DPP amuondolea Mashitaka Mustapha Kambanwa aliyedaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Tsh 188.9 Bilioni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
MKURUGENZI wa Mashitaka nchini (DPP), amewasilisha hati katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kwamba anamuondolea mashitaka mfanyabiashara Mustapha Kambangwa ambaye alikuwa anakabiliwa na mashitaka yake manne yakiwemo kuisababishia Serikali hasara ya sh.bilioni 188.9.

DPP aliwasilisha hati hiyo leo Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Luambano na kusema hana nia ya kuendelea kumshitaki.

Baada ya kusema hayo Hakimu Luambano, alisema mshitakiwa anamwachia huru

Awali Wakili wa Serikali Ashura Mnzava, alidai shauri lilipelekwa kwa kutajwa ambapo DPP hana nia ya kuendelea kumshitaki mshitakiwa hivyo anayaondoa mashitaka yote dhidi yake.

Kambangwa alikuwa anakabiliwa na mashitaka manne likiwemo kusababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) hasara ya sh. bilioni 188.9 kwa kupitia mashine ya kielekroniki.

Mshitakiwa Kambangwa alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Desemba 7, mwaka 2018 ambapo alisomewa mashitaka katika kesi ya uhujumu uchumi .

Inadaiwa mshtakiwa anakabiliwa na mashitaka manne aliyoyatenda katika siku tofauti kati ya Juni Mosi , mwaka 2016 na Novemba 2, mwaka 2018

Alidai katika mshitaka ya kwanza, Kambangwa alijifanya kama mtu aliyesajiliwa kuwa mlipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT)

Alidai katika tarehe tofauti kati ya Juni Mosi, mwaka 2016 na Novemba 2, mwaka 2018 maeneo ya jiji la Dar es Salaam mshitakiwa alijifanya kuwa amesajiliwa kukusanya kodi ya VAT sh. 188,928,752,166 kwa kujifanya anakusanya fedha hizo kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Katika mashitaka ya pili, alidai Juni Mosi, 2016 na Novemba 2, mwaka 2018 Kambangwa kwa udanganyifu alitumia mashine ya kieletroniki ya EFD yenye namba 03TZ842011315 iliyosajiliwa kwa jina la Kampuni ya Abraham's Group LTD kukwepa kodi ya VAT yenye thamani ya fedha hiyo.

Katika mshitaka ya utakatishaji fedha, tarehe na kipindi hicho, maeneo ya jiji la Dar es Salaam alijipatia au kujimilikisha fedha hizo alizozipata kutokana na makato ya kodi ya VAT ambazo zilipaswa kutolewa kwa Kamishna wa TRA na mshitakiwa huyo alipaswa kujua kuwa fedha hizo bi zao la kosa la ukwepaji kodi.

Ilidaiwa katika tarehe tofauti kati ya Juni Mosi, mwaka 2016 na Novemba 2, mwaka jana maeneo ya Dar es Salaam kwa vitendo vya makusudi vya kukwepa kodi alitumia mashine ya kieletroniki ya EFD na huku akijua kwamba hajasajiliwa kama mlipakodi ya VAT aliisababishia TRA hasara ya sh. 188,928,752,166

Zaidi, soma;
1). Mustapha Kambangwa afikishwa mahakamani kwa mashtaka manne likiwemo la kukwepa kodi na kujipatia Sh.bilioni 188.9 kupitia mashine ya kieletroniki (EFD
 
... watu waliteseka sana awamu ya tano! Unamweka mtu mahabusu for 3 years then very simply unasema huna nia ya kuendelea na kesi? Si zaidi ya ushetani huu?
 
Hapa cdm yanatetea mafisadi na mabeberu ila wanyonge hayawatetei hata chembe
 
Moderator rekebisha taito yako,kama una ushahidi wa Must kusabibisha hasara si ungeenda kusaidia DPP? Sio alisababishia hasara bali aliyetuhumiwa kusababishia hasara
Mkuu upo sahihi mwandishi wa mada hii utafikiria kasomea kwa Musiba,huyu alikua suspect sasa mwandishi huyu ameshamhukumu na kumwona na kosa la kusababisha serikali ipoteze fedha hizo wakati sio kweli,kichwa cha habari cha mada hii ni cha UONGO.
 
Halafu kuna watumishi sh elf 5 ya soda wanafukuzwa kazi lakini mijizi mikubwa inabadilishwa vituo tu,au halmashauri iendelee kuiba
 
Mafisadi wanaachiwa huru, hapo mjuba kapenyeza rupia kwa DDP halafu kaachiwa huru, Magufuli anaonekana mbaya.

Number don't lie, endeleeni kushangilia mama anaupiga mwingi
Saaaaagudaaaa sasagudaaaaaa nakuitaaa kwa sauti Saguda47 mtu wangu Dogo Saguda47 bado unazile ruby rangi ya marvy?
 
Mafisadi wanaachiwa huru, hapo mjuba kapenyeza rupia kwa DDP halafu kaachiwa huru, Magufuli anaonekana mbaya.

Number don't lie, endeleeni kushangilia mama anaupiga mwingi
Dikteta alikuwa anafunga watu kiuonevu,Sasa kama jela kuzuri mpeleke mama yako nae akakae,

Kubwa zima linamuabudu mtu ambae ameshajiozea chini ya ardhi,

Rais Ni Samia kwasasa, huyo magufuli wako Kama unampenda Sana jiue umfuate
 
Mafisadi wanaachiwa huru, hapo mjuba kapenyeza rupia kwa DDP halafu kaachiwa huru, Magufuli anaonekana mbaya.

Number don't lie, endeleeni kushangilia mama anaupiga mwingi
Hama Nchi, magufuli hakuwa na hatimiliki ya hii Nchi jinga wewe!!, Acha DPP afanye kazi yake
 
Back
Top Bottom