DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi

Unapotendewa jambo jema, ustaarabu ni kushukuru kwa yote hata kama ulionewa. Natoa wito kwa Tundu Lissu, amshukuru sana Mama Samia

Ila pia sitashangaa iwapo shukrani haitatolewa kwasababu baadhi ya wenzetu hawana shukrani.
P
Pascal acha unafiki !!. Ashukuru kwa lipi ?! . Naona mnataka wapinzani wawe na mioyo ya malaika. Umbambikie mtu kesi na kumsotesha mahakamani miaka yote hiyo. Halafu anajitokeza DPP eti hana nia ya kuendelea na kesi ??!!!

Ujinga mwingine Pascal Mayalla
 
Unapotendewa jambo jema, ustaarabu ni kushukuru kwa yote hata kama ulionewa. Natoa wito kwa Tundu Lissu, amshukuru sana Mama Samia

Ila pia sitashangaa iwapo shukrani haitatolewa kwasababu baadhi ya wenzetu hawana shukrani.
P
Hawezi kumshukuru kwasababu alipoingia madarakani alimwambia afute kesi ndio yeye(Tundu) arudi so mama anatelekeleza bado la kumuwekea ulinzi
 
DPP kufuta fits kesi nyingi za serikali ya awamu ya tano,ni ushahidi tosha kuwa mashitaka mengi yalikuwa na walakini.Serikali ijitafakari
 
Wale waliotaka kumuuwa natamani wakamatwe na wanyongelewe mbali kabisa.

Uzuri wa uyu mama hapendi uonevu wala zulma,, atawaonyeshea tu hao wauwaji.
 
Unapotendewa jambo jema, ustaarabu ni kushukuru kwa yote hata kama ulionewa. Natoa wito kwa Tundu Lissu, amshukuru sana Mama Samia

Ila pia sitashangaa iwapo shukrani haitatolewa kwasababu baadhi ya wenzetu hawana shukrani.
P
Ustaarabu wa Lumumba na wa kijima.
 
Criminal Case No.208/2016 iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu na wenzake watatu katika Mahakama ya Kisutu, imefutwa na DPP kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo ya Makosa ya Jinai. Watuhumiwa wote wako huru.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh

Washtakiwa hao kwa pamoja Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002.

Patrick Mwita wakili wa serikali mbele Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisoma shitaka la kwanza na tano.

Mwita alidai kuwa shitaka la kwanza ni la kupanga njama za kutoa chapisho la uchochezi, kosa linalodaiwa kutendwa kati ya tarehe 12 na 14 Januari mwaka 2016 ambapo;

Idrissa, Mkina na Lissu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam walipanga njama za kuchapisha taarifa za uchochezi.

Katika kosa la tano, mshitakiwa namba moja (Idrissa), namba mbili (Mkina) na namba nne (Lissu), wanatuhumiwa kuchochea hofu miongoni mwa wananchi kwa kuchapisha habari “Machafuko yaja Zanzibar” na kwamba, ingeweza kuzua vita au umwagaji damu.

Shitaka pili likimkabili Jabir, Mkina na Lissu, wakidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika Gazeti la MAWIO, toleo Na. 182 la tarehe 14-20 Januari 2016.

Shitaka la tatu linamuhusu Ismail akidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari ‘Machafuko yaja Z’bar’.

Shitaka la nne linamkabili Ismail akidaiwa kuchapisha gazeti bila kupeleka kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
DPP MFUTA KESI! Tulishamsikia YOHANA MBATIZAJI, sasa tumempata mfano wake - Lakini huyu anaitwa DPP MFUTA KESI. Maisha mema katika kiti chako cha muda.
 
Mjinga kabisa katika jukwaa hili huwa ni wewe dada !!. Umekuwa ukivishabikia vitu hivi vya kipumbavu vya kupotezeana muda.

Kelele zote za kumfuata Lissu Dodoma usiku kama jambazi. Zimeishia kwa DPP kusema hana nia ya kuendelea na kesi ?!

Ujinga
Unaniita dada dada wakati nalala na mamako

USSR
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom