nguruka wa kig0ma
JF-Expert Member
- Jan 16, 2020
- 2,946
- 2,929
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Wakati kinaanza kipindi chako tajwa hapo juu, mimi binafsi nilikipenda sana. Siyo mimi tu, niliona sehemu nyingi nilizotembelea watu wenye akili kubwa, uelewa mpana na wenye heshima wakiamka asubuhi mapema kukusikiliza ukiendesha kipindi, na kusikiliza hoja kinzani kutoka kwa washiriki uliowaalika.
Kipindi chako kilifanana na Malumbano ya hoja kilichokuwa kikirushwa na ITV kila Alhamisi na kuvutia watu wengi, ambacho kwa sasa kimepoteza maana na kukimbiwa na watu wenye weledi kukisikiliza hata kwenda kujumuika.
Nakumbuka, watu walitoka mikoani kwenda kujumuika, na makundi kukusanyika kwenye runinga maeneo mbalimbali. KWASASA KIMEPOTEZA MAANA YA KULUMBANA ILI KUTENGENEZA HOJA YA PAMOJA.
Naamini Serikali iliyopita ilikuwa inachukua vitu kwenye kipindi kile. Kipindi kile kilikuwa kama bunge, kasoro kusoma bajeti tu.
Jicho letu ndani ya habari kilikusanya watu kila Jumamosi, kusikiliza wataalam wa habari na wanasheria wakifukua madini, na wanasiasa kipigana vijembe. KIPINDI KILINOGA.
Nasikitika kusema, baada ya kutishwa na watawala ukaanza kualika watu wa upande mmoja, au watu kama Pascal Mayalla UMEKIHARIBU KIPINDI NA SASA KINAPENDWA NA UPANDE MMOJA TU, NA WASIO NA UWEZO WA KUPAMBANUA MAMBO.
Kumshirikisha Mayalla kwenye jicho letu ndani ya habari, umekiua kipindi. Mayalla anapotosha sana umma kwa kigezo cha u-nguli wa habari na kuijua sheria. Na kwakuwa watanzania wengi ni mbumbumbu, wanapotezwa.
Wenye akili na walioamka toka ujingani hawaangalii na kusikiliza jicho letu ndani ya habari siku hizi.
Mbona ulionekana ulionekana kuvaa ujasiri huko siku za nyuma, ujasiri umeupeleka wapi? Hata thread zako unazoandika humu huwa na ujasiri na nguvu kubwa, UMEUPELEKA WAPI UJASIRI?
DOTTO JITAFAKARI UPYA.
Karibuni,
Sent using Jamii Forums mobile app