DOWANS, The End Justify The Means! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DOWANS, The End Justify The Means!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jan 8, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,

  Yafuatayo yalipata kutamkwa na Mh. Harrison Mwakyembe;
  ( Ripoti ya Tume Teule ya Uchunguzi wa Richmond)

  Hakika, hitimisho la ripoti ndefu ya Tume ya Mwakyembe limenifanya niumize kichwa kutaka kujua zaidi mbali ya mambo mengine, juu ya mradi wa Stieglers George ambao kama ungekamilika, ungekuwa na uwezo wa kuzalisha MW 2100 na zaidi. Kiasi hicho cha umeme kingetosha kwa mahitaji yetu ya ndani na hata kupatikana ziada ya kuuza nje.

  [​IMG]

  Pichani ni picha ya juzi tu, maji ya mto Lukosi eneo la Ruaha Mbuyuni, Morogoro. Mto Lukosi unaunganika na mto Kilombero na hata kufika kwenye maporomoko ya Stieglers George yenye kumwaga maji yake kwenye mto Rufiji. Ni kwenye maporomoko hayo ambapo tatizo la umeme Tanzania lingekuwa historia kwa miaka mingi sana.

  Lakini ni kwanini basi viongozi wetu, tena wasomi wazuri tu, wameweza kuhalalisha mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kule Kiwira, Mbeya na kuachana na miradi kama ya umeme wa maji kama huu wa Stieglers George? Wameweza kuhalalisha ujio wa Richmond na baadae Dowans na baadae tufahamu kuwa ni makampuni yenye utata?

  " The end justify the means"- hatma ya jambo huhalalisha njia za kufikia hatma hiyo. Kwa mafisadi, kama hatma ya jambo hilo lina maslahi kwao, basi, hawajali kama njia itakayotumika itakuwa na madhara makubwa kwa walio wengi au la. Haya ndiyo tunayoyaona katika Richmond na Dowans, lakini yapo pia katika mikataba mingine ya kifisadi kama vile IPTL.

  The End Justify The Means, na hilo ni Neno La leo.

  Maggid,
  Iringa
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Wakati wa uchaguzi ulikipigia CCM debe la nguvu huku ukijua ni chama cha mafisadi sasa haya malalamiko na manung'uniko yanatoka wapi?
   
 3. k

  kayumba JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huwezi kuwa Power Master Plan wakati serikali haijawachukulia hatua wote wanaofaidika na hizi DHARURA za umeme!  Hii ya Stiegler George na MW 2100 kila siku uwa najiuliza ni kwanini basi tusielezwe kwanini tusiutekeleze na badala yake tuendele kuangaika na hivi vi-miradi vya MW 100, 60, 200, 300!

  Kwa projection ya wataalam wa nishati, mahitaji ya nishati katika nchi yetu yanakua kwa kasi sana na hivyo hii miradi MW 200, 300, 100 n.k si mipango ya muda mrefu. Kwasababu baada ya miaka 8 bado tutarudi pale pale kwenye vi-miradi vidogo vidogo na watawala watanufaika na 10% zao!


  Ni kwasababu wanaonufaika na miradi hiyo ni viongozi!


  "The end justify the means" - Here the means is not justified by the end!
   
 4. m

  maggid Verified User

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ruta,
  Huo ni mtazamo wako, hata kama sikubaliani nao, nitauheshimu.
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  kwahiyo this is based on the FISADIs Point of View, Fisadi's End.... yaani kuneemeka kwa Mafisadi...

  What About wananchi Point of View? How Can This Be Justified.
   
Loading...