Double edged sword: Haki na wajibu wa mtanzania

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Hebu wanasheria wa nchi hii mtusaidie ktk kupambanua sheria na haki za mtanzania kama inavyoainishwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano!
Kwa kuwa Mimi sio mwanasheria naogopa kuongelea sana tafsiri ya mambo nisiyo na ujuzi nayo. Lakini kuna changamoto ambazo naona zinafaa kujadiliwa kwa mapana ili kutunza heshima yetu, kutenda haki na kutimiza wajibu!
Watanzania lazima watambue haki ndio msingi Mkuu wa kila kitu ktk mustakabali wa maendeleo ya taifa letu!
Part III ya katiba ya 77 inaainisha haki za msingi za raia! Kwa mtazamo kwa sasa naona kama haki hizi wengi hawazipati kwa usahihi, na hofu yangu ni kuwa tukianza kuhisi hatutendewi haki, then ile will ya watu inapotea na watawala na raia hawatokuwa kitu kimoja hivyo kushindwa kujenga taifa!
Natizama baadhi ya acts na vipengele vyake ambavyo nahisi havitendwi kama inayostahili (naweza kuwa siko sahihi ndio maana naomba wanasheria wanisadie/watusaidie):
 1. Equality of human being act of 1984 sect. 12(1-2)
  1. All human being are born free and are all equal
  2. Every person is entitled to recognition and respect for his dignity
 2. Equity before law Act No.13 of 1984 & Act no. 4 of 1992
  1. Sect.13(6)(e) No person shall be subjected to torture or inhuman or degrading punishment or treatment
 3. Right to Privacy and Personal Security Act No.16 of 1984
  1. Sect.16(1)Every person is entitled to respect and protection of his person, the privacy of his family and of his matrimonial life, and respect and protection of his residence and private communication.
Kuna exceptions ktk kila sheria iliyowekwa hapo. Kwa upeo wangu nadhani huo sasa ndio uñakuwa wajibu kwa kila mtu ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na kwa yeyote anayeenda kinyume na maelekezo au sheria za nchi, bado katiba hii inalinda jinsi atakavyokuwa treated! Sehemu kubwa inamrejesha mikononi mwa mahakama ili akahukumiwe kwa haki na huku heshima yake ikiwa imelindwa.
Tuna tatizo ktk hili, wote wananchi na serikali (watawala).
 1. Nadhani haki ya usawa wa kiutu na usawa mbele ya sheria 12 & 13 kwa kiasi kikubwa hazifuatwi.
  • Mifano:
  • Kuna viashiria vingi vya kukosa usawa miongoni mwa raia hasa linapokuja suala la kuwa na double standards. Tunapozungumzia kashfa kwa viongozi au lugha za uchochezi au matusi. Kuna baadhi ya watu wanalindwa kupita kiasi na wengine hawalindwi kabisa. Yupo mwanasiasa wametangazwa kila ubaya bila ya uthibitisho wowote, ametukashfiwa kuwa alijisadia hadharani (iwe kweli au uongo) bado alikuwa na haki ya kulindiwa heshima yake kama inavyoainishwa ktk katiba, lkn hilo halikutendeka na bado halindwi to date! Wapo wanasiasa waliotoa lugha za kebehi zenye kudhalilisha wenzao ktk majukwaa lkn hawakuhojiwa Ila wapo ambao lugha zao za staha zinaitwa uchochezi.
  • Wapo watanzania wengi sasa wanapata inhuman or degrading treatment.
   • Hili ni jambo baya kuliko yote linalotokea kwa sasa nchini. Watu hawalindiwi heshima zao hasa wale wanaofanya kazi na serikali. Mfanyakazi akikosa basi atatangazwa aibu zake nchi nzima, na hata alifukuzwa kwa uzembe dunia itajua instantly. Wapo wanaoitwa majina mabaya fis..di, vil..za etc! Wamekosea au hawajakosea act no. 16 inavunjwa na walinzi wa nchi! Privacy and Personal Security unajua kuna sehemu camera haiingii mahakamani ili kufanya yanayoendelea kubaki kuwa na heshima zake unless kwa learned brothers or yeyote mwenye soecial interest na hiyo case!
   • Ni hivi tupo watu na heshima zetu, tunaweza kukosea kazini kwa uzembe, wizi au bahati mbaya! Tuna wajibika na endapo taratibu zikifuatwa kuna penalty inaweza kutolewa ikiwemo kufukuzwa kazi, kupelekwa mahakamani na kufungwa au kupewa adhabu nyingine yeyote kama sheria na taratibu za taasisi husika zinavyojieleza.
   • Ukinisema barabarani na kunifukuza huku ukianika kila kitu ktk TV, unawaumiza wengi wakati mwingine! Kuna wenye watoto ambao labda wapo shule, kila mtu ata speak bad kuhusu familia na kesi nyingine ni just rumours na bado tunaambiwa kuwa uchunguzi haujakamilika!
   • Enzi za Mwalimu kulikuwa na neno "kusimamisha/au kustaafishwa kwa manufaa ya umma" watawala wetu na wengine please tumieni neno hili muwalindie watu heshima zao.
Shida kama hizi pia wananchi tunazo! Hata hapa JF watu wanasikia rumours tu juu ya mtu X na haraka anawahi kuandika. Hata kama zikiwa na ukweli, bado unaweza ukawa na walakini unapomvunjia mtu heshima yake bila ya kujali. Matumizi ya social media yamekuwa ni ya hatari sana na yanaweza kusababisha hasara kubwa kwa jamii. Matusi ya Instagram na magomvi mengine ni lazima sasa yazuiwe! Yes tunalia kuwa sheria ya mtandao ni Kali sana, lkn nadhani matumizi yetu bado ni mabaya kupita kiasi!
Mtu ambaye umepata rumours zake unaweza kumuanika kwa ishara na wala sio kwa majina kama Ms. X aiba chuxxp! Ungeweza kusema mrembo kigogo wa taasisi X aiba chuxxp! Ni mfano tu, lengo ni kujua kwamba kumvunjia mtu heshima ni kosa kisheria na mbaya zaidi hilo jambo likiwa ni la uongo!
Nawaasa viongozi wa awamu ya tano, jaribuni kulinda heshima na utu wa watanzania! Wafanyakazi wa umma wapo ktk tension kubwa sana sasa, watawasusia nchi, hasa wale wa juu kama ilivyokuwa miaka 15-20 nyuma wakawa wanakimbilia South, Namibia na Botswana! Tutabaki na least elite people makazini!
Lakini uzalendo utazidi kupungua kwa kadri watu wanapohisi hawapo salama sana, why bother maana uncertainty ni nyingi mno!
 
Back
Top Bottom