Namsililiza hapa huyu aliyekuwa Mjumbe wa bunge la katiba na mwenyekiti wa UPDP Fahami Dovutwa katika kipindi cha hotmix cha EATV
licha ya kuwa mtangazaji hana uelewa mzuri wa katiba lakini maswali yote anayoulizwa mzee wetu Dovutwa hajibu sanasana tu na yeye anamuuliza maswali tena mtangazaji
na jibu lake kubwa kwenye karibia kila swali anajibu"Tumeondoa ubaguzi alioupandikiza warioba na tume yake"
lakini kilichonishangaza zaidi ni mzee wetu kuulizwa swali na mtangazaji kuwa "kama wabunge wote wakichaguliwa hawana elimu na katiba pendekezwa inataka mbunge awe waziri na waziri lazima awe na degree itakuwaje" mzee wangu dovutwa akaishia kusema embu mtafute Mama mery amesoma sana kuliko tume yote ya warioba anaweza kukujibu....
mimi nimeshindwa kumuelewa huyu mzee anamatatizo gani ya Akili???
hivi kweli huyu ndiye aliyegombea urais 2010 ..!! Na kuna wananchi wakampigia kura....??
Mwisho wa mjadala akasema atakayetaka kugombea urais kwenye "Genge"lake la UPDP atakuwa ADUI wake wa kudumu kwakua anamzuia yeye kwenda ikulu
kwakweli kama bunge letu "Tukufu"la katiba lilishesheni vihiyo kama hawa Tusitegemee chochote cha maana kutoka kwenye katiba iliyopendekezwa...
Hili suala la Elimu ni muhimu sana aiseee yaani wakipita wote elimu ya kujua na kusoma tu cjui mawaziri watatoka wapi? Au itafikA sehemu mawaziri wa kubadiri nafasi za mawaziri wanaojiuzuru hawatakwepo.
Duh aisee pia nimesikia huyu mzee hiv punde, kwa kifupi dovutwa anapelekeshwa na njaa tu km umemsikia anadai pia chama chao kipewe ruzuku, halafu ajajibu hoja alizoulizwa, japo mtangazaji pia yuko sharo maana alipaswa kumbana aweze kujibu ni aidha kakimbia swali au hajui kabisa kinachoendelea.
Mimi mambo 4 ambayo yananifanya nipigie kura ya hapana ni haya
1. vipindi vya mbunge kukaa madarakani kutokuwa na kikomo
2. kitendo cha wabunge wa zanzibar kuja kutunga katiba inayohusu mambo ya tanganyika
3. viongozi kuweka pesa nje ya nchi
4. elimu ya mbunge nalo ni balaa
kuturaghai kwamba haki za kila kundi zimewekwa halina maana,
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.