Dotto Biteko, kuwafukuza wana Chunya kwenye eneo lao la machimbo ni unafiki

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Mwanzo nilikuona wa maana sana kumbe ndio walewale walamba viatu na wajali matumbo yao. We ni mtu wa ovyo, mzandiki na usiyefaa hata kidogo!

Umeamua kuwafukuza wananchi wa Chunya kwenye eneo lao waliokuwa wanachimba eti walimdanganya rais.

Wewe kama msaidizi wa rais, iweje ukubali bosi wako alishwe matango pori na wewe ukiwepo?

Kwanini muwafukuze wananchi baada ya JPM kufa?

Wewe pamoja na bosi wako wote hamfai!

======

Waziri wa Madini Doto Biteko amepiga marufuku shughuli za uchimbaji wa madini katika Mlima Kaputa kata ya Chalangwa Wilayani chunya Mkoani Mbeya.

Marufuku hiyo imetokana baada ya kubaini wananchi kuidanganya Serikali na kuwepo na chuki binafsi na mwekezaji Joseph Mwazyele kwa kumdanganya Rais hayati John Magufuli kuwa anachimba eneo la mradi wa matenki ya maji na makaburi na kupekea kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu.

Biteko amesema amefikia hatua hiyo na kukazimika kufanya ziara ya kujirisha na kubaini mwekezaji alikuwa akimiliki kihalali na kwamba mwekezaji huyo ajaliendeleza tangu alipofutiwa leseni mwaka 2019.

“Kwanza mmechuma dhambi mlimdanganya Rais kuwa mwekezaji huyo anachimba madini kwenye maeneo ya miradi na makaburi leo nimefika kuangalia uhalisia katika mlima huo na kubaini kuna udanganyifu kwani eneo hilo limevamiwa na wachimbaji wadogo kuanzia leo marufuku”alisema.

Biteko amesema kwa marufuku shughuli za uchimbaji kuendelea wakati Serikali ikiangalia nini cha kufanya na ,mpaka utaratibu utakapowekwa na Wizara kupata taarifa na serikali imejipanga.

Aidha alisema kuwa pia Wizara imebaini kuwepo kwa utoaji leseni kiholela mchimbaji mmoja kumiliki leseni lukuki na kutokana na changamoto hizo serikali imefuta Leseni 7,000 ambazo zitatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madino nchini.

Aidha kwa upande mwingine alisema kwa wilaya ya Chunya kwa mwaka wa fedha uliopita walikusanya zaidi ya Sh Bilion 28 wakati malengo ilikuwa bilioni 17 na kwamba ni wilaya inayofanya vizuri katika sekta ya madini mkoani Mbeya.

Biteko alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Chunya Masache Kasaka kuwa amekuwa akipeleka hoja za kuhitaji msaada wa serikali katika sekta ya madini wilayani humo na hivyo kuleta msukumo kwa wizara.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Saimon Mayeka Saimon alisema kuwa changamoto ya mgogoro huo umechangiwa pia na viongozi wa chama na wananchi wamekuwa wakilishwa maneno kwa migongo ya watu wengine.

“Sasa waziri kaagiza eneo hilo lisihusishwe tena na uchimbaji wa madini nitaweka ulinzi wa kutosha vijana wanataothubutu kuingia na kuchimba wakibainika watawajibishwa ,nasi tumejipanga kwani wananchi wa kata hii mnasifika kwa ukorofi”alisema.

Mayeka alisema kuwa mgogoro huo kama serikali waliufuatilia na kubaini mwekezaji huyo anamliki kihalali na suala na kuchimba kwenya miradi ya maji na makaburi sio kweli bali ni mambo ya kiasa kuingizwa

Salum Hussein, Mwenyekiti Chadema Kata amekiri wananchi kuimdanganya hayati John Magufuli kuwa mwekezaji huyo anachimba kwenye visima vya maji na makaburi na kwamba kuna makundi ya ndani kwa ndani .

“Waziri tukiri kumdanganya Rais huyu Mwekezaji alikuwa sahihi kabisa ila kuna makundi ambayo yalipelekea kutengeneza sumu na hivyo kuchelewesha maendeleo tunaomba arejeshwe kwani amekuwa na mchango mkubwa kwenye shughuli za maendeleo hususan ujenzi wa shule”alisema.

Mbunge wa Jimbo la Chunya, Masache Kasaka amewataka wananchi kuwa wavumilivu na kusubiri maamuzi ya Wizara ya Madini na kwamba wakubaliane n Matokeo kutokana na mgogoro huo kudumu na kukwamisha maendeleo.

Kasaka alisema kuwa ujio huo wa waziri na kujirishisha na kufanya maamuzi kwa kipindi hiki utaleta tija ya kuchochea shughuli maendeleo katika kata ya chalangwa kupitia madini ya dhahabu inayopatikana katika mlima huo.

Akizungumza mbele ya wananchi na Waziri wa Madini, Mwekezaji huyo alisema kuwa amesitisha shughuli za uchimbaji tangu Hayati Rais Magufuli alipomfutia kibali cha uchimbaji mwaka 2019.
 
Biteko mbona yupo juu ya sheria, alikua anakula na wachimbaji wadogo mererani, walikua wanampa millioni 10 kila mmoja (Wapo zaidi ya 200) ili awazuie baadhi ya wachimbaji wenye mashimo yenyewe mzigo. Usiku hao wachimbaji wadogo wakawa wanavamia machimbo amabayo sio yao na kuiba mzigo.

Hao anawatikisa ili wajiongeze akili, na wakijiongeza basi utaskia amewaruhusu kuendelea kuchimba.
 
Biteko mbona yupo juu ya sheria, alikua anakula na wachimbaji wadogo mererani, walikua wanampa millioni 10 kila mmoja (Wapo zaidi ya 200) ili awazuie baadhi ya wachimbaji wenye mashimo yenyewe mzigo. Usiku hao wachimbaji wadogo wakawa wanavamia machimbo amabayo sio yao na kuiba mzigo.

Hao anawatikisa ili wajiongeze akili, na wakijiongeza basi utaskia amewaruhusu kuendelea kuchimba.
Aisee Tzs 2,000,000,000 kwa uchache
 
Wewe ndo hovyo na wa wa ajabu kama ulikuwa ukiwaamini/unawaamini ccm na kuwaona wa maana!

CCM ni shetani katika mionekano ya kibinadamu
 
Hata kama wamevamia eneo halali la mtu mwingine? Kuna mambo tusipojifunza kuyaheshimu, ipo siku tutageuka minara ya chumvi. Haki ni kitu cha muhimu sana. Sio mambo ya kuwa popular hata kama hutendi haki
 
Huyu Bora angekuwa anachukua ten percent anaondoka sio anachukua kwa kuwanyanya wengine sio Siri Huyu Biteko Mnyarwanda anaihangaisha Sana secta ya madini toka Magu afariki Kuna eneo moja la Imwelo Wilayani Chato amepandikiza mgogoro mkubwa Sana baina ya mwekezaji amemwaga wanyarwanda wenzake wanachimba kibabe ameleta hadi polisi wanalinda wananchi wananyanyaswa Sana hawa jamaa ,Amekuja Mkuu wa mkoa na greda lake pamoja na mwekezaji greda likataka kuchomwa na wale jamaa kiuhalisia ni wababe harafu ni wanyarwanda wanadai ni eneo lao kiufupi Biteko Anaharibu utaratibu Namwomba mama amtupie na achunguzwe huenda hata hii Mali anawekeza kwa Rwanda.
 
Back
Top Bottom