Chris Lukosi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 4,581
- 2,937
Ndugu Zanguni
Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.
Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.
Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?
Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.