Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 5,277
- 7,961
Watanzania mna bahati mbaya kwa kuwa hamjui mnacho taka. Nakubaliana na yote uliyoandika kasoro pale unapomkosoa Rais Samia SSH kumteua kuwa Jaji.Miongoni mwa watu walioteuliwa leo na Rais Samia Suluhu kuwa majaji wa mahakama kuu, jina la DPP Biswalo Maganga lipo pia.
Hili jambo limetushtua sana wadau wa mambo ya sheria, kuna kitu tunakiona hakiko sawa na kinakwenda kutuharibia zaidi mhimili wetu wa sheria. Nitaweka sababu za msingi sana kwanini Biswalo Maganga hastahili kuwa jaji...
Pima kati ya mawili lipi ni jema. Biswalo kubakia DPP ambaye maamuzi yake ya kimashtaka yeye hawi challenged na mamlaka nyingine yeyote, au kuwa Jaji wa Mahakama Kuu anaweza kuwa challenged na Mahakama ya Rufaa?
Kumtoa DPP ni suala la kikatiba/ kisheria kama ilivyo kumtoa CAG. Rais ana mamlaka ya kuwateua, lakini kuwatoa ofsini ni mchakato mrefu.
Je mnataka Rais avunjje Katiba Kama Mwendazake alivyofanya kwa kutoa Prof Assad aliyekuwa CAG?
Tumepata Rais msikivu na anayependa kufuata Katiba, asiyependa kuonea watu bado haturidhiki?
Hebu tujifunze kwa yaliyotupata baada ya kumponda JK, tukapata dude la kutisha