Dotto Bulendu: Najaribu kuitafakari Tanzania ya kesho itakuwaje?

mashakani

JF-Expert Member
Aug 15, 2018
618
1,000
Anaandika Dotto Bulendu
52020662_1435218229947633_6036323256011587584_n.jpg

1.Tazama jinsi baadhi ya watu wanavyoumia kuona Afya ya Tundu Lissu inaimarika siku baada ya siku,wengine mpaka wanahoji ilikuwaje Risasi zikamkosa dereva wake?,Tusifike huko,tulienda mbali.

2.Je ulipitia mitandao ya kijamii siku Waziri wa Maliasili na utalii Dr Hamis Kigwangwala alipopata ajali wakati akitoka safarini Arusha?uliona baadhi ya "comments za watumia mitandao ya kijamii?.Tusifike huko.

3.Kama hukuona zile za Kigwangwala,juzi tu hapa si ulisoma "Comments" za watumia mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wa "FB" wa EATV mara baada ya EATV kuweka nukuu ya Waziri wa Mambo ya ndani Dr Mwigulu Nchemba akiwaomba watanzania wamuombee baada ya kupata ajali huko Iringa?wapo walioona bora kumuombea punda kuliko binadamu,😳😳😳,Huko tumeenda mbali sana,tusifike huko.

4.Kuna siku EATV pia waliweka nukuu ya Mh Rais akiwataka watanzania wamuombee,ulipitia "Comments" za wachangiaji?.Tusifike huko,tutoke huko.

Nadhani kuna mahali tumeteleza na tunahijati kuzungumza ili tuueejeshe upendo tuliokuwa nao.

Nakumbuka kati ya mwaka 1995 mpaka 2010 hali ilikuwa mbaya sana kati ya wafuasi wa CUF na CCM.

Ilianza kama utani,baadhi ya viongozi wa kisiasa wakisimama majukwaani badala ya kutoa kauli za kuwaunganisha Wazanzibar,wao walitoa kauli za kuwatenganisha Wazanzibar,kisa huyu ni CUF na yule ni CCM.

Bahati mbaya kauli hizo za kuchochea chuki zilitoka kwenye vinywa vya baadhi ya viongozi wa juu kabisa ambao tulidhani wao walitakiwa kujitenga na kauli za kibaguzi.

Siku moja nikaenda Zanzibar,nikasema niende maskani ya Kisonge pale Unguja,nikichoshuhudia ni bango kubwa lenye maneno yanayohimiza ubaguzi dhidi ya Wapemba hususani CUF.

Nilipojaribu kusikiliza baadhi ya Redio za Zanzibar,nilistushwa na matangazo ya Redio moja iliyokuwa inarusha marudio ya hotuba ya Kiongozi wa juu wa Zanzibar aliyekuwa akihubiri chuki dhidi ya kada nyingine.

Hoja ya waliokuwa Serikalini ni kuwa Wapemba hususani CUF wanatumiwa na Waarabu na CUF ikishinda Sultan atarejea,hoja hiyo kwa bahati mbaya ilihubiriwa mpaka na baadhi ya viongozi wakuu wa Chama na Serikali.

Matokeo yake ni mbegu ya chuki ilijaa kwenye mioyo na vifua vya Wazanzibar,wale wa Pemba hususani CUF na wale wa Unguja hususani CCM.

Chuki ikazaa mpasuko mkubwa Zanzibar,Wazanzibar wakapasuka,chuki ikawatenga wakafikia hatua ya kutosalimiana,kutoshirikiana kwa lolote hata kwenye shughuli za misiba.

Nakumbuka mwaka 2005,wakati Rais Kikwete anachukua madaraka akilihutubia bunge,alisema "Nasononeshwa sana na mpasuko unaoendelea Zanzibar.

Bahati mbaya Rais wa kipindi hicho huko Zanzibar Dr Salmini wakati wa Utawala wa Rais Mkapa ,alimiani katika siasa za kuwajaza Wana CCM chuki dhidi ya CUF kuwa hao si Wazanzibar bali ni mawakala wa Sultan.

Bahati nzuri Rais aliyemfuatia Aman Karume hakutaka kuendelea siasa za kujaza chuki na hisia za kibaguzi katika mioyo ya Wazanzibar na hatimae CUF ikiongozwa na Maalim Seif walikaa meza moja na CCM ikiongozwa na Rais Karume kusaka suluhu ya siasa za chuki huko Zanzibar.

Bahati mbaya sasa Wabara hawataki kujifunza kwa yaliyotukuta Watanzania huko Zanzibar mpaka mwaka 2001 kwa mara ya kwanza taifa letu likatoa wakimbizi.

Taratibh huku bara nauona mseleleko wa kuelekea kwenye siasa za kujaza mbegu za Chuki na Ubaguzi miongoni mwa Watanzania na kisa kikubwa hawa ni CCM na wale ni kitoka vyama shindani.

Hebu jipe muda sikiliza maneno yanayotoka kwenye vinywa vya baadhi ya viongozi wetu,wanachochea kundi fulani kuchukiwa kwa sababu tu si wa upande wao.

Leo nchi yetu imefika mahali kiongozi wazi kabisa anashabikia na kifurahia mateso ya mtu ambaye si wa upande wake.
Leo unastuka kumsikia Kiongozi wa Serikali ama chama anawaambia wafuasi wake kuwa hawa wenzetu ni mawakala wa mataifa ya waliotunyonya(Mabeberu).

Inastusha kiongozi (Naibu waziri),anazungumza na kusema mtu huyu anayezunguka huko ni msaliti na dawa ya msaliti ni kumuondoa.

Kule Zanzibar ilianza hivi hivi,CUF wakaitwa mawakala wa Sultan,ikaonekana ni kawaida tu,mwisho wa siku matokeo yake yalikuwa mabaya sana kule Zanzibar.

Sasa hivi kuna kasi kubwa kutoka kwenye vinywa vya baadhi ya wanasiasa wakiwemo baadhi ya viongozi wa Chama tawala CCM wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari kuwahubiria na kuwajaza vifuani wanachama na wafuasi wao chuki dhidi ya wale wanaopingana na CCM.

Taratibu naona wale wa upande mwingine wanaanza kuyatapika yaliyomo vifuani mwao,tena bila woga.

Soma mrejesho wa maombi ya Waziri Mwigulu kwa watanzania kuwa wamuombee,utaona wapi tunakwenda.

Hebu tazama baadhi ya watu wanavyoumia Tundu Lissu kupona na wengine wanadiriki kusema Lissu asitishiwe mshahara wake.

Kwa kasi ya ajabu Watanzania sasa wamefikia hatua ya kuuliza huyu chama gani kabla hajatoa msaada hata ule wa hali(Sala).Ni hatua mbaya tunaikaribisha.

Si unafahamu pale bungeni kuna mwaka wabunge hawakushirikiana kwenye futari?si unafahamu kwenye mazishi ya mbunge mmoja kutoka Magharibi mwa Tanzani,wabunge wa kambi nyingine waliondoka na hawakuhudhuria maziko?si ukisikia kuna wabunge walipigwa stop kwenda kumuona mbunge mwenzao aliyekuwa rumande Arusha?si ulisikia eti kuna wabunge waliambiwa kwenda kumuona Lissu Nairobi ni usaliti?kama ni kweli tunatengeneza tatizo kubwa ambalo wenzetu Zanzibar walilijaribu kati ya Mwaka 1995-2000 na likasababisha tatizo kubwa sana.

Kule Rwanda ilikuwa kama utani tu,kabila hili linaitwa mende,(huku kwetu watu wanaitana Nyumbu),kabila lingine likatengeneza mpaka Amri zao kumi dhidi ya lingine na bahati mbaya baadhi ya vyombo vya habari vikahubiri chuki na kuzijaza vifuani mwa Wanyarwanda,kila mtu anajua nini yalikuwa matokeo yake.

Zile siasa za hoja kwa hoja,za kukaa mezani na kuzungumza pale tunapopishana zimeenda wapi?Maana mwana CCM ni Mtanzanja kama walivyo wana Chadema,CUF,Act,NCCR n.k

Mwaka 2005,Ndani ya CCM wakati wa mchuano wa kusaka mgombea Urais wa kuchukua kijiti cha Benjamini Mkapa,baadhi ya wanamtandao wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari waliamua kufanya siasa za kuchafuana.

Mgombea mmoja aliyekuwa na nguvu wakati huo na alipata kuwa kipenzi cha Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake,aliitwa kuwa ni Muhisbul,naambiwa na watu wake wa karibu ulikuwa ni mkuki uliochoma moyo wake na kuichukia siasa.

Hebu mioyo yetu itawaliwe na upendo,akili yetu iongozwe na siasa za hoja kwa hoja.

Panapovuka Moshi?
 
Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,392
2,000
Viongozi waangalie vinywa vyao, maneno yao hayafutiki nakumbuka madhara ya ukabila katika uchaguzi uliopita 2015 hayajatafutiwa suluhu na Watanzania huko vijijini na mijini haswa kanda ya Ziwa walilalizimishwa kufanya wasichokitaka, ukiwa kiongozi hafu hutaki hoja mbadala wewe ni mufilisi.
Mtu anaibuka anasema fulani sitaki nisikie anajiita Rais utadhani mtu akiitwa jina hilo basi ameshachukuwa nafasi ya JPM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,503
2,000
Tatizo kubwa ni la rais Magufuli kuwa mnafiki anayoyahubiri siyo anayoyaishi, na anayoyaishi siyo anayoyahubiri

Hawa viongozi wote wanaotoa kauli za kugawa Watanzania wanafanya hivyo kwa sababu nafasi yao ya uteuzi ndivyo inavyotaka

Ukiangalia ile kauli aliyomwagiza spika kuwatoa nje wabunge wa upinzani aliowaita yeye wapiga kelele ili Magufuli awashughulikie nje ya bunge ilikuwa kauli ya aibu

Baada ya Lissu kuipinga ile ripoti ya pili ya madini ya Prof Osoro na kuiita uchafu wa kitaaluma, rais Magufuli akaja kutamka maneno yafuata "hatuwezi kuwa vitani halafu askari aliye mbele ageuke na kuanza kushambulia wenzake, huyo hatuwezi kumuacha salama, hawezi kutugeuka tukamwacha" haya maneno ya rais Magufuli ni ya kichochezi na ya kisaliti kwa taifa, huwezi kuwa rais ukahubiri chuki hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Twoten

JF-Expert Member
May 4, 2014
1,408
2,000
Watu wasiyojulikana wamekuwa na nguvu kuizidi serikali ya awamu ya tano na wanapongezwa na ccm kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kumshambulia Lissu. Huu ni ubaguzi.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
6,759
2,000
Tumesikia maneno na tumeona juhudi za kuua vyama vya upinzani. Huu ndiyo msingi wa shida tunayopata sasa-nia ikiwa kuhodhi madaraka kwa njia yeyote ile. Wenye madaraka wasipo jitathmini hali itazidi kuwa mbaya. Siku hizi vigumu kuona tofauti ya mihimili mitatu navyombo vya usalama tilivyokuwa tunavisikia kwa mbali siku hizi utaviona penda usipende. Mola tusaidie.
 
Alex Mbwilo

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
343
500
Anaandika Dotto Bulendu
View attachment 1024639
1.Tazama jinsi baadhi ya watu wanavyoumia kuona Afya ya Tundu Lissu inaimarika siku baada ya siku,wengine mpaka wanahoji ilikuwaje Risasi zikamkosa dereva wake?,Tusifike huko,tulienda mbali.

2.Je ulipitia mitandao ya kijamii siku Waziri wa Maliasili na utalii Dr Hamis Kigwangwala alipopata ajali wakati akitoka safarini Arusha?uliona baadhi ya "comments za watumia mitandao ya kijamii?.Tusifike huko.

3.Kama hukuona zile za Kigwangwala,juzi tu hapa si ulisoma "Comments" za watumia mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wa "FB" wa EATV mara baada ya EATV kuweka nukuu ya Waziri wa Mambo ya ndani Dr Mwigulu Nchemba akiwaomba watanzania wamuombee baada ya kupata ajali huko Iringa?wapo walioona bora kumuombea punda kuliko binadamu,😳😳😳,Huko tumeenda mbali sana,tusifike huko.

4.Kuna siku EATV pia waliweka nukuu ya Mh Rais akiwataka watanzania wamuombee,ulipitia "Comments" za wachangiaji?.Tusifike huko,tutoke huko.

Nadhani kuna mahali tumeteleza na tunahijati kuzungumza ili tuueejeshe upendo tuliokuwa nao.

Nakumbuka kati ya mwaka 1995 mpaka 2010 hali ilikuwa mbaya sana kati ya wafuasi wa CUF na CCM.

Ilianza kama utani,baadhi ya viongozi wa kisiasa wakisimama majukwaani badala ya kutoa kauli za kuwaunganisha Wazanzibar,wao walitoa kauli za kuwatenganisha Wazanzibar,kisa huyu ni CUF na yule ni CCM.

Bahati mbaya kauli hizo za kuchochea chuki zilitoka kwenye vinywa vya baadhi ya viongozi wa juu kabisa ambao tulidhani wao walitakiwa kujitenga na kauli za kibaguzi.

Siku moja nikaenda Zanzibar,nikasema niende maskani ya Kisonge pale Unguja,nikichoshuhudia ni bango kubwa lenye maneno yanayohimiza ubaguzi dhidi ya Wapemba hususani CUF.

Nilipojaribu kusikiliza baadhi ya Redio za Zanzibar,nilistushwa na matangazo ya Redio moja iliyokuwa inarusha marudio ya hotuba ya Kiongozi wa juu wa Zanzibar aliyekuwa akihubiri chuki dhidi ya kada nyingine.

Hoja ya waliokuwa Serikalini ni kuwa Wapemba hususani CUF wanatumiwa na Waarabu na CUF ikishinda Sultan atarejea,hoja hiyo kwa bahati mbaya ilihubiriwa mpaka na baadhi ya viongozi wakuu wa Chama na Serikali.

Matokeo yake ni mbegu ya chuki ilijaa kwenye mioyo na vifua vya Wazanzibar,wale wa Pemba hususani CUF na wale wa Unguja hususani CCM.

Chuki ikazaa mpasuko mkubwa Zanzibar,Wazanzibar wakapasuka,chuki ikawatenga wakafikia hatua ya kutosalimiana,kutoshirikiana kwa lolote hata kwenye shughuli za misiba.

Nakumbuka mwaka 2005,wakati Rais Kikwete anachukua madaraka akilihutubia bunge,alisema "Nasononeshwa sana na mpasuko unaoendelea Zanzibar.

Bahati mbaya Rais wa kipindi hicho huko Zanzibar Dr Salmini wakati wa Utawala wa Rais Mkapa ,alimiani katika siasa za kuwajaza Wana CCM chuki dhidi ya CUF kuwa hao si Wazanzibar bali ni mawakala wa Sultan.

Bahati nzuri Rais aliyemfuatia Aman Karume hakutaka kuendelea siasa za kujaza chuki na hisia za kibaguzi katika mioyo ya Wazanzibar na hatimae CUF ikiongozwa na Maalim Seif walikaa meza moja na CCM ikiongozwa na Rais Karume kusaka suluhu ya siasa za chuki huko Zanzibar.

Bahati mbaya sasa Wabara hawataki kujifunza kwa yaliyotukuta Watanzania huko Zanzibar mpaka mwaka 2001 kwa mara ya kwanza taifa letu likatoa wakimbizi.

Taratibh huku bara nauona mseleleko wa kuelekea kwenye siasa za kujaza mbegu za Chuki na Ubaguzi miongoni mwa Watanzania na kisa kikubwa hawa ni CCM na wale ni kitoka vyama shindani.

Hebu jipe muda sikiliza maneno yanayotoka kwenye vinywa vya baadhi ya viongozi wetu,wanachochea kundi fulani kuchukiwa kwa sababu tu si wa upande wao.

Leo nchi yetu imefika mahali kiongozi wazi kabisa anashabikia na kifurahia mateso ya mtu ambaye si wa upande wake.
Leo unastuka kumsikia Kiongozi wa Serikali ama chama anawaambia wafuasi wake kuwa hawa wenzetu ni mawakala wa mataifa ya waliotunyonya(Mabeberu).

Inastusha kiongozi (Naibu waziri),anazungumza na kusema mtu huyu anayezunguka huko ni msaliti na dawa ya msaliti ni kumuondoa.

Kule Zanzibar ilianza hivi hivi,CUF wakaitwa mawakala wa Sultan,ikaonekana ni kawaida tu,mwisho wa siku matokeo yake yalikuwa mabaya sana kule Zanzibar.

Sasa hivi kuna kasi kubwa kutoka kwenye vinywa vya baadhi ya wanasiasa wakiwemo baadhi ya viongozi wa Chama tawala CCM wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari kuwahubiria na kuwajaza vifuani wanachama na wafuasi wao chuki dhidi ya wale wanaopingana na CCM.

Taratibu naona wale wa upande mwingine wanaanza kuyatapika yaliyomo vifuani mwao,tena bila woga.

Soma mrejesho wa maombi ya Waziri Mwigulu kwa watanzania kuwa wamuombee,utaona wapi tunakwenda.

Hebu tazama baadhi ya watu wanavyoumia Tundu Lissu kupona na wengine wanadiriki kusema Lissu asitishiwe mshahara wake.

Kwa kasi ya ajabu Watanzania sasa wamefikia hatua ya kuuliza huyu chama gani kabla hajatoa msaada hata ule wa hali(Sala).Ni hatua mbaya tunaikaribisha.

Si unafahamu pale bungeni kuna mwaka wabunge hawakushirikiana kwenye futari?si unafahamu kwenye mazishi ya mbunge mmoja kutoka Magharibi mwa Tanzani,wabunge wa kambi nyingine waliondoka na hawakuhudhuria maziko?si ukisikia kuna wabunge walipigwa stop kwenda kumuona mbunge mwenzao aliyekuwa rumande Arusha?si ulisikia eti kuna wabunge waliambiwa kwenda kumuona Lissu Nairobi ni usaliti?kama ni kweli tunatengeneza tatizo kubwa ambalo wenzetu Zanzibar walilijaribu kati ya Mwaka 1995-2000 na likasababisha tatizo kubwa sana.

Kule Rwanda ilikuwa kama utani tu,kabila hili linaitwa mende,(huku kwetu watu wanaitana Nyumbu),kabila lingine likatengeneza mpaka Amri zao kumi dhidi ya lingine na bahati mbaya baadhi ya vyombo vya habari vikahubiri chuki na kuzijaza vifuani mwa Wanyarwanda,kila mtu anajua nini yalikuwa matokeo yake.

Zile siasa za hoja kwa hoja,za kukaa mezani na kuzungumza pale tunapopishana zimeenda wapi?Maana mwana CCM ni Mtanzanja kama walivyo wana Chadema,CUF,Act,NCCR n.k

Mwaka 2005,Ndani ya CCM wakati wa mchuano wa kusaka mgombea Urais wa kuchukua kijiti cha Benjamini Mkapa,baadhi ya wanamtandao wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari waliamua kufanya siasa za kuchafuana.

Mgombea mmoja aliyekuwa na nguvu wakati huo na alipata kuwa kipenzi cha Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake,aliitwa kuwa ni Muhisbul,naambiwa na watu wake wa karibu ulikuwa ni mkuki uliochoma moyo wake na kuichukia siasa.

Hebu mioyo yetu itawaliwe na upendo,akili yetu iongozwe na siasa za hoja kwa hoja.

Panapovuka Moshi?
Unajua bwana watu wanajisahau sana, hawaelewi kwa nini wazungu wa ulaya wanawalipa posho wananchi wasio na ajira.ukipata nafasi ya kuula ili ule kwa raha usiwasahau ambao hawako katika anga hizo, masikini wakichachamaa kwa kuwa hawana cha kupoteza matajiri ndio watadhurika zaidi. tunaofaidi tunapokutana tuwakumbuke na walioko pembezoni, tukiendelea kuwaona mafala iko siku tutajuta zaidi hasa kwa kuwa hatujazoea dhiki kuliko wenye dhiki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom