Dotto Bulendu: Rais, walioelemewa na mizigo ni wengi na siyo wale tu waliokuwa CCM na kwenda upinzani. Mizigo haipo kwenye siasa pekee

Kwani wewe ulitaka bei ya sukari ya 2005 iwe mpaka leo? hauoni juhudi ya serikali ya kujenga kiwanda kikubwa cha sukari huko Morogoro? Vipi kuhusu wachina wanaokwenda kujenga kiwanda kikubwa Africa mashariki na kati cha cement huko Tanga? Watanzania tuwe wavumilivu hiki ni kipindi cha mpito tu.
 
Jana wakati akitangaza majina ya wateuliwa kuwania nafasi za ubunge kupitia CCM kwa ajili ya uchaguzi mdogo,

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli alisema chama kitaendelea kuwapokea wanasiasa wote wanaotaka kurejea CCM na kuwaahidi pumziko lenye furaha.

Mh Rais alisema wale wote wenye mizigo huko walipo wahamie CCM ili waishushe mizigo waliyonayo na akasema wengi waliondoka CCM kutokana na figisu walizokutana nazo lakini wamekutana na figisu zaidi.

Sasa Mh Mwenyekiti na Rais wa chama,na sisi ambao hatupo kwenye siasa na hasa si wabunge na madiwani,mizigo yetu tukaitue wapi?maana

1.Huku mtaani tunaelekewa na mzigo wa kupaa kwa bei ya simenti,bei ya sukari ilivyopanda haijawahi kushuka,bei ya mafuta ya taa,Petrol na diseli nayo haikamatiki siki hizi,huu mzigo umetuelemea tukautue kwa nani Mh Rais?

2.Watumishi wa umma wameelemewa na mzigo wa kutokupandishwa madaraja(baadhi),miaka mitatu sasa hakuna nyongeza ya mshahara Mh Rais,huu ni mzigo umeaelemea watumishi wa Umma,wakautue wapi Mh Rais?usipoutua mzigo huu Mh Rais kuna hatari ya "Go slow strike".

3.Sekta binafsi zimeelemewa,sasa hivi wafanyakazi kwenye sekta binafsi wanahenya na maisha ya bila mishahara,waliowekeza huko wanalia mazingira ya biashara kiujumla hayawapi faida baadhi wanapunguza tu wafanyakazi,huu nao ni mzigo,kama ulivyo nukuu kitabu kitakatibu (Biblia),kwamba wote wenye mizigo iliyo waelemea waje kwako,wenye hii mizigo nao waje?

4.Mh Rais,vijana waliomaliza masomo yao vyuoni,shuleni ma vyuo vikuu kuanzia mwaka 2015 ulipotangaza oparesheni saka watumishi hewa na wasio na vyeti,asilimia kubwa hawajaajiriwa mpaka leo,wapo mtaani hawajui hatma yao,wameelemewa na mzigo wa ukosefu wa ajira na ukali wa maisha,Mh Rais watoto wako hawa unawasaidije kuutua huu mzigo,na jana ulisema wote walioelemewa na mzigo waje kwako Mh Rais,hawa nao waje?

5.Mh Rais yalifanyika mabadiliko ya kisheria ya mifuko ya jamii kwa kuzuia wastaafu kulipwa mafao yao mpaka watakapofikisha umri uliopotishwa,Mh Rais kuna kundi la watu wapo kwenye umri wa kati na wameamua kuacha kazi ili wakafanye mambo mengine,sasa wanapoambiwa wasubiri
mpala wafikishe umri uliopotishwa kisheria wamebaki njia panda,mzigo sasa umewaelemea hawajui pa kuutua,sijui tunawasaidiaje?

6.Mh Rais familia na ndugu wa Azory Gwanda,Ben Saanane wamelia sana kuwasaka ndugu zao,wanaelewa na mzigo wa mawazo walipo wapendwa wao,Mh Rais kama ulivyosema wote walioelemewa na mizigo waje kwako,kwa kutumia vyombo vyako,wasaidie familia hizi kuutua mzigo unaowaelea,hakuna mzigo mzito kama mzigo wa mawazo Mh.

7.Mh Rais,kule vijijini katazo la kusafirisha mazao nje,liliporomosha bei ya mazao,Maeneo mengi wanavijiji wamejikuta wamekaa na mazao ndani kwani soko la ndani limetengeneza hasara kubwa kwao,hawa nao wameelemewa na mzigo huu Mh Rais.

8.Mh Rais nadhani umesikia jana kuwa Ligi kuu msimu huu haitakuwa na mdhamini mkuu,na nimeona kuna mdhamini eti atadhamini kwa kuvipa vilabu shilingi milioni 15 kila kimoja,Mh Rais sekta binafsi iliyokuwa imewekeza huku waliowengi wanalia na faida kiduchu,wanadai mazingira ya biashara yamebadilika sana,sasa hata kwenye michezo taasisi za michezo zimeelemewa na mzigo,kuna kila dalili kwa sekta hii kuyumba huko mbele,hawa nao wameelemewa na mzigo hawa,wasaidie kuutua.

9.Mh Rais huko halmashaurini huko,hawezekana hawasemi ila sisi tunawasikia wakilalamika kuwa wameelemewa na mzigo wa miradi isiyotekelezeka kwani pesa nyingi wanazoomba hazipelekwi na zinazopelekwa hazipelekwi kwa wakati,Mh Rais wakurugenzi unaweza dhani hawafanyi kazi kabisa,hapana
mabadiliko ya kisera yamewabebesha mzigo mkubwa na umewaelemea,huu mzigo nao wanautuaje?

Mh Rais,walioelemewa na mizigo ni wengi na siyo wale tu waliokuwa CCM na kwenda upinzani,mizigo haipo kwenye siasa pekee.
Dotto ni mwana habari anaye jielewa sana hapa Tanzania
 
Doto Bulendu! Nimekumiss sana siku hizi sikuoni kwenye kipindi cha JICHO LETU NDANI YA HABARI. Wapi hicho kipindi? Maana siyo kwa ule uchambuzi wa kina!
 
Kwani wewe ulitaka bei ya sukari ya 2005 iwe mpaka leo? hauoni juhudi ya serikali ya kujenga kiwanda kikubwa cha sukari huko Morogoro? Vipi kuhusu wachina wanaokwenda kujenga kiwanda kikubwa Africa mashariki na kati cha cement huko Tanga? Watanzania tuwe wavumilivu hiki ni kipindi cha mpito tu.
Nmefikiria sana ulichoandika mpaka nmelazimika kuandika SIKUWA NA MPANGO WA KUANDIKA CHOCHOTE nlitaka nisome tu!.

Hivi kipindi cha nyuma hicho kiwanda kilikuwepo?,mbona bei hazikupanda?

Leo ya hizo juhudi ni nini kwa wananchi? Juhudi zisizo na manufaa za nini?
 
Halafu utoke hapa useme nchini hakuna uhuru wa maoni wakati unamtuka Rais kiasi hicho

Ungejijikita zaidi kwenye post namba moja maana ndio ina mambo ya msingi. Kama wangalau ungethubutu kujibu kwenye ile post ndio ningeamini ccm ina watetezi. Ukiangalia ile post namba moja ndio iliyo sababisha watu wengi hawapigi kura, kwani wakipiga na kumuonyesha rais hisia zao, matokeo yao yanabadilishwa na kupewa ccm.

Cc: Phillipo Bukililo, misuli, jmc06,
 
Jana wakati akitangaza majina ya wateuliwa kuwania nafasi za ubunge kupitia CCM kwa ajili ya uchaguzi mdogo,

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli alisema chama kitaendelea kuwapokea wanasiasa wote wanaotaka kurejea CCM na kuwaahidi pumziko lenye furaha.

Mh Rais alisema wale wote wenye mizigo huko walipo wahamie CCM ili waishushe mizigo waliyonayo na akasema wengi waliondoka CCM kutokana na figisu walizokutana nazo lakini wamekutana na figisu zaidi.

Sasa Mh Mwenyekiti na Rais wa chama,na sisi ambao hatupo kwenye siasa na hasa si wabunge na madiwani,mizigo yetu tukaitue wapi?maana

1.Huku mtaani tunaelekewa na mzigo wa kupaa kwa bei ya simenti,bei ya sukari ilivyopanda haijawahi kushuka,bei ya mafuta ya taa,Petrol na diseli nayo haikamatiki siki hizi,huu mzigo umetuelemea tukautue kwa nani Mh Rais?

2.Watumishi wa umma wameelemewa na mzigo wa kutokupandishwa madaraja(baadhi),miaka mitatu sasa hakuna nyongeza ya mshahara Mh Rais,huu ni mzigo umeaelemea watumishi wa Umma,wakautue wapi Mh Rais?usipoutua mzigo huu Mh Rais kuna hatari ya "Go slow strike".

3.Sekta binafsi zimeelemewa,sasa hivi wafanyakazi kwenye sekta binafsi wanahenya na maisha ya bila mishahara,waliowekeza huko wanalia mazingira ya biashara kiujumla hayawapi faida baadhi wanapunguza tu wafanyakazi,huu nao ni mzigo,kama ulivyo nukuu kitabu kitakatibu (Biblia),kwamba wote wenye mizigo iliyo waelemea waje kwako,wenye hii mizigo nao waje?

4.Mh Rais,vijana waliomaliza masomo yao vyuoni,shuleni ma vyuo vikuu kuanzia mwaka 2015 ulipotangaza oparesheni saka watumishi hewa na wasio na vyeti,asilimia kubwa hawajaajiriwa mpaka leo,wapo mtaani hawajui hatma yao,wameelemewa na mzigo wa ukosefu wa ajira na ukali wa maisha,Mh Rais watoto wako hawa unawasaidije kuutua huu mzigo,na jana ulisema wote walioelemewa na mzigo waje kwako Mh Rais,hawa nao waje?

5.Mh Rais yalifanyika mabadiliko ya kisheria ya mifuko ya jamii kwa kuzuia wastaafu kulipwa mafao yao mpaka watakapofikisha umri uliopotishwa,Mh Rais kuna kundi la watu wapo kwenye umri wa kati na wameamua kuacha kazi ili wakafanye mambo mengine,sasa wanapoambiwa wasubiri
mpala wafikishe umri uliopotishwa kisheria wamebaki njia panda,mzigo sasa umewaelemea hawajui pa kuutua,sijui tunawasaidiaje?

6.Mh Rais familia na ndugu wa Azory Gwanda,Ben Saanane wamelia sana kuwasaka ndugu zao,wanaelewa na mzigo wa mawazo walipo wapendwa wao,Mh Rais kama ulivyosema wote walioelemewa na mizigo waje kwako,kwa kutumia vyombo vyako,wasaidie familia hizi kuutua mzigo unaowaelea,hakuna mzigo mzito kama mzigo wa mawazo Mh.

7.Mh Rais,kule vijijini katazo la kusafirisha mazao nje,liliporomosha bei ya mazao,Maeneo mengi wanavijiji wamejikuta wamekaa na mazao ndani kwani soko la ndani limetengeneza hasara kubwa kwao,hawa nao wameelemewa na mzigo huu Mh Rais.

8.Mh Rais nadhani umesikia jana kuwa Ligi kuu msimu huu haitakuwa na mdhamini mkuu,na nimeona kuna mdhamini eti atadhamini kwa kuvipa vilabu shilingi milioni 15 kila kimoja,Mh Rais sekta binafsi iliyokuwa imewekeza huku waliowengi wanalia na faida kiduchu,wanadai mazingira ya biashara yamebadilika sana,sasa hata kwenye michezo taasisi za michezo zimeelemewa na mzigo,kuna kila dalili kwa sekta hii kuyumba huko mbele,hawa nao wameelemewa na mzigo hawa,wasaidie kuutua.

9.Mh Rais huko halmashaurini huko,hawezekana hawasemi ila sisi tunawasikia wakilalamika kuwa wameelemewa na mzigo wa miradi isiyotekelezeka kwani pesa nyingi wanazoomba hazipelekwi na zinazopelekwa hazipelekwi kwa wakati,Mh Rais wakurugenzi unaweza dhani hawafanyi kazi kabisa,hapana
mabadiliko ya kisera yamewabebesha mzigo mkubwa na umewaelemea,huu mzigo nao wanautuaje?

Mh Rais,walioelemewa na mizigo ni wengi na siyo wale tu waliokuwa CCM na kwenda upinzani,mizigo haipo kwenye siasa pekee.
Duuu umegusa maeneo muhimu sana yanayogusa utendaji kisera ambao huathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya kila siku
 
Haya mambo yalizungumzwa sana na wajuzi wa mambo huko nyuma na waliliona hili, ndiyo mzee inazidi kuipeleka nchi yetu kubaya washauri wamezira wamebaki kupiga makofi. Tutegemee matatizo na mizigo zaidi ya hii.
 
Na bado endeleeni tu kushabikia hakika tutakuja kuyashuhudia ya Somalia. time will tell, ujue mwenye shibe hajui maumivu ya wenye njaa.
 
kila kitu anachosema Rais ni kulingana na mazingira na mada usika,hawezi kuongelea mambo ya ccm kutawala milele akiwa kwenye mikutano ya EAC.Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais aliyoisema jana ni ya kisiasa anajaribu kuwavuta wapinzani waje ccm,sasa msitake kila Rais anapoongea azungumzie maji,afya na ajira kila kitu kinawakati wake wa kukiongelea.Jana Magufuli alisimama kama mwenyekiti wa ccm na sio Rais,ndio maana waziri mkuu akiwa jimbmi kwake anaongea kama Mbunge na sio mtendaji wa serikali.Halafu kumlaumu Rais kisa kupanda kwa mafuta ni ujinga maana mafuta yakipanda yanapanda dunia yote.FANYA KAZI ACHA KULIALIA
 
Back
Top Bottom