DPP amvaa Dk Hoseah, ataka mdahalo majalada kesi za kifisadi

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
1,195
KWANZA ilikuwa ni ndani ya chama tawala CCM, lakini malumbano baina ya vigogo sasa yamehamia serikalini baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi kujibu mashambulizi ya mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, akitaka uitishwe mdahalo baina ya wawili hao ili ajibu tuhuma dhidi yake.

Pendekezo hilo la Feleshi limekuja wakati malumbano baina ya viongozi wa CCM hayajapoa baada ya kutuhumiana kwa ufisadi na wivu wa nafasi mbalimbali zilizotokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Dk Hoseah, ambaye amekuwa akirusha makombora kwa taasisi tofauti, juzi alitoa tuhuma nzito alipokaririwa na gazeti moja akisema kuwa ameshawasilisha kesi zaidi ya 60 za tuhuma za rushwa kwa DPP na akashangaa sababu za mteule huyo mwenzake wa rais kukalia mafaili hayo badala ya kufungua kesi dhidi ya watuhumiwa.

Lakini jana Feleshi alikuwa mbogo na akasema kuwa ili ukweli uwekwe bayana kuna haja ya kuandaa mdahalo baina yake na Hoseah.

DPP Feleshi, akizungumza na gazeti dada la Mwananchi la The Citizen baada ya hafla ya mafunzo ya kamati ya kitaalamu ya mawakili wa serikali iliyofanyika Kunduchi jijini Dar es Salaam, alisema njia pekee ya kuweka sawa rekodi ni kuwepo kwa mdahalo huo wa wazi.

"Ninataka mdahalo na Hoseah katika masuala haya yanayoendelea hata kama utakuwa wa simu tena iwekwe ‘loud speaker (kipaza sauti)’ ili tujadili masuala haya na kumaliza kiu ya wananchi," aliweka msimamo DD Feleshi.

"Kama mtu anasema kuna majalada 60 ofisini kwangu, then (kisha) tunamuuliza yamefika lini? Yeye pia atajibu, kwa kufanya hivyo tutatoa mwanga mzuri kwa wananchi ambao ofisi hizi zipo kwa ajili yao tu."

DPP Feleshi alisema anataka mdahalo huo ufanyike mbele ya waandishi wa habari ili jamii ijue masuala mbalimbali yanayoelekezwa ofisini kwake.

Hoseah pia aliwahi kuirushia kombora mahakama akisema inaendesha taratibu kesi za ufisadi, hivyo kupunguza kasi ya taasisi hiyo kushughulikia watuhumiwa wa rushwa.

Miongoni mwa kesi ambazo zilifunguliwa kwa wingi hivi karibuni na Takukuru ni pamoja na kesi zaidi ya 20 zinazohusu wizi kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), matumizi mabaya ya madaraka na uzembe na tuhuma za kula njama na kuisababishia hasara serikali.

Hata hivyo, mwenendo wa kesi nyingi umekuwa wa kasi ndogo kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha ushahidi.

Akizungumzia madai hayo ya Hoseah, Feleshi aliweka bayana kwamba hayajui majalada hayo na anachojua ni kwamba ofisini kwake kuna majalada ya kesi ambayo yanaingia na kutoka kila siku na anayashughulikia kwa mujibu wa sheria.

Feleshi, ambaye aliwahi kurejesha Takukuru baadhi ya majalada kutokana na kuonekana udhaifu katika ushahidi, alimtaka Dk Hoseah kutoa ufafanuzi kwa kueleza ni majalada gani yanayokaliwa na ofisi yake na yamefika lini.

Alifafanua kwamba ofisi yake haiwezi kukalia majalada kwa kuwa inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kwa maslahi ya umma na kusisitiza hayajui majalada hayo 60 anayodai Dk Hoseah kwamba yamekaliwa ofisini hapo.

"Hayo mafaili (majalada) ya vigogo mimi siyajui. Ninachojua ni kwamba tuna majalada yanaingia kila siku ya Watanzania wanaotuhumiwa. Tunapokea na kuyafanyia kazi... na hatubagui kuwa haya ni ya PCCB (Takukuru) , TRA( Mamlaka ya Mapato) au ya Polisi. Katiba ya nchi inatoa haki sawa kwa wote kufikishwa mbele ya sheria ili kupata haki," aliongeza DPP.

"Tunafanya kazi kwa maslahi ya umma na tunaendesha shughuli zetu kisheria wala si kwa kuzingatia jambo lolote kwa kuwa hatuna maslahi yoyote kumshtaki mtu bila kuwa na ushahidi wala hatuna maslahi yoyote kumwachia mtu kama kuna ushahidi. Ndiyo maana nasema hakuna kukalia majalada."

Feleshi, ambaye ana mamlaka ya kufunga au kufungua mashtaka kwa watuhumiwa, alisema katika hali hiyo ni vigumu kusema kuna majalada yana muda mrefu kwani hajui hayo yanayosemwa yaliingia lini ofisini kwake.
"Labda kama angekuwepo mwenyewe (Dk. Hoseah) angeeleza zaidi hayo majalada anayodai tumeyakalia. Ni vema mkamuuliza hilo," alisema.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,274
2,000
I'm getting a very evil idea.. an idea that is terrible in its essence and purely evil.. wacha nilale nisije kuchuma dhambi bure.
 

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
1,195
Lala usingizi Babu yangu teh vuta kidogo ugoro wako ili kesho uje na hiyo idea na pia itakuwa vizuri ukisema maana siku zote unakuwa makini katika masuala haya mzee wangu na babu yangu Mwanakijiji
 

Yetu Macho

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
224
195
Hii tabia ya kurushiana lawama/ mambo ndo danadana tulizozizowea hapa Tanzania. Hosea anajaribu kutumia kila juhudi kusafisha jina lake kwa jamii ambalo lisachafuka mbayaa baada ya Richmond. Analifanya hili kujaribu kuonyesha taasisi nyingine ndizo zinazorudisha nyuma jitihada za taasisi yake. Huu ni uzandiki na unafiki mkubwa.

Felesi nae asituzuge kwamba kesi za vigogo vitatreatiwa sawa na zakajambanani toka tandale kwa mfuga mbwa na asiejulikana vyovyote. Inasikitisha kama ofisi yake haina vipaombele na haijui uharaka wa mambo. Sikweli na naamini ametudanganya kama kuna file 60 za ufisadi mkubwa ofisini kwake na asijue ati kwakua ofisi yake inashuhulikia kesi zote sawa. Huu ni upotosaji mkubwa na unarudisha nyuma maoambano haya dhidi ya ufisadi.

Watumishi wa serikali na watanzania kwa ujumla. Tujifunze kuwajibika kila mtu kwa eneo lake ni katika uwajibukaji na kilamtu kutambua wajibu wake kwa taifa hili ndipo tunaweza kuleta mabadiliki.

Kurushiana mipira hakusaidii. Tunataka kuona mambo yakisonga mbele
 

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,379
2,000
DPP Kutaka mdahalo na hosea ni sawa na baba aliyewalaza watoto wake kwa njaa sababu ya kilauri(poombe) then anataka mdahalo na mama watoto mbele ya watoto. HUO MDAHALO UTAYAONDOA MADHARA WALIYOSABABISHIWA WATOTO NA NJAA? Achenini mzaha wajameni!!
 

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,408
2,000
Hivi ni mhimili gani wa Taifa letu uliobakia usiokuwa wa kimipasho au kuhitaji kwenda kupimwa akili Mirembe au kule Karibia?!!
 

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,221
1,225
Hamna kitu hapa.

Amandla..........


Na ni kweli! mpwa maana humo PCCB na DPP kumetawaliwa na siasa sana and both PCCB&DPP they dont take action or deliver issues by professional just fuatilia mambo yao utayaona tu haya kichwa wal miguu, wao kama hawajui hizo kazi basi wapishe watu wazijuao na kama wao wanzijua hizo kazi basi wanazifanya kwa minaajili ya kundi fulani ktk jamii yetu na kuwaridhisha wao na kuwaacha jamii ya kina sisi walala hoi njia panda na kuwasiliza marumbano yao.

its really pathetic

 

Nurujamii

JF-Expert Member
Jun 14, 2007
414
195
Tatizo la Feleshi amejipachika madaraka ya uhakimu na kutoa hukumu kabla kesi hazijaingia mahakamani. Feleshi ni kikwazo. Na kwa jinsi alivyojipachika madaraka sioni sababu yoyote ya kuwa na mahakama kwani ofisi ya DPP ndio yenye kuhukumu.

Hata hivyo ukweli unajulikana. Anatafuta kila sababu ili kuzuia kesi za vigogo kuingia mahakamani. Hilo linajulikana na halina ubishi. Feleshi ni mzigo kwenye vita ya ufisadi.

Hivi hata bila kuwa mtaalamu wa sheria hivi kweli kuna sababu yoyote ya kesi ya Chenge kuendelea kuzuiwa kuingia mahakamani kwa zaidi ya mwaka sasa? Mbona it is too obvious?

Au na Kagoda Je? Hata kama Rostam is not implicated at this point kwa kutumia ufisadi na hela zake, lakini si kuna wale watu waliondikishwa kuwa ndio wamiliki wa Kagoda na ndio wanaoonekana kwenye makabrasha kuwa ndio waliochota hizo hela? Mahakama si ndio itawahoji na kujua ukweli wa wapi walipopata mtaji? Kwa nini DPP asiwapeleke hata hao maboya mahakamani basi ili mahakama ifanye kazi yake ya kujua ukweli na kutoa hukumu kwa wahusika?

Kwa jinsi mambo yalivyo ni kwamba Feleshi tayari anajua Rostam ndio mmiliki wa Kagoda na kinachokosekana ni ushahidi wa kumuunganisha nayo! Hiyo si kazi yake DPP. Yeye anachopaswa kufanya ni kuamuru wamiliki waliondikishwa wakamatwe na kupelekwa mahakamani. Ni kazi ya mahakama ku-implicate kina Rostam sio DPP!

Huu ni uchuro wa kisheria Tanzania. Badala ya kuangalia uhalifu ulivyotokea na wahusika waliojiorodhesha kuhisika na hiyo kampuni kukamatwa ili wakahojiwe na kutoa ushahidi mahakamani; anaangaliwa mtu kwanza halafu ndio kesi iamuliwe kupelekwa au kutopelekwa mahakamani! Upuuzi mtupu! Arrrggg!
 

Kafara

JF-Expert Member
Feb 17, 2007
1,392
1,500
baada ya hapo makatibu wakuu nao watadai mdahalo.

amakweli dereva usukani unamletea matatizo
 

Wasegesege

Senior Member
Oct 22, 2009
107
0
Hata Tanzania kuna Watu ambao kwa nafasi zao (Nyadhifa ) ni Viongozi wa Umma na pia ni Watumishi wa Umma. Bw. TAKUKURU na Bw. DPP ni miongoni mwao wao ni Viongozi wa Umma na pia ni Watumishi wa Umma.

Kwa mujibu wa Sheria ya ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2007, Ukisoma pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumihi wa Umma toleo la pili la mwaka 1994, pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma za mwaka 2004 zinamtaja Mtumishi wa Umma ni nani. Aidha, ukisoma Sheria nA. 13 ya maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 inawataja aina ya Viongozi wa Umma. Kwa hiyo katika Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2004 kama zilivyotolewa na Waziri mwenya dhamana ya Utumishi wa Umma zinasema " MTUMISHI YOYOTE WA UMMA ANATAKIWA KUTOKUTENDA AU KUACHA KUTENDA JAMBO AMBALO LITAUDHALILISHA UTUMISHI WA UMMA. Pia, katika Sheria Na. 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 kuna Kifungu kinasema "KIONGOZI WA UMMA HATATAKIWA KUTENDA AU KUACHA KUTENDA JAMBO LOLOTE LITAKALOUDHALILISHA UONGOZI WA UMMA.

Sasa Kila uwazi una mipaka yake. Wewe huwezi kusema kila kitu unachofanya kwa Mke usiku kwa Baba yako hata kama yeye ndo aliyetoa mahali uliyoolea, au aliyekujengea na nyumba na alikusomesha na akakutunza. Hapana kuna sehemu ya kusemea matatizo yako na Mke kama yapo. Hawa DPP na YAKUKURU wametenda TENA KWA MAKUSUDI jambo ambalo limeudhalilisha siyo tu Utumishi wa Umma bali hata Uongozi wa Umma. leo magazeti hayasema Fereshi kasema vile au Hosea Kasema vile yanasema "HEBU ONENI DPP NA MKUU WA TAKUKURU wanavyorushiana maneno kwenye Magazeti.

Ile nidhamu ya Utumishi wa Umma iko wapi. Hawa huwa wanavikao vya Kiutendaji ammbavyo huwa wanakutana. Sasa iweje leo wasimame hadharani na kuanza kuivua nguo Serikali. Maana Serikali imevaa nguo wao wanaivua nguo ili iweje.

Unajua kuna Msemo wa kiswahili unasema "UKITAKA KUJUA TABIA YA MWANAO MTAZAME RAFIKI YAKE" utajua tu kama mwanao ni wa tabia gani, maana wewe mzazi wake atakuficha. Hivi ndivyo imejidhihirisha kwa DPP na TAKUKURU kwamba kama wao WAKUU WA TAASISI hizi hawajuwi MIPAKA YA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA NA UONGOZI WA UMMA je hao wanaowaongoza wakoje?

Mimi ningekuwa Mamlaka yao ya nidhamu ningewafukuza kazi. Kwa sababu Makosa yao kwenye pande zote mbili (kwenye Kanuni za Utumishi wa Umma na kwenye Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma) adhamu yake ni kufukuzwa kazi mara moja baada ya kufunguliwa mashataka ya kukiuka Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma na kwenye Uongozi wa Umma nao unatenguliwa cheo chako ili uwapishe watumishi wenye uadilifu.

Ni sawa na Butiku anatoa siri za Vikao vya NET. Sheria ya mwaka 1981ya Viongozi wa Umma na ile ya mwaka 1995 zinasema Kiongozi yoyote wa Umma au Mtumishi yoyote wa Umma aliyekabidhiwa madaraka na nyadhifa ya Utumishi wa Umma na Uongozi wa Umma mara atakostaafu HATATAKIWA KUTOA AU KUELEZA JAMBO LOLOTE lililoamuliwa kwenye VIKAO AMBAVYO MASUALA YAKE AU MAAMUZI YAKE HAYATAKIWI KUTOLEWA. NA ATAKAPOKIUKA ATAFUNGULIWA MASHASTAKA YA KUTOA SIRI KAMA ILIVYO SIRI ZA BARAZA LA MAWAZIRI.

Huyu mtu mimi nashangaa mpaka sasa hajakamatwa. Ningekuwa Mimi ni Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Butiku angekuwa "KOROKORONI" akisubili hatua nyingine za kupelekwa MAHAKAMANI.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,872
2,000
KWANZA ilikuwa ni ndani ya chama tawala CCM, lakini malumbano baina ya vigogo sasa yamehamia serikalini baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi kujibu mashambulizi ya mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, akitaka uitishwe mdahalo baina ya wawili hao ili ajibu tuhuma dhidi yake.

Na Mkuu wao wa kazi kama kawaida yake yuko kimyaaa!
 

Ex Spy

Senior Member
Jan 15, 2007
184
1,000
Itabidi wawe na mdahalo lakini wasizuie kurushwa LIVE. Maana naona Hoseah kaliibua tena

:fencing:
 

Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,653
2,000
wadau km mtwaelewa vizuri hawa wateule vizuri, wengi wao kwa mfano kwenye maoni ya katiba mpya wanataka rais apunguziwe madaraka au post zao zisiwe za kiteule toka kwa rais. Kikwazo kikuuubwa hapo ni Jk, na ndio mzigo wenyewe huo, wanashindwa kufanya lolote sababu ya washkaji wa jk walomweka madarakani anawalinda
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,992
2,000
Nimetafakari juu ya hili suala, na kutambua kwamba wote Hosea na DPP wako sahihi. Hosea kapeleka mafaili zaidi ya 60 kwa DPP, na DPP hajayapata. Suala ni kwamba yameishia wapi?

Ukweli unaobaki ni kwamba kuna wajanja wachache wameyageuza mradi, wakijua kwamba hizi taasisi mbili haziko jengo moja. Mafaili ya hizi kesi yanaishiwa hewani, ikimaanisha kuna watu wanawauzia wenye kesi ili yapotee hewani - yamechakachuliwa!

Kilichobaki, ni DPP na Hosea kukaa ili waone nani amekuwa akifanya mchezo huu mchafu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom