Masikini Afrika na vipaji vyake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
Jana usiku rafiki yangu kaniletea clip ya huyu mzee anapiga gitaa mtaani.

Huyu sahib yangu kaniletea hii clip kwa kuwa ni mimi ndiye niliye mtia yeye kwenye muziki wa kupiga gitaa kupitia muziki wa Mwenda Jean Bosco.

Yafuatayo hapo chini ni mazungumzo yetu:

Ingekuwa Ulaya recording companies zishamfuata kwa haraka na nyimbo ziko kwenye CD.

Afrika ataishia kuvaa koti jua kali na vumbi linampiga.
Umesema kweli..

Huyu Feruzi nyimbo hii kapiga na Franco lyrics anamsimanga tajiri aliyemkuta mtaani anapiga accordian iliyochoka akamuahidi mpya.

Hakutimiza miadi yake.
Soma title ya nyimbo.

These were creative geniuses

Hugh Tracey 1952 kamkuta Mwenda Jean Bosco mtaani anapiga gitaa.

Akamrekodi tape ikaenda Gallotone Johannesburg, South Africa.

Iliyobakia ni historia.

Peter Colmore kamkuta Edward Masengo River Road, Nairobi
ndani ya kilabu cha pombe kakaa chini walevi wamemzunguka anawaburudisha na gita lake akamtoa pale akamtia kwenye studio za High Fidelity Productions.

Masengo akawa star mkubwa Afrika Mashariki na kwao Congo.

1562039772203-png.1144356

Umeikamata spirit ya wakati
Wamanyema kukwezana!

Ndo ukweli ambao Wamanyema wapewa kipaji cha kuutambua!

Nasoma Nyaraka za Sykes.

Ndani nakuta barua ya Hugh Tracey akiwa Sauti ya Dar es Salaam amemwandikia barua mbaya sana Kasella Bantu afukuzwe kazi hana adabu kwa Wazungu.

Hapo namwambia, "Baba hizi nyaraka ndiyo historia ya harakati za kupigania uhuru zifungue zienda Nyaraka za Taifa."

Haya maneno yangu kayasikia mara elfu.
Siku nyingine ananijibu siku nyingine ananipuuza.

Akifurahi ataniuliza, "Wewe ushakunywa chai?"

Nikisema sijanywa anavuta pochi lake ananambia, "Unajua bwana kama mtu hajanywa chai asubuhi maneno mengiiiiii!"

Hapo ndiyo nichukue hela nikanywe chai niache kumbughudhi.

Udongo unakula watu.

Nyaraka sasa anazo nani?

Anazo mama Bi. Zainab.

Si nyaraka tu na mswada nilioandika na Bwana Ally kuhusu maisha yake upo na hizo nyaraka.

Lakini leo najua kwa nini Bwana Ally alikuwa anajidai.

Alipojua kama zile nyaraka kanifungulia mie na ninaandika kitabu sasa alichokuwa anasubiri kitabu kitoke na dunia ijue Nyaraka za Sykes zina nini.

Sasa dunia ishazijua hizi nyaraka na kama ulimwengu unazijua kuwa zipo na zina historia ya uhuru wa Tanganyika kwake hiyo inatosha.

Jonathon Glassman wa Northwestern University kwenye review ya kitabu cha Sykes katika Cambridge Journal of African History kazitaja ingawa zimemkera.

Ila namshuhukuru kwani alinialika ''impromptu,'' kwenda kuzungumza chuoni kwake baada ya mhadhara niliofanya University of Iowa ambae alikuwako siku ile.

Wazee wa zamani wana hikma za aina ya kipekee.

Iko siku nilikuwa mubashara Azam TV Morning Trumpet nazungumza
historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nadhani ilikuwa wakati wa Saba Saba.

Nilipomaliza niko njianinarudi nyumbani nikapokea simu.

Ilikuwa waandishi wa habari wananambia kuwa wameniona na historia niliyoeleza imewasisimua lakini wana miadi na Mama Maria Nyerere wanaomba wakitoka huko waje kunihoji.

Basi wakaja na camera man.

Tukafanya kipindi na wakaomba niwajulishe kwa Bi. Zainab.

Walifika kwa Bi. Zainab na aliwapokea vizuri na aliwapandisha
hadi juu kwenye ofisi ya marehemu mumewe kwa sharti wasiguse chochote lakini wapige picha wazitakazo.

Hii video ninayo nitakurushia In Shaa Allah.

In Shaa Allah naisubiri.



Msomaji wangu ikiwa unataka historia zaidi za watu hawa ingia:

https://mohamedsaidsalum.blogspot.com/…/kutoka-jf-ally-syke…
 
Back
Top Bottom