DPP awafutia kesi Maimu, wenzake wawili mashtaka 10 ya utakatishaji fedha

Taaratibu pengine DPP anakaribia faili la Mwenyekiti na wenzie 3 ktk kesi namba 16 / 2021, hivyo anatuma ujumbe wa moshi mweupe utaonekana...
Hivi umeelewa kilichoandikwa hapo? Hao wote bado wataendelea kusota jela, hizo ni delay tekiniki za DPP anapokuwa hana ushahidi na ana maelekezo hampaswi kuachiwa huru lazima mkomeshwe kwa kukaa jela tu.
 
Wanawafutia mashtaka wengine huku wakiwapachika wengine mashtaka ya uongo, huu ni muendelezo wa upuuzi wa awamu iloyopita.
Hakuna aliyefutiwa mashtaka hapo, wengi hamuelewi michezo ya ofisi ya DPP.

Hao wanasomewa kesi upya na mashtaka mapya wanaanza square one.

Niambie ni yupi ameachiwa huru katika hao wote? Wote wapo jela na hakuna dhamana.

Mwanangu mwakani anaingia University kwakweli sitaki achaguwe fani hii, ni pacha wa shetani.

Kina Kibatala ni wachache sana kwenye fani hii, wengi ni waumiza binadamu wenzao, kuanzia mahakimu, majaji hata hawa mawakili binafsi.

Msione leo Mbowe anatetewa kwa nguvu kubwa na uzalendo lakini baadhi yao hawa mawakili binafsi nao ni mashetani vilevile.

Sintomsahau wakili mmoja wa kujitegemea aliyemgeuza mzazi wangu dili na akaandaa mazingira yote mimi na mzazi wangu tusimame mahakani kwa jambo ambalo mtu yeyote anayetumia akili yake vizuri na ana hofu na Mungu angelimaliza kwa kutuweka chini na kuondowa sintofahamu zilizojitokeza.

Kama unajihisi una dhambi na hutoiona pepo wala usiogope, wewe utakwenda mbinguni ila watu wa fani ya sheria 90% moto wa kuzimu unawasubili kama yule mungu wao wa Chatu.
 
Karibuni na mbowe atafutwa kesi ya ugaidi atakapoapishwa rais mpya mwenye busara
 
Vitambulisho vya Taifa toka awamu ya pili ni story tu za kusadikika, watu wako ofisini raia hawana vitambulisho....mishahara, posho za vikao na mambo kibao yanaicost nchii..

Mara paap picha linaanza kaja msela mmoja miaka 6 tu, zaidi ya nusu ya watanzania wana vitambulisho na its applicable everywhere na taasisi ikaonekana active yule jamaa pamoja na mambo yake ila kuna mahala angesaidia sana hii nchi na wapumbavu wengi wangefutika kwenye mifumo na hata Taifa lingeanza kuzalisha kizazi active sio vijana hawa rojorojo aka mchele mchele...
 
Kesi za wapigaji ndio zinafutwa. Miaka mingapi vitambulisho bado watu kupewa wote kwa upigaji wa funds za vitambulisho. Halafu wapigaji wamerudishwa ulingoni wanafutiana kesi. Eti kesi za kijinga? Wakati ndio kesi za maana.
Mambo ya visasi peleka kaburini mkajadili na mwenzio. Miaka zaidi ya 5 kama ushahidi hajapatikana kwanini tusiamini mhusika aliwekwa ndani kwa kuonewa kwa sababu ya visasi binafsi vya shetani mchawi? Kama hao wangekuwa na hatia, shetani mwenye roho mbaya kwanini hakuacha wameshahukumiwa ktk miaka yake zaidi ya 5 aliyokaa ktk kiti akitesa watu kwa visasi vyake? Mbona kina Sabaya ambao walipelekwa mahakani bila kuonewa wamehukumiwa kwakuwa ushahidi ulikuwepo na haukuwa na shaka ndio maana hata yeye mwenyewe akashindwa kuukana ushahidi dhidi yake?

Kama hao waliokamatwa na shetani wangekuwa sio visasi vyake binafsi vya shetani, kwanini miaka inaenda tu na ushahidi haupatikani huku watu wanateseka tu! Kama ushahidi hakuna, futeni kesi hizo watu warejee kufarahia na familia zao.
 
Ndio ubovu wa kutokuwa n taasisi imara na zenye meno. DPP yeye alipewa maagizo kutoka kwa ibilisi mwovu joka kuu weka ndani hao kwa visasi vyake. DPP naye hana hata muda wa kujiridhisha kama kweli kuna jinai sma la anatekeleza maagizo. Sasa tukisema hawa walikuwa wafungwa wa kisiasa mtatukatalia?
Kweli kabisa yule alikuwa MWOVU IBILISI kabisa. Hivi JK alikuwa hamjui hadi akakubali kutuchomekea yule jamaa? Hivi kama Mungu asingeamua kumfutilia mbali hadi sasa tungekuwa taifa la aina gani?
Kama alikuwa na vijana kama Sabaya jee yeye yake ya uficho yako kiasi gani?
Kuna habari za chini kwa chini hata yeye kwa mkono wake mwenyewe aliwalaza watu.
 
Ndio ubovu wa kutokuwa n taasisi imara na zenye meno. DPP yeye alipewa maagizo kutoka kwa ibilisi mwovu joka kuu weka ndani hao kwa visasi vyake. DPP naye hana hata muda wa kujiridhisha kama kweli kuna jinai sma la anatekeleza maagizo. Sasa tukisema hawa walikuwa wafungwa wa kisiasa mtatukatalia?
Kww hiyo mbowe ameshitakiwa na taasisi imara chini ya awamu ya 6
 
Kweli kabisa yule alikuwa MWOVU IBILISI kabisa. Hivi JK alikuwa hamjui hadi akakubali kutuchomekea yule jamaa? Hivi kama Mungu asingeamua kumfutilia mbali hadi sasa tungekuwa taifa la aina gani?
Kama alikuwa na vijana kama Sabaya jee yeye yake ya uficho yako kiasi gani?
Kuna habari za chini kwa chini hata yeye kwa mkono wake mwenyewe aliwalaza watu.
Kwa hili CCM kama hawakujifunza sijui itakuwaje mbeleni wakituletea mtu wa sampuli Ile ya ibilisi mwovu joka kuu. Uzuri nao walionja joto la jiwe.
 


MKURUGENZI wa Mashitaka nchini (DPP) amewafutia mashitaka 10 ya utakatishaji fedha washtakiwa watatu kati ya watano akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu.

Mbali na Maimu washitakiwa wengine waliofutiwa mashitaka hayo ni aliyekuwa Ofisa Usafirishaji Nida, George Ntalima na Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka 55 likiwamo utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya amedai jana Oktoba 22 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa shauri hilo limekuja kwaajili ya kutajwa lakini wanakusudia kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka.

Amedai kesi hiyo iko katika hatua za usikilizwaji lakini Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) amekusudia kufanya marekebisho madogo chini ya kifungu cha 234(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA).

“Jumla ya mashtaka yaliyokuwa yanawakabili ni 55, baada ya marekebisho haya yatakuwa mashtaka 45, kwa mshtakiwa wa kwanza Dickson Maimu, mshtakiwa wa tatu, George Ntalima na wa nne Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo ambao wameondolewa mashtaka ya utakatishaji fedha,” amedai Wakili Komanya.

Wakili Komanya amedai endapo hakutakuwa na pingamizi, wangeomba kuwasilisha hati mpya, hata hivyo hati hiyo haikupokelewa kutokana na Hakimu Mkazi Mkuu Rashid Chaungu anayesikiliza kesi kutokuwepo.

“Hata mkiwasilisha hati mpya, kesi hii haiko haiko mbele yangu, nawashauri muiwasilishe mbele ya Hakimu husika tarehe itakayopangwa, na kuhusu dhamana nawashauri kuwasilisha maombi Mahakama Kuu,” alieleza Hakimu Shaidi.

Baada ya maelezo hayo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4 mwaka itakapotajwa ambapo upande wa mashtaka utawasilisha hati mpya.

Katika kesi hiyo, tayari upande wa mashitaka umeshafunga ushahidi kwa kuwaita jumla ya mashahidi 26 pamoja na kuwasilisha vielelezo 45. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Meneja Biashara wa (Nida), Aveln Momburi na Mkurugenzi wa Sheria, Sajina Raymond.
 
Tuna Mahakama za ajabu sana, sionagi umuhimu wa Mahakama kwa Tanzania maana haki ya MTU inaamuliwa na MTU mmoja! Yaani mtawala akisema ukamatwe upewe kesi basi inakua hivyo na unakutwa na "hatia" au ndio kama huu upuuzi wa kumsumbua MTU kwa miaka sita kisha unakuja kusema unamfutia mashtaka
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom