DOUBLE STANDARDS ZA CHADEMA, Lwakatare angekuwa kiongozi wa CCM wangeandamana kushinikiza ajiuzuru

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,000
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.
 
FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,083
1,225
Correction: wangeandamana kudai sheria ichukuwe mkondo wake. And that's exactly what's happening - kesi iko mahakmani.

Na wewe ukiwa kama ex-cop you should know better, "everyone is innocent until proven otherwise". So, put that in pipe and smoke it!
 
JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
0
Mkuu umefata ushauri wa Dr. Lakini au Ndo Njaa Haina mwenyewe? Big time ila soma hapa.

SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu kufichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare, baadhi ya wahusika wameanza kuvurugana.

Kwa mujibu wa Lissu, njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA.

Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare.

Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.

Jana gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.

Vile vile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu' huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana kuhusu kuvuja kwa siri zao.

Saumu akiwa katika grosari maarufu kwa jina la Kwa Kimaro jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.

"Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda," alitamba.

Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling'aka: "Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?"

Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake' aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA.

"Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?" alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.

Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana.

Katika madai yake, Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.

"Awali walipewa 400,000, wakapewa tena 300,000, pia wakapewa 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa," alisema Lissu.

Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.

Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kama anahusika nazo kwa namna yoyote.

CHANZO:TANZANIA DAIMA

MY TAKE:
HUU NI MWANZO TU WA KUUMBUKA!
 
Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,000
Correction: wangeandamana kudai sheria ichukuwe mkondo wake. And that's exactly what's happening - kesi iko mahakmani.

Na wewe ukiwa kama ex-cop you should know better, "everyone is innocent until proven otherwise". So, put that in pipe and smoke it!
Mimi nadhani kama kweli mna wataalam wenu na nyinyi mngefanya uchunguzi kuliko kumtetea wakati nyie wenyewe hamjui ukweli ukoje
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,764
2,000
duh you should grow-up and be a man enough unachusha sasa kama wali wa chuya,unachojipendekeza upitishwa 2015 kugombea ubunge lakini kwa posti zako hapa JF hata MACCM menzio wameshaanza kuona ni bongolala,maandamano ya chadema siku zote yamekuwa na theme ya kutetea haki za wananchi
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,500
Kama hayo ndio mawazo yako, afadhari ulitoka CDM......swala la lwakatale ni mchezo wa CCM, utumia akili kidogo tu, huitaji kuwa na degree kujua hilo

Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,995
2,000
Daaaa @ Dr paurine njoo huku utoe ushauri!

Haya twambie ni lini ccm walishaamua kujiuzulu tena kwenye mambo yaliyo wazi? Yani kwenye swala kama hili mlitegemea chadema wakurupuke na kumvua mtu nyazifa?
 
Mzawa Halisi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
635
500
Chris Lukosi
Umeshindwa kuona tofauti ya madai ya uwajibikaji yanayotolewa na Chadema dhidi ya viongozi wa Serikali na hili unalolitaka wewe?

Lwakatare anaweza vipi kutatiza uchunguzi akibaki kwenye nafasi yake chamani?

Kumbuka Chadema pia wana madai mazito dhidi ya serikali na CCM kwenye jambo hili.
 
Last edited by a moderator:

kisimani

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
550
170
Pitia hii kwanza ndio uone jinsi chadema ilivyo makini......

Wakuu JF

Jana akitoa briefing ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA mbele ya wanahabari (nakala ya kilichozungumzwa iko hapa JF), Mkurugenzi wa Katiba na Sheria wa CHADEMA, Tundu Lissu aliweka wazi moja ya masuala ambayo watu wengi wamekuwa wakihoji, wakiwemo waandishi wa habari, kwa nini CHADEMA inasimama na Lwakatare!

Lissu alisema, azimio la kikao cha Kamati Kuu na hivyo msimamo wa CHADEMA ni kwamba chama kitasimama na kumtetea Lwakatare kwa gharama zote, ikiwemo kumwekea utetezi wa kisheria kwa sababu kesi hiyo ya ugaidi ni kesi ya uongo, kesi ya kutungwa na watawala (CCM) kutafuta namna ya kuondokana na 'headaches' za CHADEMA.

Alisema wazi kuwa CHADEMA isipoweza kumtetea Lwakatare, haitaweza kumtetea mtu mwingine yeyote yule dhidi ya tuhuma za namna hii, ambazo zimeandaliwa na zinaandaliwa nyingi. Kamati Kuu iliona kufanya hivyo ni kujitumbukiza kwenye mtego wa CCM ambao wangependa kuona hilo linatimia.

Kesho watamtengenezea tuhuma na kumshtaki Naibu Katibu Mkuu, kesho watamuundia tuhuma Katibu Mkuu, keshokutwa wataunga unga maneno kumtungia mashtaka Mwenyekiti wa chama, leo itakuwa kwa mkurugenzi, kesho huyu keshokutwa yule. Mtawatosa wote. Ndivyo wanavyotaka. Kisha wataenda hatua nyingine wanayokusudia katika adhima iliyoshindwa mapema, ya kuimaliza CHADEMA, tumaini jipya la watu.

Kwa mujibu wa Lissu, Kamati Kuu ilifikia uamuzi huo baada ya kupewa taarifa ya kina juu ya makando kando mengi kuhusu suala la Lwakatare kubambikiwa kesi ya ugaidi.

Ni makando kando hayo yaliyowasilishwa mbele ya Kamati Kuu kwa ushahidi wa kina, yanakiweka na kuonesha wazi namna CCM ilivyo katikati ya mchezo mzima, kwa asilimia karibu zote kupika tuhuma na kisha kesi hiyo kwa kusudio la kutaka kuonesha kuwa viongozi wa CHADEMA na hatimaye chama hicho kinajihusisha na masuala ya ugaidi na mipango ya mauaji ya raia. Lengo; bambika tuhuma, label CHADEMA, tafuta visingizio vya msajili kufuta CHADEMA, kosanisha na wanahabari.

Kwa mujibu wa Lissu, unawezaje kumtosa Lwakatare katika kesi ambayo involvement ya CCM na watu wengine fulani fulani katika kutengeneza suala hilo ni kubwa kwa kiwango kisichotiliwa shaka kuwa mchezo huu umetengenezwa! Unawezaje kumtosa kamanda wako katika suala ambalo CCM na watawala, kupitia vyombo vya dola, wanakesha wakipanga mipango ya ku-fubricate (that is criminal) ushahidi kumhusisha Lwakatare, viongozi wengine na chama katika matukio ya kutunga?

Lissu alihoji juu ya mawasiliano makubwa hadi ya kutumiana pesa kati ya mtu aitwaye Mwigulu Nchemba na Ludovick Lwezaura, hadi kutumiana fedha kwa njia ya Mpesa, siku chache tu baada ya video hiyo kutengenezwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba kuwa ameitangazia dunia kupitia Star tv kuwa anao mkanda/CD inayoonesha viongozi wa CHADEMA wakipanga njama za mauaji. Je, Mwiguku alikuwa na biashara gani na mtuhumiwa wa ugaidi, Ludovick?

Hiyo ni mbali na yale mawasiliano yaliyofanyika kati ya Ludovick na Mwigulu siku ile ile ambayo video inaonekana ilichukuliwa. Wana uhusiano gani, Kiongozi mwandamizi wa CCM na mtuhumiwa wa ugaidi!

Mwanasheria msomi Lissu, mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare, alisema kumekuwepo na mawasiliano ya kiwango cha juu kati ya mtu aitwaye Ludovick Joseph Lwezaura na Dennis Msaki. Alihoji iweje Msaki awasiliane mara nyingi zaidi na mtu anayetuhumiwa kutakiwa kumlisha Lissu au kumteka, kuliko hata alivyoweza kuwasiliana na mke wake!

Kwa mujibu wa Lissu, Kamati Kuu pia ilipokea taarifa namna watu wanaodaiwa kuwa ni watumishi wa vyombo vya dola, wanamtumia mtu aliyewahi kufanya kazi Makao Makuu ya CHADEMA (kabla hajafukuzwa mwanzoni mwa mwaka jana kwa tuhuma za ukosefu wa uadilifu), kwanza kuwarubuni watumishi wa idara fulani waibe nyaraka za CHADEMA kwa ahadi ya fedha nyingi.

Pili, kuwarubuni watumishi wa CHADEMA Makao Makuu wanaohusika na ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake, wakubali kuandika maelezo ambayo yatatumika kama ushahidi dhidi ya Lwakatare, viongozi wengine na chama kwa ujumla, mahalamani.

Walinzi hao wa CHADEMA wameshaitwa katika vikao mara tatu sasa, mojawapo ya maeneo ya makutano ikiwa ni Sea Cliff Hotel na Jakees. Wanafundishwa namna ya kuandika maelezo, huku wakiambiwa wawe tayari kushikiliwa kwa muda polisi, lakini baadae wataishi maisha mazuri (huko waliko) kwa kupewa pesa na familia zao zitawezeshwa kwa muda wote. Yote ni katika kutengeneza ushahidi. Lissu alisisitiza kuwa kutengeneza ushahidi ni kosa kisheria. Ni kosa hata liwe limefanywa na nani!

Pia wameombwa wawe tayari kutoa maelezo ya uongo kwenye vyombo vya habari, ili kukichafua chama, kukipaka matope meusi ya kuwa ni chama cha kigaidi kinahusika kupanga njama za mauaji. Yote hii ni mwendelezo wa siasa chafu za maji ya mtaroni. Gutter politics. Ambazo, kwa mujibu wa Lissu mbele ya wanahabari, zilianza na kuita CHADEMA 'chama cha familia ya Mtei na Mbowe, chama cha Wachaga, chama kikabila, chama cha Kaskazini, chama cha Wakristo, chama cha Wakatoliki...aah aah chama cha Wakatoliki' yote hayo yameshindikana. Sasa ni zamu ya 'chama cha ugaidi, chama cha mauaji'.

Makando kando ni mengi. Kila jambo na wakati wake. Ni muhimu kuwa na akiba ya maneno. Lissu alisema yako mengi yatasemwa wakati mwafaka ukifika.

Lissu alimalizia kwa kuwapatia mfano waandishi wa habari, namna ambavyo TANU ilikuwa tayari kumlinda kwa gharama yoyote Mwalimu Nyerere pale wakoloni wa Kiingereza walipombambikia tuhuma na kumfungulia kesi ya uchochezi na wenzake wawili, wanahabari wenzetu Robert Makange na Rashid Bagidele. Ilikuwa mwaka 1958.

TANU iliweka mawakili watatu, kutoka Uingereza, mwingine Kenya na mmoja akiwa Mtanzania. Kumtetea 'mcochezi' Nyerere, ambaye wakoloni walitaka kumpeleka gerezani, kwa kuonesha kuwa ni kiongozi mchochezi, na hivyo TANU kilikuwa chama cha wachochezi, wanaochonganisha wananchi na serikali, wanaotaka wananchi waichukie serikali yao, hivyo ni chama kisichofaa. Kifutwe. Ilishindikana kwa sababu TANU, na Watanzania walisimama na kiongozi wao, wakiamini hakufanya hivyo.

Lissu alitumia mifano kadhaa.

Upo pia mfano mwingine wa Nelson Mandela. Huyu makaburu walisema ni gaidi. Wakamkamata na kumweka gerezani. Kumbukumbu zinaonesha, CIA wamemwondoa Mandela katika orodha yao ya magaidi duniani, mwaka 2007 hivi.

Hivyo ANC walipaswa kumtosa Mandela baada ya kutungiwa tuhuma na kubambikiwa kesi na makaburu, ambao walikuwa wanaona dawa pekee ya kuzuia mapambano ya kumkomboa mnyonge Afrika Kusini kwa kuuondoa utawala dhalimu wa makaburu (hapa kwetu ni CCM, maana kaburu si rangi) ni kudhibiti na kufungia/ kufuta ANC kwa kuanza na viongozi wake?

Hivyo Kamati Kuu ya CHADEMA, ambayo ni chombo cha juu cha maamuzi ya chama, ikaweka azimio la kuwatetea makamanda wake wanaobambikiwa tuhuma za uongo, ambapo lengo kuu la 'wabambikaji' ni kutafuta sababu ya kutesa/kukatisha tamaa wanachama na viongozi (kuweka mahabusu au gerezani) kukichafua chama na hatimaye kutafuta sababu ya kukifuta.

Lissu alimalizia kwa kusema "wanapambana na wazo ambalo muda wake umeshafika. Halizuiliki. Hawataweza. Tutawashinda"

Makene

0752 691569/0688 595831​
 
Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,000
Daaaa @ Dr paurine njoo huku utoe ushauri!

Haya twambie ni lini ccm walishaamua kujiuzulu tena kwenye mambo yaliyo wazi? Yani kwenye swala kama hili mlitegemea chadema wakurupuke na kumvua mtu nyazifa?
Mh Lowassa, Mzee Mwinyi, Mh Mrema...
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
2,000
Dr. Slaa ameruhusu barua ya Zitto uvuje kwa makusudi.

Kama kuna mtu anayetakiwa kuwajibika kwa kujiuzuru ni Dr. Slaa kwa kushindwa kutunza siri za ofisi yake.
 
Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,072
1,195
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.

Hawa jamaa hawakubali ukweli hivyo subiri matusi na kejeli!
 
mugayasida

JF-Expert Member
Nov 3, 2012
480

Nadhani kama CCM wakisema wenye njaa kama wewe wagawe ukameruni nadhani wewe ungeshakuwa mwenza wa Nape kwa ukaribu saana..Hivi hii njaa yako wewe ni ya aina gani?Inazidi njaa ya Tambwe Hiza eeh.Unanitafutia ban sio?
 
Chris Lukosi

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,581
2,000
Chris Lukosi
Umeshindwa kuona tofauti ya madai ya uwajibikaji yanayotolewa na Chadema dhidi ya viongozi wa Serikali na hili unalolitaka wewe?

Lwakatare anaweza vipi kutatiza uchunguzi akibaki kwenye nafasi yake chamani?

Kumbuka Chadema pia wana madai mazito dhidi ya serikali na CCM kwenye jambo hili.
Na kesho ukija gundua kuwa ni Lwakatare mwenyewe anataka kuihujumu chadema utasemaje?
Never say Never, anything is possible.
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,521
2,000
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.
mramba na chenge walikua na kesi mahakamani za kujibu,lakini cha ajabu mkiti wa ccm taifa wakati wa kampeni za ubunge 2010 alikua akiwanadi ili wapate kura.Tunajua Kesho utaiweka video ya mh.mbowe na slaa ili wanachadema waandamane.ume bugi meeeeni!
 
punainen-red

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
1,732
0
Hivi mtu aliye ndani anazuiaje uchunguzi kufanyika??? Binafsi simuamini Lwakatare, lkn hiki ulichoweka hapa hakileti maana... Hivi Lowassa amewahi kusema alijiuzuli ili iweje vile?? Baada ya kujiuzuli mliwaadhibu wahusika au mlifunikafunika mambo yakaisha?
 
KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,829
1,195
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.

lukosi unatumia msuli mkubwa sana kushupalia na kufananisha vitu ambavyo is by far.kwa wakati huu jaribu kuwa unawasiliana na wakuu wako msije mkapishana kauli huko mbele.
Ni vyema pia ukatumia muda mwingi kujibu yale ambayo yameelekezwa kwako binafsi.
Nikukumbushe pia ndoto zako za kuwa mbunge zitaendelea kuwa ndoto ilihali bado ungali macho.
 
Froida

JF-Expert Member
May 25, 2009
8,764
2,000
Dr. Slaa ameruhusu barua ya Zitto uvuje kwa makusudi.

Kama kuna mtu anayetakiwa kuwajibika kwa kujiuzuru ni Dr. Slaa kwa kushindwa kutunza siri za ofisi yake.

Wewe ndio umevujisha na unakuja kutaka kumpaka matope hapa,hujifahamu unahitaji tiba make post zako zote za kumhusudu Dr Slaa,Mbowe, na kumsupport Juliana Mtela na Mchange huwa tunazireje bro uzuri JF Mods hawafichi kitu ,Huyo Zitto kwa historia ya JF aliwahi kukili kuwa kigagula kwahiyo mapepo yanamsumbua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom