Dowans nyingine inakuja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans nyingine inakuja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jenifa, Dec 27, 2010.

 1. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Tanzania yaingia ubia umeme wa upepo


  [​IMG] Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Power Pool East Africa, Machwa Kagoswe, akitoa maelezo kwa Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu (katikati)kuhusiana na eneo litakalotumika kuzalishia umeme wa upepo mkoani Singida juzi. Serikali imeingia ubia kupitia Shiriaka la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni binafsi ya Power Pool East Aftrica ili kuzalisha umeme huo kuanzia mwakani

  Mpoki Bukuku
  Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), limeingia ubia na Kampuni ya Power Pool East Africa kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida utakaogharimu zaidi ya Sh180 bilioni.
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu, alisema tayari makubaliano yamesainiwa na NDC na kwamba, serikali itakuwa ikimiliki asilimia 51 ya hisa na nyingine zitakuwa za mwekezaji.
  Nyalandu alisema mradi huo utakuwa wa gharama nafuu katika uzalishaji utaingizwa kwenye gridi ya taifa na kwamba, kwa kuanzia zitazalishwa megawati 50 na baadaye zitaongezwa kulingana na uwezo wa wabia hao.
  “Tokea kuanza kufungwa kwa mitambo, itachukua takriban miezi 15 ili umeme uingie gridi na hii itakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme kwa sasa,” alisema Nyalandu.
  Waziri huyo alisema katika makubaliano hayo, serikali itakuwa ikimiliki hisa za asilimia 51, nyingine zitabaki kwa mwekezaji binafsi na ujenzi unatarajia kuanza muda wowote.
  Mkurugenzi wa Viwanda wa NDC, Alley Mwakibolwa, alisema ujenzi wa mitambo ya kutumia upepo kutasaidia kuzalisha umeme mapema, kwani mitambo ya aina hiyo huchukua muda mfupi kuwekwa ikilinganishwa na ile ya maji au gesi.
  ”Tutajitahidi mradi huu uende kwa kasi kubwa, kwani kwa kuanzia tutazalisha megawati 50 na baadaye tutaongeza 50 ili kuingia gridi ya taifa,” alisema Mwakibolwa.
  Mwakibolwa alisema kwa kuingia ubia huo, itasaidia kupunguza gharama kwa taifa, kwani ni rahisi kuliko umeme wa aina nyingine na kuwa shirika hilo litalinda maslahi ya taifa na wananchi.
  ”Tuna maeneo mengine ambayo tunaweza kuzalisha umeme, ikiwamo wa makaa ya mawe na kwa mikoa ya kusini machimbo ya makaa ya mawe tunaweza kuzalisha zaidi ya megawati 1,800 wakati mahitaji ya nchi kwa sasa ni 800,” alisema.
  Alisema nchi itaanza kuuza umeme kwa nchi za jirani hususan za Afrika Mashariki na kwamba, tayari viongozi wa nchi hizo wamekubaliana kuachia Tanzania kuzalisha umeme kwa ajili ya nchi zote tano.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Power Pool East Afrca, Machwa Kagoswe, alisema wameagiza mashine zinazoweza kumudu upepo wa Singida, kwani kwa kawaida nchi za Ulaya zinazalisha umeme wenye kasi ya mita tano kwa sekunde wakati wa Singida hufikia hadi mita 21 kwa sekunde.
  “Huu ni umeme mkubwa ndiyo maana tumeweka oda maalum ya mitambo itakayoweza kuhimili upepo huu, natumaini hii itakuwa njia rahisi ya kuzalisha umeme mwingi kwa gharama nafuu,” alisema.
   
 2. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  nime google jina la mkurugenzi na kukutana na habari hii. umeme na wanasiasa wetu ni kama mbwa na chatu

  Dk. Mwakyembe sasa akiri tuhuma

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]:: Asisitiza hataomba radhi kwa kutoweka wazi mgongano wa maslahi [/FONT]​

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na Mwandishi Wetu [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), amekiri kuwa ni mbia kwenye kampuni inayotaka kuzalisha umeme unaotokana na nguvu za upepo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Dk. Mwakyembe amesisitiza kuwa hataomba radhi kwa uamuzi wake wa kutoweka bayana ushiriki wake kwenye kampuni hiyo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kauli hizo alizitoa alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ambako alikwepa kujibu baadhi ya maswali, akidai tuhuma dhidi yake zinatokana na kuandamwa na mafisadi. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Mwanasiasa huyo anamiliki hisa katika kampuni ya Power Pool East Africa Limited, yenye makao makuu katika majengo ya Posta ya Zamani Dar es Salaam. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Akizungumza kwa jazba, Dk. Mwakyembe, alimshambulia Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, akimhusisha na habari zilizoandikwa na Gazeti la MTANZANIA Jumapili, kuhusu kuwamo kwake kwenye Power Pool East Africa Limited. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Dk. Mwakyembe ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, alipoulizwa sababu za kutotangaza mgongano wa maslahi wakati akiongoza Kamati Teule ya Bunge kuhusu kampuni ya Richmond, aling'aka na kusema asingeweza kutangaza mgongano huo kwa kuwa uzalishaji wa kampuni yake ulikuwa haujaanza. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]"Ningetangaza nini wakati kampuni haijaanza kuzalisha umeme, nitatangaza mangapi?" alihoji na kupigiwa makofi na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, Mbunge yeyote mwenye maslahi na jambo fulani, anapaswa kutangaza mgongano wa maslahi kabla ya kuchangia au kushiriki jambo hilo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Dk. Mwakyembe alidai habari zilizondikwa dhidi yake ni juhudi za kuwakwamisha Watanzania weusi. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]"Mwaka 1932 ilitungwa sheria iliyowazuia watu weusi kupewa mikopo benki, tumepata Uhuru bado sheria hiyo iliendelea. Baadaye ilifutwa, lakini bado iko kwenye vichwa vya watu kwamba mtu mweusi hastahili kupewa mkopo. Ukienda benki utadhani sheria hiyo ipo," alisema. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Dk. Mkwayembe alisema kuwa, ana kampuni nyingi, na si hiyo ya Power Pool East Africa Limited pekee. Mimi siendi kwa Manji (hakusema Manji yupi) kuomba fedha, nina kampuni serious," alisema. Alisema ili umeme uweze kuzalishwa na kampuni hiyo, mtaji wa Sh nusu trilioni unahitajika. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]"Huu ni mradi mkubwa, tutatoa wapi fedha zote hizo? Ndiyo maana sasa mradi huu una watu wengi maarufu, ili tuwatumie hao kupata mikopo benki. Ukianza uzalishaji utatoa megawati 1,800. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]"Hii ni kampuni ya Watanzania masikini, lakini wenye akili, tumepata kiwanja cha kwanza Singida. Walienda wengine kutaka kiwanja hicho wakiwa na helikopta, wakanyimwa. Sisi walienda vijana, wakaomba na kupewa," alisema. Dk. Mwakyembe akisoma azimio namba 11 la Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza Richmond, alipendekeza kutenganisha kazi za siasa na biashara. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Alipoulizwa kama atakuwa tayari kuachia ubunge baada ya mradi wa umeme wa kampuni yake kuanza, alisema; "Ubunge si kazi ya kudumu. Kuna muswada nimeandaa wa kutaka ukomo wa ubunge". Dk. Mwakyembe na wenzake walianzisha kampuni hiyo kabla ya kuwapo Kampuni ya Richmond nchini. Akiwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Richmond, hakuwahi kutangaza hata mara moja mgongano wa kimaslahi aliokuwa nao kwenye suala hilo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Pamoja na Dk. Mwakyembe anayemiliki hisa 1,485 katika kampuni hiyo, wengine wenye hisa ni Emmanuel Kasyanju (99), Victor Mwambalaswa (99), Machwa Kagoswe (4,455), Josephine Pina (99), Athuman Ngwilizi (99), Prosper Tesha (99), TBC (1998) Limited inayowakilishwa na Isaac Mwamanga (297) na MECCO Limited inayowakilishwa na Maungo Kwabhi, hisa moja. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kwa hisa hizo, Dk. Mwakyembe ni mtu wa pili kwa uamuzi katika kampuni hiyo, kwa sababu kwa mujibu wa kanuni za kampuni, nguvu na uwezo wa mtu hutokana na hisa zake. Mwenye hisa nyingi ni Machwa Kagoswe. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Wengine ni Beston Mwakalinga (99), Niels Dahlmann (891) na Lennard Tenende (99). [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Wanahisa wote isipokuwa watatu, anuani zao zinaonyesha kuwa wako nje ya nchi. Mwakalinga anuani yake ni 1591 Bruckner Blud, Marekani; Dahlmann anuani yake ni G.I.A AG, Avenue 1, Brussels, Ubelgiji; ilhali Tenende anuani yake ni 8107 Meadow, Marekani. Wengine ni wa Dar es Salaam na Arusha. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Power Pool East Africa Limited, inafanya kazi kwa kushirikiana na Sixtelecom Limited, ambayo kwenye nyaraka haionyeshi inatoka nchi gani. Kampuni ya Suzlon ya Denmark nayo inahusika na usambazaji vifaa vya mradi huo. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Pamoja na Dk. Mwakyembe, baadhi ya watu wengine maarufu kwenye kampuni ya Power Pool East Africa Limited iliyosajiliwa mwaka 2004 ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa na Machwa Kagoswe ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Tanzania, mali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Kagoswe bado anakumbukwa kutokana na kujihusisha kwake kwa kila hali, kuiuza kampuni ya bahati nasibu kwa raia wa Afrika Kusini, kabla ya kuingiliwa kati na Mwenyekiti wa CCM wa wakati huo, Rais Benjamin Mkapa. Mwambalaswa ni miongoni mwa wabunge waliomshambulia Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dk. Idris Rashid kwa uamuzi wake wa kutaka kununua mitambo ya Dowans. [/FONT]

  [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Mwambalaswa, pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO. Kama ilivyokuwa kwa Dk. Mwakyembe, Mwambalaswa naye hajawahi kutamka hadharani mgongano wa maslahi alionao kwenye tasnia ya umeme.[/FONT]
   
 3. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  ule umeme wa mkapa na yona kule kiwira umeishia wapi. rostam na lowasasa na richmond. baadaye pinda naye aje na umeme wake.
   
 4. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,933
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Acid nimeona post yako iliyo futwa (sjui na nani). Uliuliza kuwa dowans hapo imekujaje?

  Hata mimi binafsi sijaona na kuelewa jinsi dowans ilivyo ingia hapo. Muanzisha mada tafadhali binafsi naomba unijuze jinsi dowans ilivyo ingia HAPO.

  Maana tusiwe tu na mawazo hasi muda wote. Tunaweza tusifike popote.

  Tafadhali kwa ufafanuzi wako mkuu.
   
 5. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Nakumbuka swala la Mwakyembe kumiliki hisa katika kampuni tajwa lilijitokeza baada ya kuwasha moto wa richmond na alitoa ufafanuzi kama huo. Labda wanasheria mtusaidie iwapo sababu ali/nazo zitoa Dr. Mwakembe kisheria ni sahihi au la.

  Lakini kwa upande mwingene sidhani kama mtoa mada analenga kuonesha kuwa hoja ya Richmond/Dowans haikupaswa kuibuliwa na hasa kuvaliwa njunga na Dr. Mwakyembe. Kama kusudio ndo hilo hapo siungi hoja mkono.

  Katika swala la Dr. Mwakyembe na Richmond/Dowans nasimama kusema "ENDs justified the MEANS"
   
 6. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  suluhisho ya maswali yote mlionayo ni kuondoa ccm madarakani. FUll stop.
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sasa umeme wa upepo na Dowans wapi na wapi?
   
 8. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wawekezaji wa umeme wanakaribishwa nchini, katika kufunga mikataba ni vyema capacity charge na tarrif zikaangaliwa kwa umakini mkubwa, haijalishi nani ni mmiliki
   
 9. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,933
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  hilo ndilo neno mkuu. Makapasite chaji ndiyo yanayo tuua walala hoi.
   
 10. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  How much are we paying per day?
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  jamani kama tutakuwa waoga wa kufanya kila kitu basi tutakuwa tayari ni watumwa wa nchi yetu, tuKO HURU KUFANYA CHOCHOTE, yeye kama waziri haimaanishi kuwa asiweze kufanya mambo mengine, ni binadamu pia.
   
 12. Nyodo1

  Nyodo1 Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  If you can't kill them, join them. I choose to join before it's too late! Another five years...
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kapacity tunadungwa mil. 533 kila siku
   
 14. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Jamani hii ni DOWANS nyingine!hizo 51% nani ameridhia kwa upande wa serikali?wananchi tumeshirikishwa?halafu kama si rushwa inakuaje mwakyembe anasema eti watu maarufu wameshirikishwa ili wapewe mkopo benki?jee sisi walalahohi tutapataje mikopo?halafu 50Mw tuu huo si mchezo?tunavimiradi vingi vya umeme lakini vinakula pesa tuu bila umeme wa kukidhi matakwa yetu!mbona mradi wa RUFIJI BASIN 2000MW serikali haujatilia mkazo kwani tutaondokana na mianya hii ya ufisadi?
   
 15. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  watanzania tuogope miradi inayoanzishwa na wanasiasa. walipokuja richmond tulidhani wa maana kumbe wezi. power pool east africa hawajawahi kuwa na mradi wa umeme hata mdogo ghafla projekti ya bilioni 180.

  hii inaweza kuwa sawa na mkapa na kiwira.
   
 16. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Me nlishajisemea TZ sijaona mwanasiasa ambaye yupo ofisin kwajil ya kuniletea maendeleo maana wote wanatumia mamilioni kupata izo nafasi kwaiyo lzm watuibie ili waweze kuyalipa.

  Huyu mwakyembe nae ni wale wale tu hana la maana hapo utasikia capacity charges milioni 300 kwa siku,same goes to sitta anajifanya anapinga ufisadi wakati alikua anakaa jumba wanalipa milioni 12 kila mwezi kma kodi. Me sijaona mtu wa kutuletea maendelea zaidi ya nyerere aliyejifia too bad I was nt arond when he was in power but his philosophy speaks out loud and his legend will lives on
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,805
  Likes Received: 83,184
  Trophy Points: 280

  Hapo ndipo inapokuja Dowans/IPTL nyingine maana (capacity charge na tarrif) zinaweza kuwa ni kubwa sana kuliko nchi yeyote ile duniani na kujiondoa kwenye mkataba si rahisi maana kutaambatana na faini kubwa sana na hivyo kuendelea kuathiri uwezo wa TANESCO katika kuhudumia Watanzania wachache wanaotumia nishati ya umeme

   
Loading...