DOWANS yaibwaga TANESCO; TZ kulipa gharama na adhabu Bil. 185!

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,032
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,032 280
International Chamber of Commerce, imetoa hukumu yake katika kesi iliyoletwa na Dowans (T) Ltd kupinga uamuzi wa Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans.. Hukumu hiyo inaonesha kuwa Tanesco imebwagwa vibaya na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu pamoja na gharama ya kesi kwa Dowans.. Hesabu za kwangu zinaonesha gharama mbalimbali za kesi na adhabu zinazidi Dola milioni 120! Mtu mwingine kanipigia hesabu anasema Dola milioni 180 ngoja wakija public sijui itakuwa figure ipi..

Habari (Mwananchi, December 2, 2010)

Na Waandishi Wetu
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limeamriwa kulipa fidia ya Sh106 bilioni kwa kampuni ya ufuaji umeme ya Dowans Tanzania Limited baada ya kuvunja mkataba.Uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru Tanesco iilipe Dowans kiasi hicho cha fidia.

"Jopo la wasuluhishi limeamuru zaidi ya Sh36bilioni (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya Sh 26bilioni (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa,' imeeleza sehemu ya uamuzi huo.

Pia jopo hilo la wasuluhishi wa migogoro ya kibiashara liliamuru Sh60bilioni (sawa na dola za kimarekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na Sh 55bilioni (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.

Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala Sh1bilioni (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zinatakiwa zilipwe na pande zote husika.

"Tanesco wanatakiwa kumlipa mdai (mlalamikaji) Sh3bilioni (dola 1,708, 521) ikiwa ni gharama za uendeshaji wa kesi na gharama zingine na kwamba madai mengine yaliyotolewa na pande zote katika kesi hiyo yanatupwa.

Mpango wa kuuza mitambo hiyo uliwahi kuibua mjadala mzito nchini huku baadhi ya wabunge akiwemo mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe wakikubaliana na dhamira hiyo jambo lililosababisha serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kutangaza rasmi kuwa haina mpango wa kununua mitambo hiyo.

Kufuatia uamuzi huo Dowans iliamua kutangaza kuiuza mitambo yao nje ya nchi jambo lilosababisha serikali kuiwekea pingamizi katika Mahakama ya Biashara ikitaka wamalize kwanza masuala ya mikataba.

Siku chache baadaye Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), iliikamata mitambo hiyo kwa madai kuwa ilikuwa ikidaiwa ushuru.

Hatua ya kuiwekea pingamizi ili mitambo hiyo isiuzwe ilipigwa vikali na Dowans na kuamua kukimbilia katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court) iliyopo nchini Ufaransa ili kuhakikisha mitambo hiyo inaweza kuuzwa.

Lakini taarifa iliyotolewa na Dowans jana ilionyesha kuwa mgogoro huo umepatiwa ufumbuzi na kwamba kampuni hiyo na Tanesco sasa wamekubaliana baada ya mahakama hiyo kuketi.

"Jopo la waamuzi uliojumuisha waamuzi watatu chini ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), limetoa tunzo kuhusu mgogoro baina ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited (kwa pamoja ‘Dowans'), kwa upande mmoja dhidi ya Tanesco kwa upande mwingine.

"Dowans wameridhika na tunzo iliyotolewa na jopo hilo na kwa matokeo hayo wanayo furaha kuutangazia umma kuwa mgogoro baina yetu na Tanesco sasa umekwisha,"alisema sehemu ya taarifa hiyo.

Akizungumzia uamuzi wa kumaliza mgogoro huo baina ya Tanesco na Dowans, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alisema hajapata taarifa hiyo rasmi wala maamuzi yaliofikia katika mahakama hiyo.

"Kwa sasa nipo nje ya ofisi kama ni kweli Mahakama hiyo imeweza kuwasuluhisha ni lazima nitaletewa taarifa na kuweza kusoma rasmi ili kujua iwapo katika makubaliano hayo suala la kuuza mitambo hiyo nalo wamekubaliana nalo au la ndio nitaweza kuzungumza chochote,"alisisitiza Waziri Ngeleja.

Waziri Ngeleja alisema kuwa anachojua yeye pingamizi la serikali lipo mahakamani na kwamba hakuna mabadiliko yoyote.

Kwa upande wa Tanesco, Meneja Uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud alipoulizwa alisema kwa sasa Tanesco hawezi kusema chochote watatoa taarifa mara baada ya uongozi wa Tanesco kukutana.

Mara ya kwanza dhamira hiyo ya serikali kupitia Tanesco kutaka kununua mitambo ya Dowans, iliibua mjadala mkali miongoni mwa Watanzania, huku wakionyesha shaka kuhusu uamuzi huo.

Mjadala huo ulitokana na malumbano ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na Shellukindo na ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyokuwa chini ya Zitto (Chadema). Kati Kamati ya Shellukindo ikisisitiza kutokuwepo umuhimu kwa Tanesco kununua mitambo hiyo.

Mvutano wa kamati hizo ulikuwa mkubwa, baada ya Zitto kusisitiza kuwa atamuomba Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuitisha mkutano wa kamati hizo mbili ili kujadili upya suala hilo na kwamba utetezi wake wa kununua mitambo hiyo unatokana na kuweka mbele maslahi ya taifa.

Wakati huo, Watanzania wengi ambao walikuwa wakitoa maoni yao kwa gazeti hili kwa njia ya simu za mkononi na katika mitandao ya ‘internet', walionyesha kupingana katika suala hilo, jambo linaloonyesha kuwapo kwa mgawanyiko wa wazi kuhusu kununuliwa au kutonunuliwa kwa mitambo hiyo.

Kutokana na mjadala huo uliochukua mwelekeo wa kupinga ununuzi wa mitambo hiyo, hatimaye Tanesco ilitangaza kuondoa nia yake hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa mjadala wake umechukua sura ya kisiasa kuliko kuzingatia utaalamu.

Shirika hilo lilichukua uamuzi huo siku chache baada ya Spika Sitta, kutoa mwongozo na ushauri wa kupinga nia hiyo ya Tanesco iliyopigiwa chapuo na serikali ambapo msimamo wa Tanesco ulitangazwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk Idris Rashid, katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema wameamua kuondoa nia hiyo kwa kuwa mwelekeo wa ununuzi wa mitambo ya Dowans, unalipeleka shirika hilo kwenye ugomvi wa wanasiasa, jukwaa ambalo alidai hawana mamlaka nalo.

Alisema Tanesco itaandika barua serikalini kwa Waziri wa Nishati na Madini, kumfahamisha kuhusu maamuzi hayo, ambayo yalionyesha dhahiri kuchukuliwa kwa shingo upande.

Akifafanua zaidi kuhusu mahitaji halisi ya umeme nchini na mazingira yaliyoifanya Tanesco kutaka kununua mitambo ya Dowans ili izalishe umeme wa dharura, alisema shirika hilo liliwasilisha tathmini ya hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini kwa wakati huo na matarajio ya uzalishaji wa umeme kwa muda wa kati na mrefu na pia mahitaji.

Alisema, Tanesco iliwasilisha taarifa kwamba hali ya ukuaji uchumi inafanya mahitaji ya umeme yaongezeke kwa megawati 75 kila mwaka na kwamba kulingana na tathmini hiyo, hivi sasa nakisi ya mahitaji ikilinganishwa na uzalishaji ni megawati 150.

Mkurugenzi huyo alibainisha ifikapo mwezi Desemba, nakisi hiyo itakuwa ni megawati 225 kwa uchache, ikiwa hapatakuwa na ongezeko lolote la uzalishaji wa umeme.

Alisisitiza pia kuwa shirika lake ilizingatia kuwa, ongezeko la uzalishaji uliotarajiwa kutoka vyanzo vya Kiwira na Tegeta, lisingesaidia kwani vyanzo hivyo visingeingia kwenye mtandao kwa muda uliokuwa umepangwa, kwa sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wa Tanesco.

Dowans ilirithishwa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura mwaka 2006 baada ya kampuni iliyoshinda zabuni hiyo, Richmond Development Company LLC kushindwa kuleta mitambo hiyo na baadaye kukumbwa na kashfa ya ushindi wa zabuni hiyo uliosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake na baadaye kufuatiwa na mawaziri wawili, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.

Jenereta hizo za kufufua umeme ambazo zinatumia gesi asilia zilitangazwa kuuzwa nje ya nchi kwa zaidi ya Sh101 bilioni ingawa bishara hiyo ilishindwa kufanyika baada ya serikali kuiwekea pingamizi mahakamani kampuni hiyo isiuze mitambo hiyo.

MWISHO


Kusema tulishasema
Dhamira zilitutuma
Sasa kauli zakwama
Ndimi zetu zinagoma

Twabaki twaangalia
Machozi yakitujia
Hasira na chuki pia
Vyote twavikumbatia

Midomo inatetema
Vidole vinaachama
Na nyusi zimesimama
Twashindwa hata kuhema

Wapeni hao Dowani
Tunazugana kwanini
Tuwaage kwa amani
Na tuwalipe jamani.

Aliyewaleta nani
Mbona twamuogopani
Atoka sayari gani
Suraye hatuioni

Kama Air Tanzania
Hili nalo naachia
Mengi nimeandikia
Wakuu kuwalilia

Mapesa nikatumia
Na simu kuwapigia
Safari kuwafungia
Huko walikojifichia

Tukaweka hadharani
Yote yale ya Dowani
Sasa mwashangaa nini
Ni kipi hicho kigeni?

Tuwape na nchi yetu
Bila roho yenye kutu,
Tuuze na utu wetu
Tuwape kila cha kwetu

Sitajadili Dowani
Sitauliza nani,
Sijui kafanya nini
Msiulize kwanini?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
International Chamber of Commerce, imetoa hukumu yake katika kesi iliyoletwa na Dowans (T) Ltd kupinga uamuzi wa Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans.. Hukumu hiyo inaonesha kuwa Tanesco imebwagwa vibaya na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu pamoja na gharama ya kesi kwa Dowans..
Mitambo ile waliizuia ili wainunue kwa bei ya kutisha sasa iliposhindikana yaliyofuata yalijulikana.........Tatizo hapa hakuna atakayewajibika.............Hakukuwa na sababu ya Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans waliokuwa na sababu walikuwa ni TRA kwa kutolipwa kodi.....................This country is run by cursed people to put it mildly............
 
Tundapori

Tundapori

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2007
Messages
534
Likes
70
Points
45
Tundapori

Tundapori

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2007
534 70 45
International Chamber of Commerce, imetoa hukumu yake katika kesi iliyoletwa na Dowans (T) Ltd kupinga uamuzi wa Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans.. Hukumu hiyo inaonesha kuwa Tanesco imebwagwa vibaya na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu pamoja na gharama ya kesi kwa Dowans..

More info to come..
Safiiiiiiiii kabisa, vitu vya namna hii ndo vinahitajika bongo iliyo na great leadership.
 
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,379
Likes
2,857
Points
280
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,379 2,857 280
International Chamber of Commerce, imetoa hukumu yake katika kesi iliyoletwa na Dowans (T) Ltd kupinga uamuzi wa Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans.. Hukumu hiyo inaonesha kuwa Tanesco imebwagwa vibaya na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu pamoja na gharama ya kesi kwa Dowans..

More info to come..
I see! Hii nchi imelaaniwa....hivi kweli hakuna kitu tunaweza kuwafanya hawa 'watu' wanaotudhulumu?
 
F

Froida

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2009
Messages
8,216
Likes
1,582
Points
280
F

Froida

JF-Expert Member
Joined May 25, 2009
8,216 1,582 280
Maajabu na huu umaskini tulonao fedha ziende tena kuwalipa majambawaazi usikute hata kwenye kesi tulikuwa hatuwakilishwi
 
Tundapori

Tundapori

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2007
Messages
534
Likes
70
Points
45
Tundapori

Tundapori

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2007
534 70 45
Maajabu na huu umaskini tulonao fedha ziende tena kuwalipa majambawaazi usikute hata kwenye kesi tulikuwa hatuwakilishwi
Nani alikuambia sisi wa-TZ ni maskini?
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,550
Likes
642
Points
280
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,550 642 280
Kwa maamuzi kama haya ndiyo unaona kuwa ZITTO aliona mbali ingawa wengi tulimpinga.

Kwa nchi ya kawaida, Zitto alikuwa anachemsha ila labda mwenzetu alijua hili linakuja.

Sasa mbona TRA hawaji na wao kudai hela na faini kubwa tu?

Pesa za watu lazima zirudi. CCM kweli ni Chama na Tanzania ina wenyewe............... Yanamwisho.
 
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Messages
12,765
Likes
1,031
Points
280
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2009
12,765 1,031 280
International Chamber of Commerce, imetoa hukumu yake katika kesi iliyoletwa na Dowans (T) Ltd kupinga uamuzi wa Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans.. Hukumu hiyo inaonesha kuwa Tanesco imebwagwa vibaya na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu pamoja na gharama ya kesi kwa Dowans..

More info to come..
Kwa nchi kama Tanzania ambao ni hamnazo watalipa. Huu ni uzembe wa rais Mwizi, mosi Dowans mkataba wao na Tanesco uliingiwa kinyemela na sidhani kama serikali walipeleka competent lawyers. Ujinga mtupu bila Wizi wa kura za rais mambo yote haya yangekuwa kama kupiga mswaki. Dowans = RA


Hivi nani alisema sheria za kimataifa ndizo zitakuwa na amri ya mwisho na wala sio sheria za nchi hii? ******! Hivi hawa imbeciles wataisha lini?


 
N

Newvision

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
448
Likes
1
Points
0
N

Newvision

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
448 1 0
My God if this is true we gonna pay over our red noses mpaka na wajukuu
 
Mfamaji

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2007
Messages
6,598
Likes
663
Points
280
Mfamaji

Mfamaji

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2007
6,598 663 280
Kwa maamuzi kama haya ndiyo unaona kuwa ZITTO aliona mbali ingawa wengi tulimpinga.

Kwa nchi ya kawaida, Zitto alikuwa anachemsha ila labda mwenzetu alijua hili linakuja.

Sasa mbona TRA hawaji na wao kudai hela na faini kubwa tu?

Pesa za watu lazima zirudi. CCM kweli ni Chama na Tanzania ina wenyewe............... Yanamwisho.
Inside info kupindisha ukweli alito Zito .alikuwa anajikosha tu baada ya mlungula
 
Zipuwawa

Zipuwawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Messages
3,051
Likes
96
Points
145
Zipuwawa

Zipuwawa

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2010
3,051 96 145
Sijui nani aliyeturoga Watanzania tarehe 9 Dec tunakaribia kuazimisha Nusu karne lakini bado hatujajitambua tu! Mungu ebu tuepushe na hawa viongozi wetu wasioweza kusaidia! wamekuwa watu wa kunenepesha matumbo yao tu!
 
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
2,865
Likes
32
Points
0
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
2,865 32 0
International Chamber of Commerce, imetoa hukumu yake katika kesi iliyoletwa na Dowans (T) Ltd kupinga uamuzi wa Tanesco kuzuia mitambo ya Dowans.. Hukumu hiyo inaonesha kuwa Tanesco imebwagwa vibaya na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu pamoja na gharama ya kesi kwa Dowans..

More info to come..
Definitely, the general public will ultimately pay the price as TANESCO will have no option of recovering such costs other than incorporating them in their tariffs.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,032
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,032 280
And guess what.. mgao unaondelea sasa nani atakuwa "hero"? you guessed it!.... ni kama kumkata ng'ombe nyama huku unamkamua maziwa!!
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
Kwa maamuzi kama haya ndiyo unaona kuwa ZITTO aliona mbali ingawa wengi tulimpinga.

Kwa nchi ya kawaida, Zitto alikuwa anachemsha ila labda mwenzetu alijua hili linakuja.

Sasa mbona TRA hawaji na wao kudai hela na faini kubwa tu?

Pesa za watu lazima zirudi. CCM kweli ni Chama na Tanzania ina wenyewe............... Yanamwisho
Zitto is part of the problem but not the solution.....................Haiwezekani wezi wakatulazimisha kununua vifaa vibovu kwa bei ya waitakayo kwa sababu hakuna ushindani......................sasa hivi hiyo mitambo ingelikuwa imekufa kama ile ya IPTL na SONGAS......................hakuna majibu mepesi hapo..................
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,510
Likes
4,882
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,510 4,882 280
Kwa maamuzi kama haya ndiyo unaona kuwa ZITTO aliona mbali ingawa wengi tulimpinga.

Kwa nchi ya kawaida, Zitto alikuwa anachemsha ila labda mwenzetu alijua hili linakuja.

Sasa mbona TRA hawaji na wao kudai hela na faini kubwa tu?

Pesa za watu lazima zirudi. CCM kweli ni Chama na Tanzania ina wenyewe............... Yanamwisho.
Tuko pamoja kaka!! wengi hawatalikubali hili, lakini fedha zetu ndiyo hizo zinaondoka live! mchana kweupe sijui wa kulaumiwa nani sasa!!! where is mwakyembe?? kuwalaumu vilaza wengi wa JF ni kuwaonea tatizo ni akina Mwakyembe waliotaka popularity, ona sasa

Dowans, aibu hii!!

Inside info kupindisha ukweli alito Zito .alikuwa anajikosha tu baada ya mlungula
Mfa maji! Zitto ana nini tena cha kujitetea katika hili? hukumu hiyo!! na mahakama! kamata adabu yako!! semeni tena wafuata mkumbo!
 
Deodat

Deodat

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2008
Messages
1,279
Likes
52
Points
145
Deodat

Deodat

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2008
1,279 52 145
I see! Hii nchi imelaaniwa....hivi kweli hakuna kitu tunaweza kuwafanya hawa 'watu' wanaotudhulumu?


Ni kuwatandika viboko tu ndio itasaidia!
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,556
Likes
2,368
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,556 2,368 280
Bila shida si nchi yetu ina mapesa ya kumwaga yasiyokuwa na kazi? acha tu tutawalipa na tutaendelea na mkakati wa kubboresha maisha ya kila mtz kwa kazi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi. Hii nchi sijui tunaipeleka wapi huku ndo kujiingiza kichwakichwa kwenye kesi zinazokula kwetu!
 
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Likes
61
Points
145
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 61 145
Kwa maamuzi kama haya ndiyo unaona kuwa ZITTO aliona mbali ingawa wengi tulimpinga.

Kwa nchi ya kawaida, Zitto alikuwa anachemsha ila labda mwenzetu alijua hili linakuja.

Sasa mbona TRA hawaji na wao kudai hela na faini kubwa tu?

Pesa za watu lazima zirudi. CCM kweli ni Chama na Tanzania ina wenyewe............... Yanamwisho.
Mkuu Sikonge,

Tanzania tumezidi kutumbukiza siasa kwenye kila kitu na matokeo yake tutaendelea kuliwa kila mara.

Watu si walisema bora tule majani kuliko kununua hiyo mitambo? Wacha tuendelee kula majani labda huko mbele tutajifunza namna ya kushughulikia migogoro yetu kwa kuondoa siasa.

Inabidi haya mambo yaamuliwe na wataalam wa shirika husika badala ya wanasiasa. Kama hao wataalam wataiingiza nchi kwenye hasara basi wawajibishwe. Mikataba ya kuangalia magazeti yanasema nini, hata siku moja haiwezi kuwa na maana.

Kuna maamuzi mengi sana ya kisiasa ambayo yanakula kwetu. Hivi wale samaki wa Magufuli wametuingizia hasara kiasi gani?
 
Mzuzu

Mzuzu

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2007
Messages
487
Likes
50
Points
45
Mzuzu

Mzuzu

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2007
487 50 45
Hivi kuna nchi ilipata ukombozi wa kweli bila baadhi ya watu kumwaga damu??? Sidhani kama tutakuja badilika jamani........ aaaagh! Kila kitu kwetu ni hasara tu, hakuna wasomi walioelimika wakazuia haya mambo jamani???? Wanasheria, wahandisi wetu, mabingwa wa kila fani kwa nini hii nchi inakuwa imelaaniwa hivi!

Nafikiri tunatakiwa kufanya mabadiliko makubwa katika kila kitu, tunahitaji watu watu kabisa na mawazo mapya kabisa! Inatia uchungu sana kuona nchi inapokwenda na hatuna uwezo wa kuzuia haraka. Hivi hawa wasanii wanavyozunguka nchi za watu kuchekacheka na kunywa chai hawaoni aibuu??

Dah maskini Tanzaniaa!!

Rais yupo busy anafanya birthday......... hayamuhusu haya!
 
D

Deo

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Messages
1,215
Likes
119
Points
160
D

Deo

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2008
1,215 119 160
Hii nji habari ya kusikitisha. Labda walarushwa wanyongwe au hukumu iachiwe wananchi kama ilivyo kwa wezi wa simu kariakoo. Nani ameshitaki wakati Richmond haikuwa na mwenyewe? Kikwete na CCM wanatakiwa watuambie.

Laiti Dr Slaa angeshinda hawa wote wangepigwa pingu na deni halitalipwa!
 

Forum statistics

Threads 1,237,920
Members 475,774
Posts 29,306,272