Dotto Bulendu: Kwanini Ikulu tu ndio wapate live coverage, Bunge, Mahakama zinafunikwa?

Tunachotakiwa kujadili ni UHURU wa kuonge na kujadili mustakabali wa TAIFA letu.Na unapokuwa umeamua kuwa MTAWALA basi hakikisha unajua kwamba umeamua kuwa Mkubwa,na UKUBWA ni JALALA ambalo taka zote huwekwa humo.

Kawaida ya JALALA ni kutolalamika,hata vitupwe visivyotakiwa kutupwa halilalamiki hukubali yote na kuhifadhi yote.

Wakubwa hawa wakishajua kwamba wao ni MAJALALA basi watuache watanzania tunaowalisha na kuwavisha tutupe uchafu humo.Uchafu mwingine ni wa kwao wao wenyewe.Na ukifanya mema yale mema ni sawa na kupunguza uchafu kwenye JALALA.

Wanaompelekea mkuu maneno ya mitandaoni wamweleze tu Mkuu UKUBWA ni JALALA
 
Watanzania wengi waliumia sana walipoona bunge live limesitishwa kwa sababu lukuki ziso za msingi ila kwa mimi nasema kheri hutokana ndani ya tumbo la shari sasa zile live coverage zimekua diverted kutoka kwenye bunge mpaka hafla rais, katika shughuli zote rasmi rais amekua akionyeshwa mubashara hapa kwa jicho la ndani kabisa rais amelipiku bunge,

Kwangu mimi naona ni approach nzuri ya rais kutaka asikike zaidi ndani ya kila pembe na mipaka ya Tanzania, ila naona rais haitumii opportunity hii vizuri kama ilivyo ni golden chance, sasa imekua na kugeuka disaster, kwani baada kuona utamu ambao tumeukosa kuona ndani bunge live sasa tunaona khutuba za rais zilivyokua zinavunja moyo watanzania, zina zinaondoa matumaini, imekua sasa drama haionekanwi kwenye bunge ila inaonekanwa katika official function za rais anapotoa khutuba zake,

Imekua kawaida kuwa sisi watanzania tusubiri rais afanye shughuli iliyo rasmi kisha tunasuburi atasema nini au atamshambulia nani au atamjibu nani au atamkomesha kwa hiyo watanzania tumepata replacement ya bunge live, sidhani kama watanzania wanatumia nguvu kama walokua wanaitumia hapo mwanzo ilipokua bunge limezuiliwa kuwa live sasa hivi kuna drama inawaburudisha, Magufuli pity proverbs,

Tafadhali wahusika jaribuni kumshawisha rais awe anatumia khutuba anayo anandikiwa ili kuondoa hili, JMP PITY PROVERS ambazo zinalete negativity katika jamii
 
Kama kila mtu anabembeleza kuwa Rais atumie hotuba anazoandikiwa kwani akisema yake anaharibu basi ni wazi kuwa hana uwezo mzuri wa kuongoza na sio tegemeo katika kutumia akili yake mwenyewe.
Hiyo ndio maana halisi. Watu mnapochagua kiongozi wenu huwa mna tegemeo kubwa kuwa anao uwezo Mkubwa wa kufikiri haraka, hekima na busara, huruma na maadili na yote mazuri zaidi ya wengine. Sasa haya ndiyo maajabu kuwa mnaogopa asitoe hutoba kutoka kichwani kwake kwa vile hamuamini mazuri kutokea kichwani. MAAJABU HAYA KWA TANZANIA. Kwamba mna raisi mnampenda na kumwamini lakini hamuamini akili yake mwenyewe?
 
Walisema tufanye kazi badala ya kuangalia bunge live, sasa sijui yeye hizo hotuba zake za live ni kwa ajili ya watu gani na bado anahimiza hapa kazi.
 
Back
Top Bottom