Doyo Hassan Doyo karata dume ya CHADEMA kuiteka Tanga

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,186
79,378
Wasalaam Aleihkum wana JF,

Wahenga wanasema "vita vya panzi furaha ya kunguru na pia adui yako muombee njaa! Huu ndio ujumbe ninaoweza kuutoa hapa leo JF: nina uhakika hamna anayefurahia migogoro katika vyama vya Upinzani lakini vilevile migogoro ni fursa njema ya kuangalia uelekeo na mrengo wa mwanasiasa haswa kama itikadi zinakinzana baina ya wahusika ndani ya chama na sera za chama! Mbali ya kuwa waliofukuzwa uanachama walikuwa wakipigania katiba, taratibu na sera za chama zizingatiwe na kuheshimiwa likiwamo pia suala la ubadhirifu kuzungumziwa bila kusikilizwa basi ni muda muafaka kwa wahusika kuanza kuangalia jahazi lingine litakalo wafikisha ng'ambo ya pili!

Madhalaaani CHADEMA imekuwa ikipata ugumu kujipenyeza katika zile ngome za Pwani basi tuchukulie fursa hii ya kuvuliwa uanachama Doyo Hassan Doyo kama mtaji wa kujitanua na kuuza sera huko Pwani! Naomba wahusika katika CHADEMA kufanya juu chini kumkaribisha huyu bwana kundini maana ni ukweli usiopingika CHADEMA imekuwa ikipata mapokeo hafifu Pwani na Visiwani! Japokuwa ninajua pia Hamad Rashid ni mtaji pia huko Wawi Pemba ila kwa siasa za kinazi za Zanzibar sina uhakika sana kama ana ushawishi mkubwa kuwabadili wapemba kuona nyeusi ni nyeupe! Siasa za visiwani kama tunavyojua zimejaa majungu, visasi na chuki na hata matokeo ya leo yaliyowavua uanachama waliokuwa wana CUF leo yameonyesha kutokuwa na Mzanzibari hata mmoja aliyeweza kung'amua Seif anaipeleka kubaya CUF na mustakabali wa Maridhiano ni kukosa upinzani wa kuikosoa serikali.

Tumeona jinsi suala la MV Spice Island lilivyogeuzwa likawa suala la kishabiki na kuhusishwa hata bara katika ajali hiyo wakati meli iliruhusiwa kuondoka na viongozi wa bandari ya Unguja! Hii yote ni kuondoa uwajibikaji kwa wahusika akiwemo mmiliki wa meli ile ambaye naskia yuko ndani ya Baraza la wawakilishi! Mbali ya kuwa wengi wa walipoteza maisha walikuwa Wapemba CUF imenyamaza kimya bila ya kuunlizia ripoti na uwajibikaji! Kisa Maalim Seif amefungwa mdomo amekuwa joka la kibisa sasa haling'ati bali labwia sembe za mchezesha kibisa
!

Ni hayo tu wenye dhamira safi ya kutufikisha katika demokrasia ya kweli wanaanza kuonekana sasa...
 
Ha ha ha ha te te te te te te! nimecheka sana hapo kwenye red, humu JF mna raha zake!!!!
 
Labda huyo doyo hassan lkn hamad rashid si riziki kwa chadema hata kidogo
 
Tatizo la kanda ya Pwani na Zanzibar ni udini na elimu duni!

Na TIBA yake ni rahisi tu. Mfundisheni Dr Slaa kuvaa kanzu na kibandiko. Na akipenda anaweka koti juu. Nyerere alifanya hivyo akakubalika. Mrema pia alijaribu kwa kanzu bila koti.
 
Umetoa ushauri kama wa Sheikh Yahya Hussein.
 
Wadau nimemsikiliza doyo, jamaa ni kichwa sana, anachambua cuf na kuichana chana pwaaa, yupo star tv live.
Jamaa ni mkali.
 
KAMA NI MKALI MBONA AMESHINDWA KUONYESHA UKALI HUKO (CUF) a.k.a CCM-B? AKAFIE ZAKE HUKO KAMA SIO KU-DOYOLEWA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tongindi, siasa za bongo huzijui eee, umri wa kama sikosei ukizidi sana ni miaka 24, so umri huuwezi juwa nini siasa ndomana una kurupuka doyo anaongea vizuri anaichana cuf, kipi kizuri anachokiongea mpaka kimepelekea kupost uharo humu jamvini
 
Back
Top Bottom