Dotto Bulendu: Rais, walioelemewa na mizigo ni wengi na siyo wale tu waliokuwa CCM na kwenda upinzani. Mizigo haipo kwenye siasa pekee

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Jana wakati akitangaza majina ya wateuliwa kuwania nafasi za ubunge kupitia CCM kwa ajili ya uchaguzi mdogo,

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli alisema chama kitaendelea kuwapokea wanasiasa wote wanaotaka kurejea CCM na kuwaahidi pumziko lenye furaha.

Mh Rais alisema wale wote wenye mizigo huko walipo wahamie CCM ili waishushe mizigo waliyonayo na akasema wengi waliondoka CCM kutokana na figisu walizokutana nazo lakini wamekutana na figisu zaidi.

Sasa Mh Mwenyekiti na Rais wa chama,na sisi ambao hatupo kwenye siasa na hasa si wabunge na madiwani,mizigo yetu tukaitue wapi?maana

1.Huku mtaani tunaelekewa na mzigo wa kupaa kwa bei ya simenti,bei ya sukari ilivyopanda haijawahi kushuka,bei ya mafuta ya taa,Petrol na diseli nayo haikamatiki siki hizi,huu mzigo umetuelemea tukautue kwa nani Mh Rais?

2.Watumishi wa umma wameelemewa na mzigo wa kutokupandishwa madaraja(baadhi),miaka mitatu sasa hakuna nyongeza ya mshahara Mh Rais,huu ni mzigo umeaelemea watumishi wa Umma,wakautue wapi Mh Rais?usipoutua mzigo huu Mh Rais kuna hatari ya "Go slow strike".

3.Sekta binafsi zimeelemewa,sasa hivi wafanyakazi kwenye sekta binafsi wanahenya na maisha ya bila mishahara,waliowekeza huko wanalia mazingira ya biashara kiujumla hayawapi faida baadhi wanapunguza tu wafanyakazi,huu nao ni mzigo,kama ulivyo nukuu kitabu kitakatibu (Biblia),kwamba wote wenye mizigo iliyo waelemea waje kwako,wenye hii mizigo nao waje?

4.Mh Rais,vijana waliomaliza masomo yao vyuoni,shuleni ma vyuo vikuu kuanzia mwaka 2015 ulipotangaza oparesheni saka watumishi hewa na wasio na vyeti,asilimia kubwa hawajaajiriwa mpaka leo,wapo mtaani hawajui hatma yao,wameelemewa na mzigo wa ukosefu wa ajira na ukali wa maisha,Mh Rais watoto wako hawa unawasaidije kuutua huu mzigo,na jana ulisema wote walioelemewa na mzigo waje kwako Mh Rais,hawa nao waje?

5.Mh Rais yalifanyika mabadiliko ya kisheria ya mifuko ya jamii kwa kuzuia wastaafu kulipwa mafao yao mpaka watakapofikisha umri uliopotishwa,Mh Rais kuna kundi la watu wapo kwenye umri wa kati na wameamua kuacha kazi ili wakafanye mambo mengine,sasa wanapoambiwa wasubiri
mpala wafikishe umri uliopotishwa kisheria wamebaki njia panda,mzigo sasa umewaelemea hawajui pa kuutua,sijui tunawasaidiaje?

6.Mh Rais familia na ndugu wa Azory Gwanda,Ben Saanane wamelia sana kuwasaka ndugu zao,wanaelewa na mzigo wa mawazo walipo wapendwa wao,Mh Rais kama ulivyosema wote walioelemewa na mizigo waje kwako,kwa kutumia vyombo vyako,wasaidie familia hizi kuutua mzigo unaowaelea,hakuna mzigo mzito kama mzigo wa mawazo Mh.

7.Mh Rais,kule vijijini katazo la kusafirisha mazao nje,liliporomosha bei ya mazao,Maeneo mengi wanavijiji wamejikuta wamekaa na mazao ndani kwani soko la ndani limetengeneza hasara kubwa kwao,hawa nao wameelemewa na mzigo huu Mh Rais.

8.Mh Rais nadhani umesikia jana kuwa Ligi kuu msimu huu haitakuwa na mdhamini mkuu,na nimeona kuna mdhamini eti atadhamini kwa kuvipa vilabu shilingi milioni 15 kila kimoja,Mh Rais sekta binafsi iliyokuwa imewekeza huku waliowengi wanalia na faida kiduchu,wanadai mazingira ya biashara yamebadilika sana,sasa hata kwenye michezo taasisi za michezo zimeelemewa na mzigo,kuna kila dalili kwa sekta hii kuyumba huko mbele,hawa nao wameelemewa na mzigo hawa,wasaidie kuutua.

9.Mh Rais huko halmashaurini huko,hawezekana hawasemi ila sisi tunawasikia wakilalamika kuwa wameelemewa na mzigo wa miradi isiyotekelezeka kwani pesa nyingi wanazoomba hazipelekwi na zinazopelekwa hazipelekwi kwa wakati,Mh Rais wakurugenzi unaweza dhani hawafanyi kazi kabisa,hapana
mabadiliko ya kisera yamewabebesha mzigo mkubwa na umewaelemea,huu mzigo nao wanautuaje?

Mh Rais,walioelemewa na mizigo ni wengi na siyo wale tu waliokuwa CCM na kwenda upinzani,mizigo haipo kwenye siasa pekee.
 
Kiukweli mizigo ni mingi sana! Kushikilia michango yetu ktk mifuko ya hifadhi ya jamii hata kwa wafanyakazi sekta binafsi eti mpaka miaka 55-60 huu nao ni mzigo tena mzito haswa ambao serikali imetutwisha. Wangekanyagana huko kwenye siasa huku wakatuachia. Kilio kila mahali
 
Nimestaajabu sana akili za mkulu anafikiri wabunge na madiwani ndo wenye matatizo akisahau wananchi ambao ndo wenye shida lukuki hii ina maana akili yake inawaza kubomoa upinzani kwa kuchukua viongozi wake akijitetea kwa hoja mfu kabisa.
 
Mh Rais hapa MAGU wananchi tangu nchi ipate uhuru wanamzigo wa ukosefu wa Maji mpka umeingia wewe bado maji wanatumia ya chumvi huu nao ni mzigo sasa unawasaidiaje kuutua? Au nao wajiunge ccm?kwani maji ya nchi hii ni ya wanaccm Mh Rais?
 
Kwa ujumla CCM, haiwezi kutatua changamoto zetu kama Taifa,

Kila kitu wao ni siasa,hizi pesa wanazoharibu kununua hawa wabunge na kufanya chaguzi zisizo na tija ni nyingi sana.

Zingeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo lingekuwa ni jambo la busara sana.
Yeye mwenyewe ni mzigo ,anabariki huu upuuzi kwa kusaidiana na kina pole pole,wanafikiri wanaungwa mkono wakati hali ni mbaya huku mtaani.
 
Yule bichwa maji haelewi haya,anabana pua eti mi sio mwanasiasa, matokeo yake ameendekeza upuuzi wa kisiasa anaacha nchi yetu pendwa inaangamia.
Halafu utoke hapa useme nchini hakuna uhuru wa maoni wakati unamtuka Rais kiasi hicho
 
Ndio maana yuko busy kutaka kuua upinzani kwasababu mengi yamemshinda na anahofia kushindwa katika sanduku la kura.
Jiwe yeye anajua wapinzani ndo wanamkwamisha kuleta badala kufanya maendeleo anapambana kuua upinzani ni akili za kipuuzi sana. Huwezi kuua upinzani kwa kununua madiwani na wabunge hata siku upinzani upo utaendelea kuwepo ameukuta upinzani ataondoka ataacha huo upinzani
 
Jana wakati akitangaza majina ya wateuliwa kuwania nafasi za ubunge kupitia CCM kwa ajili ya uchaguzi mdogo,

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli alisema chama kitaendelea kuwapokea wanasiasa wote wanaotaka kurejea CCM na kuwaahidi pumziko lenye furaha.

Mh Rais alisema wale wote wenye mizigo huko walipo wahamie CCM ili waishushe mizigo waliyonayo na akasema wengi waliondoka CCM kutokana na figisu walizokutana nazo lakini wamekutana na figisu zaidi.

Sasa Mh Mwenyekiti na Rais wa chama,na sisi ambao hatupo kwenye siasa na hasa si wabunge na madiwani,mizigo yetu tukaitue wapi?maana

1.Huku mtaani tunaelekewa na mzigo wa kupaa kwa bei ya simenti,bei ya sukari ilivyopanda haijawahi kushuka,bei ya mafuta ya taa,Petrol na diseli nayo haikamatiki siki hizi,huu mzigo umetuelemea tukautue kwa nani Mh Rais?

2.Watumishi wa umma wameelemewa na mzigo wa kutokupandishwa madaraja(baadhi),miaka mitatu sasa hakuna nyongeza ya mshahara Mh Rais,huu ni mzigo umeaelemea watumishi wa Umma,wakautue wapi Mh Rais?usipoutua mzigo huu Mh Rais kuna hatari ya "Go slow strike".

3.Sekta binafsi zimeelemewa,sasa hivi wafanyakazi kwenye sekta binafsi wanahenya na maisha ya bila mishahara,waliowekeza huko wanalia mazingira ya biashara kiujumla hayawapi faida baadhi wanapunguza tu wafanyakazi,huu nao ni mzigo,kama ulivyo nukuu kitabu kitakatibu (Biblia),kwamba wote wenye mizigo iliyo waelemea waje kwako,wenye hii mizigo nao waje?

4.Mh Rais,vijana waliomaliza masomo yao vyuoni,shuleni ma vyuo vikuu kuanzia mwaka 2015 ulipotangaza oparesheni saka watumishi hewa na wasio na vyeti,asilimia kubwa hawajaajiriwa mpaka leo,wapo mtaani hawajui hatma yao,wameelemewa na mzigo wa ukosefu wa ajira na ukali wa maisha,Mh Rais watoto wako hawa unawasaidije kuutua huu mzigo,na jana ulisema wote walioelemewa na mzigo waje kwako Mh Rais,hawa nao waje?

5.Mh Rais yalifanyika mabadiliko ya kisheria ya mifuko ya jamii kwa kuzuia wastaafu kulipwa mafao yao mpaka watakapofikisha umri uliopotishwa,Mh Rais kuna kundi la watu wapo kwenye umri wa kati na wameamua kuacha kazi ili wakafanye mambo mengine,sasa wanapoambiwa wasubiri
mpala wafikishe umri uliopotishwa kisheria wamebaki njia panda,mzigo sasa umewaelemea hawajui pa kuutua,sijui tunawasaidiaje?

6.Mh Rais familia na ndugu wa Azory Gwanda,Ben Saanane wamelia sana kuwasaka ndugu zao,wanaelewa na mzigo wa mawazo walipo wapendwa wao,Mh Rais kama ulivyosema wote walioelemewa na mizigo waje kwako,kwa kutumia vyombo vyako,wasaidie familia hizi kuutua mzigo unaowaelea,hakuna mzigo mzito kama mzigo wa mawazo Mh.

7.Mh Rais,kule vijijini katazo la kusafirisha mazao nje,liliporomosha bei ya mazao,Maeneo mengi wanavijiji wamejikuta wamekaa na mazao ndani kwani soko la ndani limetengeneza hasara kubwa kwao,hawa nao wameelemewa na mzigo huu Mh Rais.

8.Mh Rais nadhani umesikia jana kuwa Ligi kuu msimu huu haitakuwa na mdhamini mkuu,na nimeona kuna mdhamini eti atadhamini kwa kuvipa vilabu shilingi milioni 15 kila kimoja,Mh Rais sekta binafsi iliyokuwa imewekeza huku waliowengi wanalia na faida kiduchu,wanadai mazingira ya biashara yamebadilika sana,sasa hata kwenye michezo taasisi za michezo zimeelemewa na mzigo,kuna kila dalili kwa sekta hii kuyumba huko mbele,hawa nao wameelemewa na mzigo hawa,wasaidie kuutua.

9.Mh Rais huko halmashaurini huko,hawezekana hawasemi ila sisi tunawasikia wakilalamika kuwa wameelemewa na mzigo wa miradi isiyotekelezeka kwani pesa nyingi wanazoomba hazipelekwi na zinazopelekwa hazipelekwi kwa wakati,Mh Rais wakurugenzi unaweza dhani hawafanyi kazi kabisa,hapana
mabadiliko ya kisera yamewabebesha mzigo mkubwa na umewaelemea,huu mzigo nao wanautuaje?

Mh Rais,walioelemewa na mizigo ni wengi na siyo wale tu waliokuwa CCM na kwenda upinzani,mizigo haipo kwenye siasa pekee.
Dotto ni mwandishi mzuri sana wa habari Haogopi kusema ukweli hii ndio sauti za wasiokuwa na sauti
 
Kwa ujumla CCM, haiwezi kutatua changamoto zetu kama Taifa,

Kila kitu wao ni siasa,hizi pesa wanazoharibu kununua hawa wabunge na kufanya chaguzi zisizo na tija ni nyingi sana.

Zingeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo lingekuwa ni jambo la busara sana.
Yeye mwenyewe ni mzigo ,anabariki huu upuuzi kwa kusaidiana na kina pole pole,wanafikiri wanaungwa mkono wakati hali ni mbaya huku mtaani.
Hii sasa tumeshaingia full dictatorship hakuna aliyesalama hata wanaccm wenyewe
 
Kiukweli mizigo ni mingi sana! Kushikilia michango yetu ktk mifuko ya hifadhi ya jamii hata kwa wafanyakazi sekta binafsi eti mpaka miaka 55-60 huu nao ni mzigo tena mzito haswa ambao serikali imetutwisha. Wangekanyagana huko kwenye siasa huku wakatuachia. Kilio kila mahali
Nikiwaza hilo najikuta natamani hata kulia
Sekta binafs watu wanapunguzwa kila leo
Lkn ukitoka kazin hujui uanzie wapi
Hali ya nani huyu mtu machozi yetu na yawe juu yake na vizaz vyake
 
Hali mbaya sana mtu unaweza kazi ukiwa hujui kesho yake inakuwaje wajinga wachache wanatuletea siasa
 
Back
Top Bottom