Dotto Bulendu: Soka limekabidhiwa wanasiasa na wasanii ndio tutarajie ushindi dhidi ya Uganda? Wanasoka wetu wastaafu hawapo? Hawathaminiwi?

Kule Ulaya na mataifa mengine ambayo yameendelea kisoka,inapotokea kunahitajika hamasa kubwa ya kujenga morali kwa wachezaji na mashabiki basi wale wachezaji Nguli wastaafu hutumika sana kuhamasisha morali ya ushindi.

Hii hutumiwa sana na Vilabu vikubwa duniani ama timu za taifa ambapo wakongwe(Legendaries) huwekwa jukwaani sehemu maalum kabisa ikiaminika kuwa wale waliopo uwanjani wakitazama jukwaani na kuwaona wakongwe morali inapanda na hata kwenye kujenga hamasa wachezaji waliocheza kwa mafanikio hutumika sana.

Sasa nakaribu kutazama mbinu inayotumiwa na kamati maalum ya kuhamasisha ushindi wa timu ya Taifa hapo keshokutwa.

Kwenye mkutano wao na waandishi wa
habari,mbali na kuwajumuisha waandishi wa michezo,lakini naona inawatumia zaidi waigizaji maarufu nchini akina Wema,Shilole,Steve Nyerere n.k na kuwaweka kando wanasoka waliocheza kwa mafanikio miaka ya nyuma.

Kwa nini kamati inaacha kuwatumia wanasoka waliowika miaka ya nyuma inakimbilia kuwatumia waigizaji?kwa nini tusiandae vipande vya vidio vya wanasoka waliowika huko nyuma wakiwahamasisha vijana wetu na wanasoka hawa siku ya jumapili wakatengewa eneo maalum pale Jukwaani?

Kwa nini tumewatenga wanasoka walio hai ambao waliipekea Tanzania katika fainali za mataifa huru Afrika mwaka 1980 kama
sehemu ya hamasa kwa wachezaji na Watanzania?

Kwa nini tusiwarekodi na hata kwenda nao kwenye "Press Conference" wachezaji wakongwe waliocheza fainali hizi na wakasema neno la hamasa kwa watanzania na hata tukawaambia watanzania wajae uwanjani waungane na wakongwe pekee waliofuzu fainali hizi kutoka Tanzania na badala yake tunawatumia akina Wema pekee?

Nafahamu akina Wema wanamashabiki nyuma,lakini katika hili la Jumapili hebu tunatumie zaidi wachezaji wetu waliocheza kwa mafanikio wakati wao.

Mbali na akina Tenga waliokuwemo kwenye kikosi cha Stars kilichofuzu fainali hizi pekee,kwa nini pia tusiwatumie wanasoka waliocheza kwa mafanikio kwenye Vilabu na hata kufika ngazi ya juu?

Waliokuwemo kwenye Kikosi cha Simba kilichocheza Fainali za kombe la Shirikilo la Soka Afrika mwaka 1991 na walicheza timu ya taifa wengi wao wapo,kwa nini tusiwatumie hawa kama sehemu ya hamasa?

Walioifikisha Yanga hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza mwaka 1998 bado wapo kwa nini tusiwatumie kama sehemu ya hamasa na badala yake tunawatumia zaidi waigizaji na waimba muziki?

Tunapowatumia waigizaji na waimba Muziki kuhamaisha ushindi wa Stars,tusiwaache wachezaji nguli wa zamani akina Leodigar Tenga,Sunday Manara,Abdalah Kibaden,Juma Pondamali,Adolf Richard,Zamoyoni Mogella,Mohamed Mwameja,Ken Mkapa ,Peter Tino
mfumgaji wa bao la
Star lililoipeleka Tanzania kwenye fainali za
mataifa huru na wengine wengi katika kuhamasisha wachezaji,kuhamasisha mashabiki ili jumapili tupate ushindi.
#nizamuyetu
Wenzako wanawaza pato la mlangoni..
 
Alafu game inachezwa Jpili hamasa mpaka sasa hata daladala moja iliyoweka bendera kama sehemu ya kuhasisha, yote kwa yote kila la kheri stars japo ntashindwa kwenda
Labda kama ukiweka Bendera ukajaze mafuta bohari ya serikali pia Trafiki P. wakuache ata ukivunja shera japo kidogo..
 
Ulete waenda uchi uwanjani,mimi msuva cjawahi kuyaona haya uwanjani maana kule kwa waarabu hakunaga,macho na akili yangu...!mnapaswa kuniombea xna ili viwe kwenye kuscore2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti wema sepeto nae anahamasisha?? mtu ambaye hajui lolote kuhusu mpira.
Sio yeye tu, wengi hawana influence kwenye mambo ya kijamii, na ndio maana huoni hata wakipata endorsements za matangazo kwenye kampuni kubwa za ndani. Umaarufu wao umejengwa kwenye mambo ya kipuuzi na si kazi za sanaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom