Dowans, mauaji Arusha - ni kipi kipo mahakamani na hakipaswi kuongelewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans, mauaji Arusha - ni kipi kipo mahakamani na hakipaswi kuongelewa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magobe T, Feb 13, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Ndugu wanaJF, kuna mambo yanayotokea hapa Tz na wakati mwingine nashindwa kuelewa kwa nini inakuwa vile. Mfano, hoja ya Dowans imeachwa kujadiliwa bungeni kwa madai kuwa ni suala ambalo bado liko mahakamani.

  Lakini mauaji ya raia Arusha yalitolewa kauli na Waziri Mkuu Mizengo Pinda huku akikishtumu Chadema kwa kuwa chanzo cha mauaji hayo wakati kesi bado iko mahakamani. Je, Waziri Mkuu kutoa "hukumu" nani alaumiwe kuhusu vurugu hizo wakati kesi iko mahakamani siyo kuingilia uhuru wa mahakama? Kwa nini inakuwa rahisi kuongelea vurugu zilizotokea Arusha ambapo kesi bado iko mahakamani na wakati Dowans inaonekana kama taboo wakati kesi pia bado iko mahakamani? Ni kitu gani kimejificha hapa?
   
Loading...