DPP Biswalo Maganga kuwa Jaji, Rais Samia umekosea sana

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,106
35,038
Miongoni mwa watu walioteuliwa leo na Rais Samia Suluhu kuwa majaji wa mahakama kuu, jina la DPP Biswalo Maganga lipo pia.

Hili jambo limetushtua sana wadau wa mambo ya sheria, kuna kitu tunakiona hakiko sawa na kinakwenda kutuharibia zaidi mhimili wetu wa sheria. Nitaweka sababu za msingi sana kwanini Biswalo Maganga hastahili kuwa jaji.

1. Kabla ya mtu kupendekezwa kuwa jaji, ni lazima vetting ifanyike kisheria. Hili ni jambo la kisheria na linapaswa kufanyika kwa haki, uwazi na weledi. Biswalo Maganga hakufanyiwa vetting na tume utumishi wa mahakama popote pale.

2. Kabla ya mtu kuteuliwa kuwa jaji ni lazima jina lake lipendekezwe na tume ya mahakama. DPP Biswalo Maganga hakupendekezwa popote.

3. Nafasi iliyokuwa nayo kama DPP haiwezi kumruhusu kufanyiwa vetting au kupendekezwa kuwa jaji na vyombo vya mahakama. Ni sawa na kufanya 'vetting na kupendekeza' Rais Samia awe spika wa bunge wakati huo akiwa bado Rais!

4. Haiwezekani kwa mtu kutoka kwenye nafasi ya DPP na moja kwa moja kuteuliwa kuwa Jaji, kimahakama inatia ukakasi mkubwa. Yaani jana DPP alikuwa ana file kesi za jinai dhidi ya watu fulani halafu leo anakuwa jaji wa mahakama hiyo hiyo kusikiliza kesi na kuhukumu kesi hizo hizo!.

5. Tabia, sifa, mwenendo na vitendo vingi alivyovifanya Biswalo Maganga akiwa kama DPP dhidi ya utendaji wa mahakama havistahili hata chembe kuweza kufikiriwa kuwa hata hakimu wa mahakama yoyote ya kutoa haki hapa duniani. (Mganga aliweza kuamuru mtu yoyote afikishwe mahakamani hata kama hakuna mashtaka dhidi yake ama aachiwe huru hata kama hati ya mashtaka hairuhusu hilo kufanyika). Rais angeweza kumtunuku Biswalo Mganga chochote kile kwenye mhimili wake wa serikali (ikiwa alikuwa anamhitaji) lakini sio kumsukumizia kwenye mhimili wa mahakama. Huko ni kuwatukana wanasheria wa mahakama kuu.

Kwa wale wasio na uelewa wa mambo ya kisheria na mfumo wa uteuzi wa majaji hapa Tanzania, kikatiba uteuzi wa majaji ni jambo linapaswa kuzingatia weredi, mchakato mpana na muda mrefu. Sio jambo ghafla, fadhila au mapendekezo binafsi ya Rais aliyepo madarakani.
 
 
Teuzi zake za wasiwasi zimekuwa kielelezo cha utawala wake, kuanzia yule mkurugenzi wa TPDC aliemteua na baadae kutengua uteuzi wake within 24 hrs mpaka leo bado anayumba tu.

Sijui washauri wake huwa wanamshauri vitu gani, she is too soft hearted, hataki kutumbua yeye anakutoa hapa anakuweka pale hata kama hufai kulingana na historia yako, na ni Rais mwenyewe aliesema anamteua mtu kutokana na historia yake, sijui kwa Mganga katumia historia ipi.
 
Mambo mengine nadhani mnamuonea tu.

Hili ni moja ya janga alilolitengeneza Magu. Na hatukusaidia chochote.

Watu wake wengi aliwatungia sheria za kuwalinda ili wavuruge atakavyo. Spika, Waziri Mkuu, DPP

Hata Rais Samia yawezekana hamtaki ila kaona hiyo ndio njia yenye afadhali.

Soma hizo sheria akizotunga Jiwe 👇👇👇

IMG_20210511_204735.jpg


IMG_20210511_204739.jpg
 
Kwa taarifa tu

Jaji Kiongozi wa sasa Dr Feleshi aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2014 akitokea NAFASI ya DPP

KATIBA INAMPA MAMLAKA RAIS YA KUTENDA ALIYOTENDA BAADA YA KUSHAURIANA NA JOPO HUSIKA
Katiba yetu raha sana, ni kama tunatawaliwa kifalme vile kama Kwazulu land au E-swati kwa Mswati. Na kwa bahati mbaya/ nzuri suala la katiba halikuwepo kwenye Ilani ya Chama cha Mama, Wacha majoka yarukwe tu.
 
Nakumbuka wakati wa Magufuli aliwahi kusema Biswalo alipendekezwa kua jaji ila yeye akakataa kwani ni mtu ambae anawapeleka mafisadi jela.

Kama sasa hajapendekezwa labda mama ametumia mapendekezo ya awali. Hilo la kwanza.

La pili, kwani mapendekezo hua yanatumwa kwa nani ili tujue kama hakupendekezwa ama alipendekezwa?
 
Wale watu meko aliwaweka pale kwa sababu alikuwa na matumizi nao ambayo wote tunaelewa, sasa mama mbona anachokiongea sio anachotenda. Ni bora meko afufuke tu.
 
Kuna baadhi ya mambo tunatakiwa kuyafikiria kwa upana,sio haraka haraka za kukurupuka,kuteuliwa kuwa jaji kutoka dpp ni kama kuwa demoted in a right sense,kuwa jaji ni wa mahakama moja tu, na kama mtu ni muonevu ataonea watu kidogo tu, tafauti na kuwa dpp,dpp ni wa nchi nzima Akiwa muonevu system nzima ya kiserikali itakuwa ya kiuonevu, kumuondoa dpp lazima umpe keki isiyokatalika,sababu analindwa na sheria lazima ajiuzulu mwenyewe.
 
Miongoni mwa watu walioteuliwa leo na Rais Samia Suluhu kuwa majaji wa mahakama kuu, jina la DPP Biswalo Maganga lipo pia.

Hili jambo limetushtua sana wadau wa mambo ya sheria, kuna kitu tunakiona hakiko sawa na kinakwenda kutuharibia zaidi mhimili wetu wa sheria. Nitaweka sababu za msingi sana kwanini Biswalo Maganga hastahili kuwa jaji....
Mkuu unahakika uteuzi huo hajapitia huo mchakato? Umejuaje hilo? Ili hali nakumbuka Maneno ya JPM alishawahi seme alishawahi kupendekezwa kuwa jaji na Tume.
 
Back
Top Bottom