Double Nationalities

lidoda

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
641
573
DOUBLE NATIONALITIES
Serikali imekataza kuwa na uraia zaidi ya uraia mmoja. Yaani kama wewe ni mtanzania huruhusiwi kuwa na uraia zaidi ya Utanzania. Inasemekana Balali alikuwa na uraia mwingine yaani wa Kimarekani licha ya kuwa Mtanzania. Kama ni hivyo kweli kwa nini Tanzania iliruhusu Marehemu kushika wadhifa mkubwa kama huo?
 

Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
26
DOUBLE NATIONALITIES
Serikali imekataza kuwa na uraia zaidi ya uraia mmoja. Yaani kama wewe ni mtanzania huruhusiwi kuwa na uraia zaidi ya Utanzania. Inasemekana Balali alikuwa na uraia mwingine yaani wa Kimarekani licha ya kuwa Mtanzania. Kama ni hivyo kweli kwa nini Tanzania iliruhusu Marehemu kushika wadhifa mkubwa kama huo?

Inasemekana kuwa wapo wengine pia na wana nyadhifa kubwa tu serikalini...ndio TZ hiyo

Note: Inasemekana is the operative word here... msianze kunidai ushahidi!
 

mjinga

JF-Expert Member
May 11, 2008
328
129
Kama ni hivyo mbona huu ni moja ya ufisadi na ni criminal case! nna ndugu yangu hakujua na kaukana U Tanzania kwa sababu ya kutafuta maisha. na sasa hivi anataka kuurudia U Tanzania ambao ni mbinde. Hawa wahindi wana Uraia zaidi ya mbili kama Balali wao
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
24,085
20,702
Balali alivuliwa visa yake na Marekani mara baada ya kutimuliwa na JK.
Sasa huo uraia sijui aliupata lini na kwa kutumia jina gani!
Hapo ndio kwenye maswali!
 

Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
26
Wahindi ndio usiseme...akina Vithlani and co. mambo ya u-dual citizenship wanayaendeleza bila hofu na wala vyombo husika haviwabughudhi... Ballali naye inawezekana hivyohivyo.
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,890
1,003
Ni Kweli Kama Kuna Wanaoongoza Kwa Kuwa Na Uraia Wa Nchi Mbili Ni Hawa Watu Wanaitwa Watanzania Wa Asia Na Sio Wahindi Kama Mnavyojaribu Kuwaita. Unajua Ukiwaita Hivyo Wanasema Eti Huo Ubaguzi. Cjui Ni Ubaguzi Kweli Maana Kama Ni Ubaguzi Mbona Hawawaambii Hao Watanzania Wa Asia Ambao Ndiyo Wabaguzi Wakubwa?
 

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
5,431
6,468
Hii hoja ni yakitoto na yauongo. Balozi wa Marekani Tanzania alishasema balali si raia wa Marekani na aliomba viza kuja huku. Pili Uraia wa nchi mbili ni Jambo zuri na Watu Watanzania wengi walio nje wanatuma pesa nyingi kuliko pesa zote za kodi serikali inazopata kwa mwaka hivyo watu wa nje wanachangia kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi wa nchi. 2007 West Union Watanzania walituma $450 Million, kuna ubayagani kuwapa hawa Watanzania? Ukweli ni kwamba wanaopinga ni washamba tu
 

Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
26
Kamundu,

Hivi unahabari kuwa kuna Watanzania wenye uraia wa US lakini wakienda huko wanachukua viza ubalozini pale Drive-in, wanatumia passport zao za TZ, tena wana nyadhifa za kueleweka serikalini? Pale ubalozini kama hujajiandikisha kama raia wao watajuaje?

Hiyo point yako ya pili kutetea dual citizenship unaweza kuitoa bila kuwakejeli wanaoipinga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom