Dovutwa: Kikwete jiuzulu urais

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
MWENYEKITI wa Chama cha United Peoples' Democratic (UPDP), Fahmi Dovutwa, ametoa kauli yenye ukakasi kwa Rais Jakaya Kikwete, akimshauri ajiuzulu urais. Dovutwa alisema, Rais Kikwete hana sababu za kuendelea kubaki tena madarakani, kwa madai kuwa ameshindwa kumaliza tatizo la rushwa nchini.

"Mh. Kikwete wewe ni rais wa nchi, unavyolia rushwa imejaa ndani ya CCM, wakati wewe ndiye mwenyekiti wa chama hicho tawala, unashangaza watu," alisema.

Dovutwa ambaye aliwahi kugombea urais mwaka 2010, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na Mtanzania, kuhusu uchaguzi wa CCM kutawaliwa na rushwa.

Mwanasiasa huyo ambaye alimuunga mkono Rais Kikwete katika uchaguzi huo, alisema amelazimika kusitisha ‘uswahiba' na Rais Kikwete, kwa madai kuwa amepoteza sifa.

Dovutwa alisema, hivi karibuni Rais Kikwete aliwashangaza Watanzania wengi, pale alipoibuka na kulalamika kukithiri kwa rushwa ndani ya chama chake.
 
Devutwa naye ni sehemu ya hilo tatizo, kwa nini alikubali kuunga mkono rushwa mwaka 2010?
 
Wanasiasa uchwara kama hawa wanastahili kutafuta leseni ya uganga wa kienyeji ingawa sidhani kama vile vile atauweza .Alipomuunga Jk mkono alidhani anamkomoa nani?

-Alijua EPA ndiyo iliyomuingiza JK ikulu 2005 halafu bado akamuunga mkono 2010.Tapeli la kisiasa na mnafiki aliyekubuhu
 
Huyu si ndio alikuwa mgombea urais ambaye hata mama yake mzazi hakumpa kura yake. Sasa hata mama mzazi hakuungi mkono katika siasa zako kuna kitu hapo zaidi ya kutapatapa na kuganga njaa. Nadhani anamkumbusha kikwete kwamba bado hajampa kamgao kake kwa kumuunga mkono 2010.
 
Jina tu linaleta maana ya kuvutwa hivyo aache kabisa kusema kitu kwakuwa ni yeye alikuwa na kihelehele cha kumuunga mkono baba lizwani
 
KIZABAZABINA huyu, amekosha SHAVU la JK Ubunge wa kuteuliwa sasa ameamua atoke hivyo "kum-tarai" (read to try) JK
 
Raisi wangu Dovutwa, angepata uraisi leo Tanzania tungekuwa na kiwanda cha silaha na leo hii ningekuwa namiliki ka berreta
 
kila kitu now kiko hovyo tu,afu na sie watanzania tunazidi kushangaa?serikali inafilisika, wanainchi pesa haishikiki,mafuta hayapatikani,2015 bado ccm watatawala....

kweli tutakoma
 
Huyu vile vijisenti alivyopew na JK vimekwisha sasa anatingisha mti tena dodo zishuke, huyu hana tofauti na Mtikila.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom