Abery
Member
- Oct 18, 2016
- 25
- 59
Ameandika Mwandishi Dotto Bulendu
Kabla hatujaviona vyama vyingi ni kero na vinachelewesha Maendeleo tujiulize kwanza maswali yafuatayo;
1.Ubinafsishaji wa mashirika ya umma kwa bei ya kutupwa kulifanyika kwa sababu ya vyama vingi hivyo tuhakikishe vinakufa?
2.Kufa kwa reli ya kati kulisababishwa na vyama vingi hivyo inabidi tuhakikishe tunavifuta?
3.Kuuzwa kwa bei ya hasara kwa benki ya NBC kulitokana na vyama vingi hivyo tuhakikishe vinakufa ili tuirejeshe benki yetu?
4.Kuuzwa kwa hisa za shirika la simu la TTCL kwa bei inayotajwa ya hasara kulitokana na vyama vingi? na hivyo inabidi tuhakikishe vinafutika?
5.Kufa kwa viwanda na mashamba makubwa yaliyoasisiwa tangu wakati wa ukoloni kulisababishwa na vyama vingi vya siasa na hivyo tuhakikishe vinakufa?
5.Shule za Serikali kufanya vibaya na sasa wazazi wenye uwezo hawawapeleki tena watoto wao kwemye shule za serikali kumesababishwa na hivi vyama vingi hivyo tuhakikishe hakuna Diwani wala Mbunge wa upinzani?
6.Mikataba ya hovyo na hasara kwenye sekta ya madini iliyosababisha vifo vya watu huko Nyamongo,Kahama,Nzega n.k kulisababishwa na vyama vingi hivyo tuhakikishe halmashauri zetu,ndani ya bunge hakuna mwakilishi kutoka vyama vya upinzani?
7.Tanzania kufanya vibaya kwenye medani ya michezo kumesababishwa na hivi vyama vingi na hivyo yeyote anayeunga mkono vyama vya upinzania anatakiwa kuitwa siyo mzalendo?
8.Viwanda kutangaza kufunga uzalishaji kutokana na kukosekana kwa sukari kumesababishwa na vyama vingi vya siasa?
9.Tangu mwaka 2015,vijana wengi wahitimu wa vyuo vya kati na vyuo vikuu kukaa mtaani bila ajira kumesababishwa na vyama vingi hivyo tuhakikishe vinakufa ili ajira zifunguke?
10.Nyongeza ya misharaha kwa watumishi wa umma imekuwa inasuasua kutokana na vyama vingi vya siasa?
11.Wafanyakazi hewa serikalini walioisababishia hasara kubwa serikali kwa muda mrefu ni kutokana na vyama vingi na hasa mikutano ya vyama vya siasa?hivyo tufute mikutano yote ya vyama vya upinzani ili kuhakikisha hakuna watumishi hewa?
12.Shirika la ndege ambalo miaka 35 iliyopita lilikuwa na ndege zaidi ya kumi,zikatoweka mpaka kubaki na ndege chini ya tano,kulitokana na hivi vyama vya upinzani?hivyo tuvizike ili shirika la ndege liwe na ndege za kutosha?
13.Watu wakiwemo wabunge na mawaziri waliwahi kujigawia pesa za umma kutoka akaunti ya Escrow na kuisababishia serikali hasara,hiyo ilitokana na Uwepo wa vyama vya upinzania hivyo tuvifute ili Escrow isije jirudia?
14.Kuliibuka tuhuma za Rushwa za EPA na Meremeta,tuhuma hizi zilitokana na vyama vingi?hivyo tuvifute ili tusipate tena tuhuma za Epa na Meremeta?
15.Kuna kiongozi akijua kabisa yeye ni mtumishi wa umma,alijiuzia mgodi wa Kiwira tena kwa bei ya hovyo,alifanya hivyo kwa sababu ya uwepo wa vyama vingi hivyo tuhakikishe hakuna cha diwani wala mbunge wa kutoka upinzani kwenye halmashauri zetu na bungeni?wabaki wa chama kimoja?
16.Kuna waziri aliwahi ingia mkataba na kampuni ga Barrick kwenye mgodi wa Buzwagi ,je huyo waziri aliingia mkataba huo kwa sababu ya hivi vyama vingi?
Najaribu kuwaza tu kwa kina.