Dowans? Dowans ipi - Watanzania tumegeuzwa mataahira !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Wana JF tujikumbushe kidogo.

IPC Acquisition of Dowans Power Plant in Tanzania

IPC today announces that its Cyprus based affiliate, IPC Independent Power Corporation (Cyprus) Limited has entered into an agreement to acquire the Dowans Power Plant in Tanzania with an installed capacity of 112 MW.

IPC is one of the United Kingdom's leading developers and operators of power plants. Since it was founded fifteen years ago by Colin Moynihan, British Energy Secretary under Margaret Thatcher and John Major, and Peter Earl, an investment banker, IPC has developed, owned or operated more than 4,000 MW of thermal and hydro plant. It has operated power capacity for British Petroleum and the Ras al Khaimah Investment Authority. IPC has spun off two regional power companies serving Latin America and South Africa both of which are quoted on the London Stock Exchange. Rurelec PLC is the largest British power company in Latin America with some 700 MW of installed capacity. IPSA Group PLC owns and operates South Africa's first gas fired power plant which is also the countrys first combined cycle plant.

IPC today has operating contracts in Argentina, Bolivia and the United Arab Emirates and is developing some 1,500 MW of new gas fired capacity in Bangladesh, Indonesia, Moldova and the United Kingdom.


For further information, please contact:

Independent Power Corporation PLC
Peter Earl, Managing Director Tel: 020 7793 5610
Ana Ribeiro,Tim Weigh, Blythe Weigh Tel: 020 7138 3206
 
Mkuu tunashukuru sana taarifa hii labda niulize hivi namba hizi za simu ni za nchi gani Cyprus au UK?
Mi naona kilichobaki ni kuwapigia tu simu tujue ukweli uko wapi!
 
Kichwa cha mwenda wazimu ni watz ukiondoa viongozi wa juu akiwemo kikwete wanaoneemeka kwa kusaini mikataba hewa na kuleta kwa nguvu wawekezaji feki.
 
Ngoja nigoogle hii number hawa wasituchezee akili zetu. Ngeleja wewe una akili akili yako ya kupima naomba kukuuliza?
 
Sinema ya Dowans bado inaendelea lakini sasa haina sterling baada ya Ngeleja, Werema na Al Adawi kukataa kutoa kauli zozote za kueleweka kuhusu kampuni hii ya kitapeli.

Yule January Makamba naye kasema kwamba sasa wasemaji wakubwa wa utata wa Dowans watakuwa ni TANESCO ambao wataalamu wao waliipa ushauri Serikali kabla ya kuingia mkataba na Dowans kwamba Dowans haina uzoefu wowote katika ufuaji wa umeme hivyo msiingie mkataba nao.
 
Sinema ya Dowans bado inaendelea lakini sasa haina sterling baada ya Ngeleja, Werema na Al Adawi kukataa kutoa kauli zozote za kueleweka kuhusu kampuni hii ya kitapeli. Yule January Makamba naye kasema kwamba sasa wasemaji wakubwa wa utata wa Dowans watakuwa ni TANESCO ambao wataalamu wao waliipa ushauri Serikali kabla ya kuingia mkataba na Dowans kwamba Dowans haina uzoefu wowote katika ufuaji wa umeme hivyo msiingie mkataba nao.
Mkuu Bubu Ataka Kusema hebu shuhudia madudu haya:
Kikwete -Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. Baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi. Aidha, imesisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba wataoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa. Vile vile, watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika

Hii ina maana kuwa baada ya tu ya kikao cha Baraza la Mawaziri chini ya Raisi Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 15/2/2011 mambo mawili yakafanyika. Kikwete huyoo bila aibu akasepa Mauritania kuzima moto kwa jirani huku kwake kwateketea akipishana na tapeli Ret. Brigadier General Sulaiman Yahaya Al Adawi aliyetua nchini bila hodi, hofu wala woga eti kudai alichoita halali yake ! Kumbe
watoa huduma kutoka kampuni inayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika iliyopendekezwa na baraza la Kikwete ni Dowans !
Sasa shuhudieni maajabu mengine haya:
Kikwete - Ukweli siwajui wenye Dowans na wala kampuni hiyo siijui...siwahitaji na wao hawanihitaji

Huyo ndiye Kikwete anayeweza kutamka bila aibu kuwa haijui kampuni inayodaiwa iliirithi Richmond na kuingia mkataba na Tanesco, kampuni inayoendeshwa na mshikaji wake mkuu Rostam na kampuni inayotishia kukamata mali za serikali anayoiendesha ! Hvi tuna hakika gani kuwa hiyo mitambo iliyopo Ubungo bado ni ya Dowans kama imeweza kufanya shughuli zake nchini bila Raisi wetu kuwa na habari ? Sasa huyoo tena kasepa Ufaransa huku mkataba na Dowans ikisainiwa !
 
wanaweza vipi kuuza mitambo kwani deni la milioni 75 la Dowans kwa mabenki yetu limeshalipwa? si iliwekwa rehani ama? Mimi nimewaambia subirini tu wakishalipwa watakapoumbuliwa watu isije kuwa ugomvi
 
wanaweza vipi kuuza mitambo kwani deni la milioni 75 la Dowans kwa mabenki yetu limeshalipwa? si iliwekwa rehani ama? Mimi nimewaambia subirini tu wakishalipwa watakapoumbuliwa watu isije kuwa ugomvi

Pamoja na hayo Mwanakijiji lakini rejea hii taarifa ya tarehe 30/8/2010.
Richmond/Dowans which has since been sold to Independent Power Corporation (IPC a Cyprus-based firm), was, however identified initially as an emergency plant. Presently IPC is negotiating a draft PPA with TANESCO, with the oversight of EWURA !
Hivi hatuna hata mzalendo moja huko EWURA wa kufafanua hili ? Hii habari ilitolewa miezi mitano baada ya kuwa IPC imenunua mitambo ya Dowans !
 
Duuu! Wakuu Utata unaolazimishwa na hii Serikali ya JK ni wazi kabisa hawataki kuwajibishana. Uongozi wa JK ni wa mashaka mashaka sana. Hivi huwa anafikiri kweli? Ni lazima wawajibishwe kinguvu. This is when PUSH comes to SHOVE!
 
Back
Top Bottom