DPP Biswalo Mganga unalazimika kuwajibika kujiuzulu baada ya kumtoa "mahabusu" Nusrat Hanje gerezani akawe ghafla Mbunge

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni.

Ndivyo ninavyolazimika kuianza "thread" yangu kutokana na sakata hili la kumwachia mahabusu Nusrat Hanje kinyume cha sheria na taratibu za nchi hii.

Kama kweli nchi yetu inaendeshwa kwa utawala bora, DPP Biswalo Mganga analazimika kujiuzulu kutokana na sakata linaloendelea kumtoa mahabusu, Nusrat Hanje, kinyume cha sheria, usiku wa tarehe 23/11/2020, kwa lengo moja tu la "kumuwahisha" ili aende kuapishwa Bungeni Dodoma kesho yake ya tarehe 24/11/2020.

Wewe uliwahi kuona wapi, Mahabusu yeyote hapa nchini anatolewa gerezani usiku, bila kwanza kupitia kwenye Mahakama iliyomuhukumu aende rumande kwenye gereza hilo na kuifunga dhamana yake kwa siku 133 mfululizo?

Ndivyo ilivyotokea kwa Mahabusu Nusrat Hanje, Kiongozi wa Bavicha Taifa, baada ya kutuhumiwa na Jeshi la Polisi nchini, kufanya mkusanyiko usio halali, hapo mwezi June mwaka huu.

Tunamuomba Biswalo Mganga aueleze Umma wa watanzania, kulikuwa na udharula gani, hadi "azitengue" sheria za nchi hii na kulazimisha kumtoa Mahabusu, Nusrat Hanje, kisiri siri, tena usiku wa tarehe 23/11/2020?

Huyo Nasrat Hanje aliamka akiwa rumande tarehe 23/11/2020 akiwa hajui hili wala lile, baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na Ndugu, Jamaa, Viongozi wa Chama chake cha CHADEMA pamoja na wanasheria wao kufanya juhudi kubwa ya kumtoa rumande kwa siku 133 bila mafanikio yoyote.

Ghafla jioni hiyo ya tarehe 23/11/2020 ndipo ilipokuja amri kutoka kwa DPP, Biswalo Mganga, kwa Mkuu wa gereza alilokuwemo kuwa atolewe gerezani humo na yeye ni mtu huru kuanzia dakika ile!

DPP anaelewa fika "procedure" za kufuata kabla ya mahabusu yeyote kuachiwa Huru na utaratibu huo ni pamoja na huyo mahabusu kuachiwa majira ya asubuhi hadi mchana pekee na ipelekwe taarifa kwenye mahakama aliyotuhumiwa na ipate kibali kwa "kusainiwa" na Hakimu mwenye kusikiliza kesi hiyo.

Utaratibu huo haukufuatwa kabisa, kwa kuwa "mahabusu" huyo aliachiwa majira ya saa 1.30 jioni ya tarehe hiyo ya 23/11/2020 na taarifa yake haikupelekwa kwa Hakimu anayesikiliza kesi yake ili "aisaini" kuidhinisha kutoka kwake huko Mahabusu.

Lakini kilichobainika baadaye ni kuwa amri hiyo ya kumwachia "mahabusu" huyo Nusrat Hanje na DPP, Biswalo Mganga, kuamua kwa makusudi kuvunja utaratibu mzima wa kuachiwa kwa Mahabusu huyo ni kwa sababu tu ili awahi kwenda apishwa Ubunge wa viti maalum vya Chadema, kesho yake ya tarehe 24/11/2020 mjini Dodoma!

Kwa "blunder" hii kubwa iliyofanywa na DPP Biswalo Mganga, wananchi tunaomba ajiuzulu wadhifa wake wa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini kwa kutofuata taratibu za kumwachia huru huyo "mahabusu" Nusrat Hanje, kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa taratibu na sheria, ambazo kwa makusudi, DPP Biswalo Mganga hakutaka kuzifuata, katika sakata hilo la kumwachia mahabusu huyo, Nusrat Hanje.

Kwa mtu ambaye Taifa hili lilimwamini sana kuwa atatekeleza wadhifa wake huo kwa uaminifu mkubwa na kwa kufuata sheria za nchi kwa hii "blunder" kubwa aliyoifanya, analazimika kuwajibika kujiuzulu ili alinde heshima yake na alinde heshima ya Rais ambaye alimwamini kwa kumpa wadhifa huo mkubwa sana wa utumishi wa Umma, akiwa ni Mwendesha Mashitaka Mkuu wa nchi hii

Kama atagoma kujiuzulu tunamwomba Rais Magufuli ambaye ndiye aliyemteua kwenye nafasi hiyo amfukuze kazi mara moja, kwa kuwa kwa kitendo chake hicho amelisababishia Taifa hili aibu na fedheha kubwa ndani ya nchi na hata kwenye Jumuia ya Kimataifa.
 
Wako juu ya sheria hao usitegemee hilo mkuu katiba kwao ni takataka haiheshimiwi wala hatuna cha kuwafanya kwa sasa labda mpaka tutapojitambua na kuchukua hatua dhidi ya hawa wavunja katiba mchana kweupe.
Sasa inakuwa na maana gani kuapishwa huku umeshika Katiba na kuahidi kuitii na kuiheshimu Katiba hiyo kabla ya kukabidhiwa majukumu hayo ya Umma?
 
Sasa inakuwa na maana gani kuapishwa huku umeshika Katiba na kuahidi kuitii na kuiheshimu Katiba hiyo kabla ya kukabidhiwa majukumu hayo ya Umma?
Huwa wameshika katiba au Biblia ama Kurani?
 
Leo hii anaitwa Nusrat Hanje, sio COVID 19 tena? CHADEMA acheni kuendelea kuweweseka. Mmewachafua wamama wa watu, kwanini bado mnawaota hao wabunge wa Bunge la JMT wasio na chama?
 
Mleta mada unachoongea unadhani mtu akiwa rumande ni mawakili tu ndio huhangaika kumtoa .Wako ndugu pia na jamaa na marafiki huhangaika kivyao bila kushirikisha mawakili pia.

Mawakili wenu walikuwa wakichelewesha ili wale pesa za CHADEMA wakijitia ohh! tuko tunafanya juhudi kumbe uongo mtupu na utapeli wanachaji chama tu pesa za masaa wanayotumia kula pesa za chama

Hanje na wenzie wametolewa na ndugu na marafiki baada ya kuona mchezo mchafu uliokuwa ukichezwa na mawakili vibaka wa CHADEMA wakishirikiana na Mbowe na Mnyika na wakitumia wao kuwekwa ndani kama kick ya kisiasa na njia ya kuiba na kula hela za chama

Taratibu zote zilifuatwa kupitia ndugu zao na jamaa na marafiki zao bila kuhusisha mawakili vibaka

Naona uko na hasira sababu ya kunyang'anywa kitumbua chenu na mawakili wenu wezi mdomoni.
 
Leo hiii anaitwa nusrat hanje, sio covid 19 tena? Chadema acheni kuendelea kuwewesekaaa. Mumewachafua vya kutosha wamama wawatu, kwanini bado munawaota hao wabunge jmt wasio na chama?

Covid 19 ndio wamesababisha Biswalo atende kosa la kikatiba na ndie msingi wa mleta hoja.

Binafsi na kwa kifupi kaabisa kilichotendeka kwa Nusrat ni picha ndogo sana ndani ya kitabu chetu cha sheria zetu " Tip of the Iceberg"
 
Covid 19 ndio wamesababisha Biswalo atende kosa la kikatiba na ndie msingi wa mleta hoja,

Binafsi na kwa kifupi kaabisa kilichotendeka kwa Nusrat ni picha ndogo sana ndani ya kitabu chetu cha sheria zetu " Tip of the Iceberg"
Toka lini na nyie CHADEMA mmwite Nusrat Hanje? Simmewabatiza wao ni Covid 19? Kwani Biswalo ndo amewatimua kwa mbwembwe na fedhuri kwenye kikundi chenu??Mbona CHADEMA mnazidi kuchanganyikiwa juuu ya hawa wamama wa watuu? Waacheni wapumuzike sio kushinda mnawasengenya mitandaoni tena Mliwatimua haraka sana, sasa mnawataka nini tena?
 
Toka lini na nyie chadema mumwite nusrat hanje?? Simumewabatiza wao ni covid 19? Kwani biswalo ndo amewatimua kwa mbwembwe na fedhuri kwenye kikundi chenuu?? Mbonachadema mnazidi kuchanganyikiwa juuu ya hawa wamama wa watuu?? Waaacheni wapumuzike siokushinda munawasengenya mitandaoni tenaa. Mliwatimua haraka saanaa, sasa mnawataka nini tena?

Unaongea na Covid19?
 
Mbona humshinikizi mnyika aliyesaini makaratasi!
Tumshinikize ajiuzulu?

Wakati ukweli wote ameuelezea peupe mchana.

Kuwa form zote alikuwa nazo zikiwa bado "intact" hazijajazwa chochote!

Utuambie hizo form alizopokea Dkt Mahera alizipata wapi, kama siyo mchezo wa kufoji, uliofanywa na viongozi wenu wa Chama na serikali?
 
Mzee Msekwa pamoja na kwenda chaka Mara nyingi ila kwenye hili kasema lazima Katiba na sheria ziheshimiwe. Nashangaa sana kama hadi aliyetunga Katiba kasema hivi Kwa nini huyu jamaa hajachukuliwa hatua.
 
Watakujibu kuwa kama wewe uliiweka Post yako 1:48AM haukuwa umelala basi ujue pia serikali haina usiku muda wote ni mchana, miaka kadhaa iliyopita enzi za awamu ya pili kama sijakosea kuna hukumu iliwahi kutolewa usiku!

Subiri tuwasikie.
 
Mzee msekwa pamoja na kwenda chaka Mara nyingi ila kwenye hili kasema lazima Katiba na sheria ziheshimiwe. Nashangaa sana kama hadi aliyetunga katiba kasema hivi Kwa nini huyu jamaa hajachukuliwa hatua
Yaani huyu Jiwe anaona kama aliyetutawala ni maiti!

Hivi inawezekanaje mtu aliyefanya "blunder" ya dhahiri kama hii, aendelee kumkumbatia?
 
Back
Top Bottom