Dotto Bulendu: Bila sekta binafsi imara hakuna uchumi wa viwanda. Sie matajiri waishi kama mashetani ndo la msingi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Zimefanyika tafiti za kutosha duniani na kuthibitisha pasipo na shaka,ili utengeneze uchumi
imara na endelevu lazima ujenge sekta binafsi imara!.

Wachumi wamefanya utafiti na kugundua kuwa,sekta binafsi ndiyo "engine" ya uchumi wa taifa lolote lile linalotaka kuwa taifa lenye nguvu.

Huwezi jenga uchumi wenye nguvu kama hujawa na sera,mpango,utashi wa kisiasa na dhamira ya dhati ya kujenga sekta binafsi imara ya yenye nguvu.

Namna pekee ya kujenga uchumi endelevu ni kutafsiri misingi ya utawala bora(haki za binadamu,utawala wa sheria,demokrasia,uwazi,ushirikishwaji,uwajibaki,matumizi sahihi na sawia ya rasilimali za nchi) kwa kuzitoa kwenye nadharia kwenda kwenye vitendo pamoja na kujenga sekta ni binafsi imara.

Serikali yenye yenye kuona mbali na siyo mbele,inapoona sekta binafsi inayumba,huchukua hatua haraka iwezekanavyo ,serikali inapoona sekta binafsi inasinyaa,huja na mkakati wa dharura kuzinasua sekta hizo zisiyumbe.

Bila kuwa na jicho la namba hiyo,ndoto za kulifanya taifa kuwa lenye nguvu ni ngumu sana kuzifikia,kama kiongozi mkuu wa nchi,dhibiti rushwa,weka vipaumbele vyako,ainisha ni rasilimali zipi utakazotumia kujenga nchi,jenga sekta binafsi imara na ingia nazo ubia wa kuendesha uchumi wa nchi,tafsiri misingi ya Utawala bora/uongozi bora kutoka kwenye nadharia kwenda kwenye vitendo.
 
Huyu nae atafeli tu kama yule bwana mwingine alivyofeli katika sera yake ya ubinafsishaji.

Waliompinga walishughulikiwa na kuonekana si walendo ila leo hii kiko wapi!!

Huyu nae anafutwa nyayo zile zile za kutosikiliza ya watu.

Time will tell.
 
Sekta binafsi kwa sasa ndio ipo hoi bin taabani toka Pogba akivyochukua Nchi..
Kavuruga msingi yote ya Uchumi iliyokuwepo..
Hivi sasa mambo ni hobela hobela tu.
 
Zimefanyika tafiti za kutosha duniani na kuthibitisha pasipo na shaka,ili utengeneze uchumi
imara na endelevu lazima ujenge sekta binafsi imara!.

Wachumi wamefanya utafiti na kugundua kuwa,sekta binafsi ndiyo "engine" ya uchumi wa taifa lolote lile linalotaka kuwa taifa lenye nguvu.

Huwezi jenga uchumi wenye nguvu kama hujawa na sera,mpango,utashi wa kisiasa na dhamira ya dhati ya kujenga sekta binafsi imara ya yenye nguvu.

Namna pekee ya kujenga uchumi endelevu ni kutafsiri misingi ya utawala bora(haki za binadamu,utawala wa sheria,demokrasia,uwazi,ushirikishwaji,uwajibaki,matumizi sahihi na sawia ya rasilimali za nchi) kwa kuzitoa kwenye nadharia kwenda kwenye vitendo pamoja na kujenga sekta ni binafsi imara.

Serikali yenye yenye kuona mbali na siyo mbele,inapoona sekta binafsi inayumba,huchukua hatua haraka iwezekanavyo ,serikali inapoona sekta binafsi inasinyaa,huja na mkakati wa dharura kuzinasua sekta hizo zisiyumbe.

Bila kuwa na jicho la namba hiyo,ndoto za kulifanya taifa kuwa lenye nguvu ni ngumu sana kuzifikia,kama kiongozi mkuu wa nchi,dhibiti rushwa,weka vipaumbele vyako,ainisha ni rasilimali zipi utakazotumia kujenga nchi,jenga sekta binafsi imara na ingia nazo ubia wa kuendesha uchumi wa nchi,tafsiri misingi ya Utawala bora/uongozi bora kutoka kwenye nadharia kwenda kwenye vitendo.
Matajiri waishi kama mashetani si MOTO ya serikali hii. Labda Dotto kama nae bongo yake haiko sawa kusikiliza speach za watu. Nakumbuka Rais alisema kuna watu wanaishi kama wako peponi. Haina maana ya matajiri. Unaweza kuwa tajiri kwa halal na unaweza kuwa na pesa nyingi za wizi. Alizungumzia wezi wa mali ya UMMA si matajiri wa halali. Tumieni bongo zenu na ninyi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom