DPP Awafutia mashitaka vigogo wote wa TPDC

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,263
24,140
Vigogo wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) wameangua vilio vya furaha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuachiwa huru.

Hatua ya kuachiwa huru kwa vigogo hao akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, James Mataragio ni baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka dhidi yao.

Bw. James Mataragio ambaye hakuwepo mahakamani, alirejeshwa katika nafasi yake ya kazi hivi karibuni baada ya agizo la Rais John Magufuli.

Washtakiwa wengine walioachiwa huru ni katika ni George Seni, aliyekuwa Kaimu Meneja wa Uvumbuzi; Welington Hudson, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Utawala; Kelvin Komba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu na Edwin Riwa , aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mipango. Kwa pamoja washitakiwa hao wameachiwa huru mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina.

Ni baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kuomba kuiondoa kesi hiyo tangu Julai 10, 2019. DPP kwa niaba ya Jamuhuri amesema hakusudii kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao katika kesi hiyo na akaomba iondolewe chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina aliwaachia huru washitakiwa hao chini ya sheria hiyo.


Source : millard ayo
 
Nchi yangu Tanzania! No matter what you are my mother land, you are my land.
 
Back
Top Bottom