Dotto Bulendu: Tathmini yangu juu ya mahojiano kati ya BBC na Rais Samia Suluhu

Acheni kumpunguza salim uweledi wake ktk tasnia Ya Habari,ktk nchi za kiafrika ambazo ni dhambi kuwa mkweli na muwazi kwa kiongozi lazima mwandishi anaetaka kufanya mahojiano na mkuu wa nchi awasilishe maswali yake na yapimwe kwenye kujibika na kuangaliwa majibu yake yatakuwa na matokeo gani yakijibiwa na mkuu huyo..??.unaeza kuta salim alishaelekezwa njia Ya kupita.. Kwa hiyo tusilaumu sana, kikubwa amepata fursa na imesaidia kuelewa sasa Madame president amesimamia wapi kwenye sakata la FAM na yanayoendelea kwa sasa nchini..
 
Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Dotto Bulendu (MwanaPuge).Nikiandika kutoka kijijini Puge.
@@@@@@
Mimi mwenyewe was so disappointed na Salim Kikeke, nimemuona kama mmojawapo wa wasaka tonge na umaarufu kwa Mh. Rais Samia, aidha kwa kukusudia ama kwa kadiri ya uwezo wake. Yaani hajaonesha seriousness yeyote na Mh. Rais alikuwa very relaxed. Yaani hajachemshwa bongo yeyote. Muandishi ameenda tu kupiga selfie ila bado arudi shule akajifunze akina Amanpour wanafanyaje ....
 
Ikulu mawasiliano haina mtu/mshauri wa Rais aliyesomea sheria?

Kabla ya mahojiano Kikeke alipaswa achambuliwe script za kumhoji Rais na kisha Rais apewe mwongozo wa baadhi ya maswali kujibu kisheria kama taasisi.

Hali iliyokuwepo,wandani wabobevu wa kauli ya Rais wangeipitia hiyo news wangemwomba BBC asiirushe kwanza.
Kauli ya Mh. Rais imekiuka utaratibu wa kimahakama kwa sehemu kubwa sana ...
 
Kwanini hamtaki kukubali kwamba interview ilikuwa nzuri na Rais kajibu kwa weledi wa hali ya juu? Huu uchambuzi ni nadharia tu za darasani kama anafundisha. Lakini uhalisia Kikeke kauliza maswali professionally. Kesi ya ugaidi ya Mbowe ni rejea ya sheria kwa maana ya kesi. Tozo ya miamala ni sheria. Au alitaka ataje kifungu a, b, c? 😀😀😀
 
Tathmini yangu ya juu ya mahojiano kati ya BBC Na Rais Samia Suluhu Hassan.
Haya uliyoainisha wewe ni ya kwako siyo ya BBC, kwani kila muulizaji ana malengo yake. Una ushahidi gani kwamba 'alipaswa kusema hivyo ulivyoframe wewe masuali?'

Dunia hii sote tumekuwa washauri wa Raisi, wanahabari, watoa huduma za udaktari.... alimradi imekuwa shida tu. Sijui tumsikilize nani sasa.
 
Salimu kikeke ana uwezo mdogo sana. Hii ya kujificha nyuma ya mahojiano kufanyika ikulu haina maaana. Ikisikiliza vizuri utagundua mama alikuwa akijibu anavyotaka na hakukua na maswali fikirishi na yakuibua majibu lengwa.

Ni makosa makubwa Sana mwanzo mwisho wa interview hakuna lejea. Nafikiri hii ilikuwa press conference iliyoandaliwa na ikulu. Tafadhali Sana BBC mnaharibu bland yenu. Huyu jamaa anachemka interview karibu zote. Zuhura anajitahidi na nafikiri anaijui na kuimudu kazi yake.
Wewe mwenye uwezo mkubwa hebu nenda ukafanye hizo interviews tukuone.
Domo jumba maneno!!!!!!!!! (yaani mdomo ni nyumba ya maneno mtu anaweza kusema lolote)
 
Usikute siroccm alimtisha kabla kuwa endapo anaulizia juu ya Polisiccm kuwafanyia upekuzi haramu wa kishetani wapinzani pindi waendapo kuwakamata kwa Amri za mwenyekiti wa CCM lazima angebambikiwa kesi ya kufanya fujo ikulu
 
Wewe mwenye uwezo mkubwa hebu nenda ukafanye hizo interviews tukuone.
Domo jumba maneno!!!!!!!!! (yaani mdomo ni nyumba ya maneno mtu anaweza kusema lolote)
Aende kivipi? Yeye kachambua kasoro za interview kwa nia njema kuelimisha umma juu ya mapungufu yote
 
Aende kivipi? Yeye kachambua kasoro za interview kwa nia njema kuelimisha umma juu ya mapungufu yote
Kuchambua vya watu ni rahisi kuliko kukifanya kitu chenyewe. Ndiyo maana kuna msemo ukiona vyaelea vimeundwa.
 
Kwanini hamtaki kukubali kwamba interview ilikuwa nzuri na Rais kajibu kwa weledi wa hali ya juu? Huu uchambuzi ni nadharia tu za darasani kama anafundisha. Lakini uhalisia Kikeke kauliza maswali professionally. Kesi ya ugaidi ya Mbowe ni rejea ya sheria kwa maana ya kesi. Tozo ya miamala ni sheria. Au alitaka ataje kifungu a, b, c? 😀😀😀
Lini wapinzani walihukumiwa kwa kesi za kigaidi? na lini wapinzani waliandamana wakachoma matairi barabarani?
 
Kuchambua vya watu ni rahisi kuliko kukifanya kitu chenyewe. Ndiyo maana kuna msemo ukiona vyaelea vimeundwa.
Vya jana havielei na havijaundwa kabsa ebu tuambie ni lini uhuru wa vyombo vya habari umepatikana Gazeti la Tanzania Daima lipo wapi?
 
Salum kikeke siku ukipata nafasi ya kumhoji IGP ukumbuke kumhoji juu ya Tabia mbovu ya kwenda kuwapekua wapinzani majumbani mwao kwa njia haramu za kishetani, mpinzani akidai katiba mpya anaenda kupekuliwa saa nane usiku kisha kubambikiwa kesi ya ugaidi na pia umkumbushe yale ya kupimwa mkojo kipindi kile
 
..binafsi nadhani Salim Kikeke amefanya vizuri kuuliza maswali ambayo ni " general " bila kumbana Rais SSH na vifungu vya sheria na ushahidi wa aina mbalimbali.

..Salim angefanya kama alivyoshauri Bulendo kungeweza kutokea shutuma kwamba amemkosea heshima Rais, amemtukana, au alikuwa na ajenda binafsi.

..Ile interview ilikuwa ni nafasi ya Rais SSH kuonyesha uwezo wake kwa hadhira ya wasikilizaji wa BBC na wengine. Majibu yake hakupaswa kuyaelekeza kwa Salim Kikeke, bali alitakiwa aelekeze majibu huku mtaani na duniani anakosikilizwa.

..Kwa hiyo, pamoja na kwamba Salim Kikeke hakuuliza maswali huku akirejea vifungu vya sheria, na katiba, Rais SSH alikuwa na wajibu wa kujibu huku akirejea na kusisitiza vifungu vya katiba na sheria ili kukazia ktk majibu yake.

..Maoni yangu ni kwamba tusitumie udhaifu wa maswali ya Salim Kikeke kuhalalisha makosa ya wazi kabisa, na mapungufu, katika majibu ya Rais SSH.

cc Chige, Pascal Mayalla, tindo, Nguruvi3, Erythrocyte
 
Back
Top Bottom