoitwa kua ni ya Ugaidi utafikiri ni kesi ya kawaida ya unyang'anyi. Na niwaambie siyo kwamba kesi ya Mbowe na wenzake 3 inatetewa na mawakili Mahiri sana au laah, au mawakili wa serikali ni Vilaza, big NO! Kesi hii haileweki iko miguu chini au juu yaani mpaka hata washtakiwa wana confidence na ndio maana mnaona Shahidi wa jana yule Komandoo Adamoo alijibu kwa kujiamini sana.

Kiukweli kabisa mlitakiwa kupima, Kwanza Mbowe chama chake ni kikubwa na cha pili kwa wingi wa wanachama Tz ambao ni milion 6.5 nyuma ya CCM yenye wanachama milion 8. Kiongozi wa Chama kikubwa huwezi kumshtaki kirahisi rahisi hivyo kwa jambo usilokua na uhakika nao,Chukueni mfano wa Raila Odinga wa Kenya alivyosumbuliwa na MOI na haikusaidia kitu , na isitoshe Mbowe alikua Kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani na hana record yeyote ya uhalifu.

DPP na Polisi nilitakiwa mpime kwanza kua Mbowe alikamatwa akiandaa Kongamano la kudai katiba mpya, neno "Katiba" liko kwenye vichwa vya watu wengi wanaojitambua, liko kwenye vichwa vya wanaharakati wote na pia lipo kwenye mataifa yenye taasisi kubwa za haki za binadamu. Msigetegee hili suala likakosa attention ya ndani na nje ya nchi. Kwakweli kama mlitagemea kulinda maslahi taifa kwa jambo hili mmeingia katika mkwamo kweli kweli hata mkililazimisha.

Etii, yaani kesi inakua na attention kubwa ya watanzania na walioko ndani na nje ya nchi kuliko hata safari ya Mama huko nje na hotuba yake? Kuna kitu hakipo sawa lazima tukubaliane hapa. Tukiendekeza siasa hizi siasa mbovu hivi nawaambieni CCM haina hata miaka 10 mbeleni na huenda hiyo ikawa mingi sana,na mtayakumbuka maneno haya.

USHAURI WANGU KWENU;
Lipeni hadhi taifa hili, futeni kesi hii mpaka hapa ilikofikia kwa ushahidi uliotolewa tayari ni kama imeisha. Ukiangalia hata mashahidi wa upande wa mashtaka kwa sasa hawana jipya zaidi ya kujikanganya tu na huenda wakaharibu zaidi mbeleni wakaendelea kuwakwaza Watanzania. Toeni onyo kiaina kama kuzuga tu lakini mtakuwa mmeshamaliza mchezo hamjachelewa.
Mbowe na upinzani ndio kwanza wanaimarika na kuwa maarufu zaidi ndani na nje ya nchi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom