DPP amesoma gazeti la Jamhuri?

Daniel Mjema

Member
Jul 23, 2007
77
84
Ukitizama hili sakata na ukijumlisha 1+1 utabaini kuna jambo linaloendelea nyuma ya pazia hasa zile fununu za rupia.

DCI wanasema wana ushahidi madhubuti dhidi ya matajiri wale wa Mwanza lkn tangu wakamatwe tarehe 11.1.2016 na jalada kupelekwa kwa DPP tarehe 20.1.2016 hadi leo hajaandaa hati ya mashitaka.

Hii italeta tafsiri mbaya baadae. Someni maoni ya mhariri wa Jamhuri nimeyaambatanisha hapa
 
Attachments

  • IMG-20160223-WA0014.jpg
    IMG-20160223-WA0014.jpg
    86.5 KB · Views: 81
Wanashindwa kusoma alama za nyakati.

Uchunguzi huo mpya umetokana na agizo la Rais. DCI kafanya wajibu wake kwa uadilifu mkubwa hasa ikizingatiwa jalada la awali liliibwa ofisi ya RCO Kilimanjaro.

Leo mnaletewa ushahidi madhubuti tena uliotokana na agizo la Rais mnakaa na file mwezi mzima. Jamii itawaelewaje?

Wala hakuna kuzushiwa hapa
 
Kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia kuhusiana na hili sakata la watuhumiwa wa mauaji ya james massawe,haiwezekani DCI amekamilisha uchunguzi,akapeleka jalada kwa DPP,DPP anaanza kuhoji maswali mengiiiiiiiiii kana kwamba ofisi ya DCI ina njama na watuhumiwa.

Tunaweza kuamini fununu zilizozagaa katika mji wa moshi kwamba ofisi ya DPP imepenyezewa fungu nono ili kukwamisha kesi hiyo,lakiniyawezekana ikawa kweli kwani ni ofisi hiyo hiyo ya DPP ndiyo iliyofuta kesi ya awali kwa madai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kuweza kuwatia hatiani washitakiwa wa awali.

Hebu tumuulize DPP,anataka ushahidi gani ili aandae mashitaka dhidi ya hao watuhumiwa ambao mpaka sasa wapo kituo kikuu cha polisi mjini moshi bila kujua hatima yao?.

Kwa mwenendo huu,ni kesi ngapi zinazimwa ofisi ya DPP na watu wangapi wamenyimwa haki kwa mtindo huu wa ofisi ya DPP kukwamisha kesi?

DPP ana maslahi gani na hawa watuhumiwa wa mauaji kiasi kwamba anauwekea vikwazo vingi uchunguzi wa makachero kutoka ofisi ya DCI?
 
Hapo shida ni mpunga unatembezwa tu mwanzo wa hiyo case rpc ngomboko wa kilimanjaro aliwabeba cz ya urafiki.....wameishi mafichoni karibia miaka 4 pia ushahidi wa mauaji uko wazi sana mana marehemu aliuawa kwa kipigo hku wanakijiji wakiangalia
 
Kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia kuhusiana na hili sakata la watuhumiwa wa mauaji ya james massawe,haiwezekani DCI amekamilisha uchunguzi,akapeleka jalada kwa DPP,DPP anaanza kuhoji maswali mengiiiiiiiiii kana kwamba ofisi ya DCI ina njama na watuhumiwa.

Tunaweza kuamini fununu zilizozagaa katika mji wa moshi kwamba ofisi ya DPP imepenyezewa fungu nono ili kukwamisha kesi hiyo,lakiniyawezekana ikawa kweli kwani ni ofisi hiyo hiyo ya DPP ndiyo iliyofuta kesi ya awali kwa madai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kuweza kuwatia hatiani washitakiwa wa awali.

Hebu tumuulize DPP,anataka ushahidi gani ili aandae mashitaka dhidi ya hao watuhumiwa ambao mpaka sasa wapo kituo kikuu cha polisi mjini moshi bila kujua hatima yao?.

Kwa mwenendo huu,ni kesi ngapi zinazimwa ofisi ya DPP na watu wangapi wamenyimwa haki kwa mtindo huu wa ofisi ya DPP kukwamisha kesi?

DPP ana maslahi gani na hawa watuhumiwa wa mauaji kiasi kwamba anauwekea vikwazo vingi uchunguzi wa makachero kutoka ofisi ya DCI?

Penyeza ujumbe kwa Ombeni Sefue!
 
Ugumuu hunakuja hapa .kurudishwa kwa mashtaka kutafukuzisha watu wengi kazi.kwa DDP na polisi .kwahiyo hakuna namna zaidi ya kungangania uwamuzi wao Wa mwanzo wabaki kazini.au wageuze uamuzi watumbuliwe majipu ya kuwa walikula rushwa .
 
NINA USHAHIDI MZITO WA JAMBO hili, nimetumia private investigators namsubiri DPP kwa hamu nimlipue. ELIEZER FELESHI aliyekuwa DPP anajua ukweli wa jambo hili hautamuacha salama.
 
Siku marehemu anauwawa ata mm nilikuwa nashudia kwa macho yangu mawili ushaidi mwingine mzuri upo ITV wandishi walikuja kijijini wakaoji watu paka watoto walikuwa wanatoa ushaidi wao walichokiona kama wanataka kesi hii isiwe na mlolongo zitolewe zile video ITV
 
NINA USHAHIDI MZITO WA JAMBO hili, nimetumia private investigators namsubiri DPP kwa hamu nimlipue. ELIEZER FELESHI aliyekuwa DPP anajua ukweli wa jambo hili hautamuacha salama.
Unaweza kutueleza ni sababu zipi zilizomfanya Judge Dr Feleshi aiondoe kesi ile mahakamani kipindi kile?
 
Ukitizama hili sakata na ukijumlisha 1+1 utabaini kuna jambo linaloendelea nyuma ya pazia hasa zile fununu za rupia. DCI wanasema wana ushahidi madhubuti dhidi ya matajiri wale wa Mwanza lkn tangu wakamatwe tarehe 11.1.2016 na jalada kupelekwa kwa DPP tarehe 20.1.2016 hadi leo hajaandaa hati ya mashitaka. Hii italeta tafsiri mbaya baadae. Someni maoni ya mhariri wa Jamhuri nimeyaambatanisha hapa

Moshi kunafuka moshi tuwapelekee zima moto?.

Msitushone midomo, niliwahi sikia ya JeiJey
 
Kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia kuhusiana na hili sakata la watuhumiwa wa mauaji ya james massawe,haiwezekani DCI amekamilisha uchunguzi,akapeleka jalada kwa DPP,DPP anaanza kuhoji maswali mengiiiiiiiiii kana kwamba ofisi ya DCI ina njama na watuhumiwa.

Tunaweza kuamini fununu zilizozagaa katika mji wa moshi kwamba ofisi ya DPP imepenyezewa fungu nono ili kukwamisha kesi hiyo,lakiniyawezekana ikawa kweli kwani ni ofisi hiyo hiyo ya DPP ndiyo iliyofuta kesi ya awali kwa madai kuwa hapakuwa na ushahidi wa kuweza kuwatia hatiani washitakiwa wa awali.

Hebu tumuulize DPP,anataka ushahidi gani ili aandae mashitaka dhidi ya hao watuhumiwa ambao mpaka sasa wapo kituo kikuu cha polisi mjini moshi bila kujua hatima yao?.

Kwa mwenendo huu,ni kesi ngapi zinazimwa ofisi ya DPP na watu wangapi wamenyimwa haki kwa mtindo huu wa ofisi ya DPP kukwamisha kesi?

DPP ana maslahi gani na hawa watuhumiwa wa mauaji kiasi kwamba anauwekea vikwazo vingi uchunguzi wa makachero kutoka ofisi ya DCI?
DPP Hafanyi kazi kwa mitulinga
Kama ushahidi ni dhaifu kulingana na shitaka unataka DPP atoe kibali ambapo kesi itaanguka ikisomwa tu.
Tatizo la polisi ni wavivu kupeleleza,hawana wapelelezi mahiri na ukosefu wa nyenzo.
Ili kufunika kombe wasionekane wanawabeba watuhumiwa,wanawakamata tu halafu jalada wanasukumia kwa DPP ili aonekane ndio anakwamisha.
DPP amesaidia wengi,siku hizi hakuna kesi za kubambikiwa,ndio mana hata polisi wanagwaya kupeleka kesi za kubambikia kwa DPP
 
Huwa nawashangaa sana watu wanavyokurupuka na kuanza kumlaumu DPP kana kwamba DPP ndo chombo chunguzi, anayemjua vizuri Jaji Feleshi hawezi kaa hata siku moja akadai alihongwa waulize wanasheria wa serikali na hao mapolisi watakueleza Feleshi ni mtu wa aina gani.
 
Ndugu zangu,

Nimeona kuna member ametaka kujua kesi hii ilifutwa kwa sababu gani. Kesi ya awali ilifutwa na DPP mwaka 2012 kwa kutumia kifungu namba 94(3)(c) cha CPA na kifungu hicho alichokitumia kufuta kesi ya awali hakimzuii DPP kuifungua upya kesi hiyo kwa facts zile zile.

Mimi nilifuatilia sana kesi hii na naifahamu vizuri kwamba DPP aliiondoa baada ya kubaini postmoterm Report iliyokuwemo kwenye file ilikuwa doctored na ilikuwa haitoi sababu za kifo. Kwa maneno kutokana na kuchezewa huko, report hiyo ilikuwa haionyeshi clearly sababu za kifo. Utata huo umeisha baada ya uchunguzi mpya kumpata daktari aliyefanya postmoterm ambaye wakati anahojiwa na kikosi kazi kilichoundwa na DCI alisema report ile ya awali si yake kwani imeongezewa maneno na kuifanya ilete utata kuhusu the actual cause of death. Daktari huyo bahati nzuri under escort ya polisi alirudi KCMC na kuproduce original report. Sababu ya pili ya kufutwa kwa kesi ile ilikuwa kwamba key suspects waliokuwa wakitajwa na mashahidi sio waliokuwa mahakamani. Lkn sasa wamekamatwa watuhumiwa wenyewe. Pili, ieleweke kuwa kesi ile ya awali haikuwahi kusikilizwa wala mashahidi kutoa ushahidi wao. Hivyo japo mashahidi wameongezeka lkn hiyo ndio imesaidia kuijenga kesi hii kulinganisha na PI 9/2009. Ninaposema ninaifahamu, ninaifahamu in and out. Ushahidi mpya wa mashahidi 17 ni mzito kwani unahusisha pia maelezo ya vijana watatu waliokuwa wakiteswa sambamba na marehemu hadi mwenzao alipopoteza maisha.Upo ushahidi wa mwanamke mmoja ambaye alishuhudia tukio zima mwanzo mwisho. Ikumbukwe kuwa ushahidi huu mpya uliookusanywa unatokana na agizo la Ikulu baada ya ndugu wa marehemu kulalamika kutokamatwa kwa watuhumiwa hao muhimu. Na ikumbukwe original file la mwanzo la polisi lililokuwa na maelezo yote liliibwa kimafya katika ofisi ya RCO Kilimanjaro na nakala za jalada hizo zilizokuwa ofisi nyeti za Serikali nazo ziliibwa. Ninafahamu baadhi ya maofisa wanaohusishwa na njama za kuibwa kwa file hilo wamechukuliwa hatua za kinidhamu huku mmoja akihamishiwa Morogoro kutoka Moshi na mwingine akiondolewa kutoka CID department na kuvalishwa magwanda na kupelekwa kituo cha TPC. Ushahidi uliokusanywa ni mzito na mimi kama mwanahabari niliyelifuatilia sakata hili tangu mwanzo tunasubiri DPP kama hatapeleka suala hilo mahakamani kwa kisingizio chochote kile tutaanika ushahidi wote uliokusanywa halafu umma wa watanzania utapima wenyewe kama kweli DPP alikuwa na sababu za kushikwa kigugumizi kwa zaidi ya siku 40 tangu alipopelekewa jalada la kesi hii. Yapo mengine yaliyojificha ambayo tutayaanika muda ukifika.
 
Tunasubiri kwa HAMU ndugu MJEMA....hebu nisaidie kidogo kuwajua hawa watuhumiwa ni JEURI ya PESA tuu au kuna kitu kingine kinachofanya hadi watu wenye Dhamana kubwa huko kwenye Maofisi ya Serikali wanapata kiGUGUMIZI chakumaliza hii issue sababu nimelisikia jambo hili siku nyingi watuhumiwa wanaogopeka sana wananini cha ziada?
 
Ndugu zangu,

Nimeona kuna member ametaka kujua kesi hii ilifutwa kwa sababu gani. Kesi ya awali ilifutwa na DPP mwaka 2012 kwa kutumia kifungu namba 94(3)(c) cha CPA na kifungu hicho alichokitumia kufuta kesi ya awali hakimzuii DPP kuifungua upya kesi hiyo kwa facts zile zile.

Mimi nilifuatilia sana kesi hii na naifahamu vizuri kwamba DPP aliiondoa baada ya kubaini postmoterm Report iliyokuwemo kwenye file ilikuwa doctored na ilikuwa haitoi sababu za kifo. Kwa maneno kutokana na kuchezewa huko, report hiyo ilikuwa haionyeshi clearly sababu za kifo. Utata huo umeisha baada ya uchunguzi mpya kumpata daktari aliyefanya postmoterm ambaye wakati anahojiwa na kikosi kazi kilichoundwa na DCI alisema report ile ya awali si yake kwani imeongezewa maneno na kuifanya ilete utata kuhusu the actual cause of death. Daktari huyo bahati nzuri under escort ya polisi alirudi KCMC na kuproduce original report. Sababu ya pili ya kufutwa kwa kesi ile ilikuwa kwamba key suspects waliokuwa wakitajwa na mashahidi sio waliokuwa mahakamani. Lkn sasa wamekamatwa watuhumiwa wenyewe. Pili, ieleweke kuwa kesi ile ya awali haikuwahi kusikilizwa wala mashahidi kutoa ushahidi wao. Hivyo japo mashahidi wameongezeka lkn hiyo ndio imesaidia kuijenga kesi hii kulinganisha na PI 9/2009. Ninaposema ninaifahamu, ninaifahamu in and out. Ushahidi mpya wa mashahidi 17 ni mzito kwani unahusisha pia maelezo ya vijana watatu waliokuwa wakiteswa sambamba na marehemu hadi mwenzao alipopoteza maisha.Upo ushahidi wa mwanamke mmoja ambaye alishuhudia tukio zima mwanzo mwisho. Ikumbukwe kuwa ushahidi huu mpya uliookusanywa unatokana na agizo la Ikulu baada ya ndugu wa marehemu kulalamika kutokamatwa kwa watuhumiwa hao muhimu. Na ikumbukwe original file la mwanzo la polisi lililokuwa na maelezo yote liliibwa kimafya katika ofisi ya RCO Kilimanjaro na nakala za jalada hizo zilizokuwa ofisi nyeti za Serikali nazo ziliibwa. Ninafahamu baadhi ya maofisa wanaohusishwa na njama za kuibwa kwa file hilo wamechukuliwa hatua za kinidhamu huku mmoja akihamishiwa Morogoro kutoka Moshi na mwingine akiondolewa kutoka CID department na kuvalishwa magwanda na kupelekwa kituo cha TPC. Ushahidi uliokusanywa ni mzito na mimi kama mwanahabari niliyelifuatilia sakata hili tangu mwanzo tunasubiri DPP kama hatapeleka suala hilo mahakamani kwa kisingizio chochote kile tutaanika ushahidi wote uliokusanywa halafu umma wa watanzania utapima wenyewe kama kweli DPP alikuwa na sababu za kushikwa kigugumizi kwa zaidi ya siku 40 tangu alipopelekewa jalada la kesi hii. Yapo mengine yaliyojificha ambayo tutayaanika muda ukifika.
Ambiere!Unaweza kuwa na ushahidi hata tani 5 lakini kama huna mlalamikaji atakaeweza kuishawishi mahakama pasi na shaka yoyote ni kazi bure
Ushahidi hata ujae lori zima lakini kama una mashaka ni kazi bure.
umebainisha daktari alikataa ripoti ya awali na kusema ilichezewa.ilibidi apelekwe under escort kutengeneza cheti kingine!
Hapo pana utata,kwanza daktari hakufanya tena postmortem ya pili,hapo ushahidi umehama,pia kitendo cha kumsindikiza daktari chini ya ulinzi,inaonesha ripoti kaiandika kwa shinikizo kitu ambacho hakileti mizani kwenye haki.
Naomba tumuite Pasco atudadavulie labda anaweza kukutuliza kidogo
 
Back
Top Bottom