DOWANS: Ni mechi ya Mafisadi Stars vs Wapambanaji United | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DOWANS: Ni mechi ya Mafisadi Stars vs Wapambanaji United

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Jan 17, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mechi hii ya fainali ya mpira wa miguu kati ya Mafisadi Stars (pro-Dowans) na Wapambanaji United (anti-Dowans) inachezwa mbele ya umati mkubwa sana wa Watanzania wapatao milioni 40.7.

  Timu hizi zinagombea kombe lenye thamani ya zaidi ya $65 million (takriban shilingi bilioni 100). Malipo haya yatafanywa kutumia pesa za walipa kodi wa Tanzania.

  Wapambanaji United wamesema wakishinda kombe pesa zitaenda kujenga hospitali, kusomesha watoto shule, kusambaza maji na kujenga barabara kwa manufaa ya taifa.

  Mafisadi United wamesisitiza kuwa ushindi kwao ni lazima na pesa hizo watazitumia kujiandaa kutwaa Urais wa Tanzania mwaka 2015 ili kuendeleza maslahi yao binafsi.

  Wafuatao ni wachezaji wa timu hizi mbili:

  MAFISADI STARS

  1. Jakaya Kikwete
  2. Mizengo Pinda
  3. Frederick Werema
  4. William Ngeleja
  5. Mathias Chikawe
  6. Edward Lowassa
  7. Andrew Chenge
  8. Mark Bomani
  9. Anne Makinda
  10. Zitto Kabwe
  11. Rostam Aziz

  Bench

  1. Nimrod Mkono
  2. Nazir Karamagi
  3. Kingunge Ngombale-Mwiru
  4. Sophia Simba
  5. Emmanuel Nchimbi
  6. Dr. Mohamed Gharib Bilal
  7. Fisadi Media (Mtanzania/Rai, Tanzania Daima, Daily News, Jambo Leo)

  KOCHA MCHEZAJI: Rostam Aziz


  ***********


  WAPAMBANAJI UNITED


  1. Samuel Sitta
  2. Dr. Harisson Mwakyembe
  3. NGOs (LHRC, TAMWA, TGNP, etc)
  4. David Kafulila
  5. TUCTA na vyama vingine vya wafanyakazi
  6. Donors (World Bank, IMF, US, Netherlands, GBS group)
  7. Wasomi (UDSM, UDOM, IFM, CBE, Mzumbe, Tumaini, SAUT, etc)
  8. Wafanyakazi wa kada ya chini wa TANESCO
  9. Tundu Lissu
  10. Dr. Willibrod Slaa
  11. Umma wa Tanzania


  Bench

  1. Bernard Membe
  2. Frederick Sumaye
  3. John Samuel Malecela
  4. Abdulrahman Kinana
  5. Cleopa Msuya
  6. John Pombe Magufuli
  7. Media huru (MwanaHalisi, Mwananchi, THISDAY/KULIKONI, Raia Mwema)

  KOCHA MCHEZAJI: Samuel Sitta

  *********

  REFA WA MECHI: Jakaya Kikwete


  • Refa wa hii mechi (Jakaya Kikwete), ndiye mlinda mlango wa Mafisadi Stars na pia ni kocha mchezaji wa timu hiyo. Matokeo ya hii mechi yatakuaje? Ngoja tusubiri dakika 90 pamoja na dakika za majeruhi kupata matokeo kamili.

  • Beki nambari 4 wa Wapambanaji United (David Kafulila) kafundishwa mpira na mshambuliaji hatari namba 10 wa Mafisadi United (Zitto Kabwe). Je, atauza timu au atakuwa shujaa? Majibu tutapata mwisho wa mechi.

  • Timu ya Mafisadi Stars imejaa vigogo hatari wa ufisadi ambao wana uzoefu mkubwa wa ushindi. Wapambanaji United haina vigogo wengi, lakini inaungwa mkono na umati mkubwa wa Watanzania. Nani ataibuka kidedea?
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Vigezo vya uteuzi wa timu hizi ni nini?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwenye Bench ya wapambanaji, huyo mchezaji no 4 simkubali kabisa!...mimi najua huyu ndiye mtetezi mkuu wa maslahi ya timu ya mafisadi, ukiachilia yeye mwenyewe kuwa mporaji mkuu wa rasilimali za taifa, hasa kwenye eneo la maliasili.
   
Loading...