Dowans hawakulipa kodi muda wote walipolipwa na Tanesco - Ubovu wa mikataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans hawakulipa kodi muda wote walipolipwa na Tanesco - Ubovu wa mikataba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 25, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  KAMATI ya Nishati na Madini imedai kupitiwa mikataba yote iliyoingiwa na serikali na kampuni zinazozalisha nishati ya gesi baada ya kubaini kuwapo kwa mapungufu makubwa kwenye mkataba mmoja ambao umeelezwa kumpa nguvu muuzaji kuuza nishati hiyo kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) kwa bei ya dola za Kimarekani badala ya shilingi za Kitanzania.

  Kwa hali hiyo, imeelezwa kuwa TANESCO imekuwa ikipata hasara na kushindwa kujiendesha; huuza umeme kwa bei ya shilingi za Kitanzania lakini huuziwa gharama kubwa ya dola za Kimarekani.
  Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, ndiye aliyeonekana kuishawishi kamati hiyo kupitia mikataba yote iliyoingiwa na serikali kwa sababu ya kile alichokieleza kuwa "haiwezekani gesi iwe yetu halafu kampuni iliyopewa zabuni kuisafirisha kutoka Songosongo iuze gesi hiyo kwa TANESCO kwa bei ya dola za Kimarekani."

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam mara baada ya kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (CCM), kufanya ziara ya kutembelea mitambo mbalimbali ya kuzalisha umeme, Meneja Mkuu wa kitengo cha Theo Generation kinachosimamia uzalishaji wa umeme gesi, Gregory Chegele, alisema yote hayo yanatokana na mikataba iliyoingiwa na serikali.
  Alisema Kampuni ya Pan Afrika ndiyo iliyopata zabuni ya kuuza gesi hivyo gharama za uendeshaji inategemea bei ya gesi ilivyo katika soko la dunia.

  "Aliyepata hiyo tenda hana uwezo wa kuzalisha megawatts 120 bali umeme unaokwenda katika gridi ya taifa kutokana na gesi ni megawats 80 pekee," alisema.

  Alisema kuna kipindi uzalishaji ulipungua baada ya kutokea tatizo katika kisima cha Songosongo hali iliyoathiri utendaji.
  Chegele alisema kuwa pamoja na mabadiliko ya bei bado tatizo la utengenezaji wa vipuri na mafuta ya uendeshaji wa mitambo vinachangia katika kuathiri uzalishaji wa umeme huo.

  "Unajua sisi tunaponunua gesi kutoka kwa Pan Afrika tunauziwa kwa bei ya dola tena inategemea bei ilivyo kwa wakati huo katika soko la dunia…lakini tunapozalisha umeme tunauza kwa shilingi," alisema. Hatua hiyo iliwafanya baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kuhoji maswali mbalimbali huku Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akisisitiza kuwa kamati hiyo inahitaji kupata taarifa zaidi pamoja na kukutana na wahusika hao. Alisema wakati wa majadiliano hayo ni bora kamati ikajiridhisha kwa kupitia mkataba huo maana haiwezekani gesi iwe ya kwetu halafu kampuni hiyo iuze gesi hiyo kwa bei ya dola. "Mwenyekiti naomba kama hiyo kesho tunakutana na kuzungumzia masuala haya ni bora tukakutana na wadau wote na pia tukaletewa mkataba huo kwa kuwa hauna siri ili tuuone ukoje," alisema. Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Makamba alisema kutokana na taarifa hiyo ni vyema kamati ikaangalia na kujadili kwa kina kuhusu jambo hilo maana hatua hiyo imeashiria kuna "katatizo" mahali.

  Kauli ya Makamba kuliita suala hilo kuwa ni "katatizo" ilipingwa vikali na mjumbe Sendeka, ambaye alimjibu akisema, "Hapa sio katatizo mwenyekiti, hapa inaonekana wazi kuna tatizo kubwa katika mkataba huo, hivyo ni lazima kamati yetu ilijadili hili kesho."
  Wakati huo huo kamati hiyo ilikagua mtambo wa kuzalisha umeme wa kampuni ya Dowans na kukutana na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Stanley Munai ambapo alisema mitambo hiyo imekuwa ikiwashwa kwa muda wote lakini haipeleki umeme katika gridi ya taifa. "Kila kitu kimeunganishwa; hakijazimwa kitu chochote lakini kila baada ya wiki mbili tunawasha mashine hizo ili zisiharibike," alisema.

  Alisema ni neno baya kuita mitambo hiyo ni chakavu maana hakuna mashine iliyo mbovu kwani zote zina uwezo wa kufanyakazi kwa muda wa miaka 50. "Mashine hizo zililetwa hapa zikiwa hazijatumika na hata ile kubwa inayozalisha megawats 40 ilifika hapa ikiwa katika namba sifuri, haijawahi kutumika mahali popote," alisema. Makamba alihoji sababu za mitambo hiyo kuendelea kuwepo wakati imesimamisha uzalishaji kwa kipindi kirefu. Akijibu hoja hiyo, Munai alisema walitegemea kuondoa mitambo hiyo mwaka 2008 lakini kutokana na kuwa na kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court) iliwaweka katika wakati mgumu kuondoa mitambo hiyo. Alisema taratibu za uwekezaji wa kampuni hiyo uliipa kodi ya kawaida kama kampuni nyingine ndiyo maana Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) haikuendelea kudai fedha kwa Dowans. "Taratibu za uwekezaji tunatakiwa kufanya kazi kwa miaka mitatu au minne bila kulipa kodi hivyo hatujavunja sheria ya aina yoyote katika suala hilo; tumekuwa tukitimiza wajibu wetu kulipa mapato kama wengine," alisema.

  Alisema mmiliki wa mitambo hiyo Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi alifika nchini ili kusikiliza kilio cha Watanzania ndiyo maana akafikia hatua ya kuiandikia TANESCO barua ili kuweza kukaa katika meza ya majadiliano. Alisema iwapo TANESCO watakataa kujibu barua hiyo basi kampuni hiyo itaacha suala hilo lifanyike mahakamani kama walivyoamua kusajili tozo ya hukumu hiyo.
  "Unajua mmiliki hatataka wajadiliane kuhusu kutumika kwa umeme wa kipindi cha nyuma kama miezi 10 ambapo wananchi walitumia umeme uliozalishwa na dowans pasipo kulipwa," alisema. Alisema walizalisha umeme na kudai kiasi cha dola milioni 24 ambazo serikali haijalipa hadi sasa. Munai alisema benki pekee inayoidai kampuni ya Dowans ni ya Baclays ambayo inaidai kampuni hiyo kiasi cha dola milioni mbili. "Tuliwahi kukopa huko nyuma benki ya Stanbic ambapo mawakili wa Rex Attorney ndiyo waliotusimamia na tukaweza kupata mkopo lakini kama unavyojua mfanyabiashara anaangalia riba tulipoona Barclays wana riba ya chini tukaamua kuchukua mkopo huko," alisema.

  Alisema mmiliki huyo alifika nchini kutokana na yeye kuwa anamiliki hisa nyingi katika kampuni hiyo kuliko wengine.
  Munai alisema ikiwa serikali itahitaji kuuziwa mitambo hiyo kampuni hiyo haitakuwa na pingamizi iwapo itakataa itauza mitambo hiyo kwa watu wengine wanaohitaji. Alisema hadi sasa fedha inayohitajika kulipwa kwa kampuni hiyo si bilioni 94 kama wengine wanavyofikiri bali kiwango hicho kilianza kupanda tangu Juni 15 mwaka jana.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Jaribu kuweka basi in paragraphs kurahisisha usomaji. Mimi sijahangaika kuisoma kwa sababu hiyo. Pia weka chanzo cha habari.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nimeshaiparagrafusisha tayari ili kurahisisha wasomaji kupata mtiririko mzuri. Ujuavyo si wote tulio na ujuzi wa editing, ila tu mahiri wa kukosoa haririsho za wengi.:rain:
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mbona chanzo cha habari ameweka?
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Yani hii ishu ya dowans!hivi Tz hakuna mwenye final decision?taifisha hii mitambo halafu kamata wamiliki na wale waliowakaribisha.kila siku upuuz huu mpaka lini?
   
Loading...