Dotnata afanya kufuru kwa kvuta "Hummer" la nguvu

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
MSANII matawi ya juu katika tasnia ya filamu Bongo, Husna Mohamed Posh ‘Dotnata’ amefanya kufuru baada ya kutoa ‘burungutu’ kununua‘mkoko’ wa kifahari aina ya Hummer, Amani Jipya limeinyaka.

Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali za kuukomboa mkoko huo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam, Dotnata alisema kuwa ametumia kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 270 kununua ‘mchuma’ huo kutoka katika tawi la kiwanda cha magari hayo huko Detroit, nchini Marekani.

“Kila mtu atasema lake lakini ni kweli nimenunua gari hili kutoka Marekani na nimetumia kiasi cha shilingi milioni 270 mpaka linafika hapa,” alisema Dotnata.

White%20H2%20White%20Rims.jpg

Akiendelea zaidi, msanii huyo mwenye heshima kubwa ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo alianika kuwa watu wasimuelewe vibaya kwa kununua gari hilo amefanya hivyo akiwa na lengo la kulikodisha kwenye kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kupunguza makali ya maisha na siyo kutanua nalo kwa matanuzi yasiyo na lazima.

“Leo natarajia kukamilisha usajili hivyo mwishoni mwa wiki hii litakuwa barabarani lakini sitalitumuia kwa matanuzi kama ambavyo watu wanaweza kufikiria, nimepanga kulikodisha kwenye sherehe na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili linisaidie kujikwamua, ” alimaliza Dotnata

dotnata+3.JPG
 
aaache uongo Hummer hazizalishwi tena, sijui anamdanganya nani?, toka May 24, 2010, hummer haizalishi wala kuuza tena toka kiwandani.
 
Nashindwa kuamua kama ana rangi nzuri ya ngozi ama ni mambo yetu yaleee ya kujichubua...!:A S-confused1:
 
bongo bwana ushamba unatusumbua, hilo ndio suala la kuandika kwenye gazeti. Safi dada mwenyewe kajieleza vizuri yaani hajashoboka kabisa tofauti na mwandishi wa habari hy
 
bongo bwana ushamba unatusumbua, hilo ndio suala la kuandika kwenye gazeti. Safi dada mwenyewe kajieleza vizuri yaani hajashoboka kabisa tofauti na mwandishi wa habari hy

Mzee, Huijui Bongo? hapo usikute huyo bibie atakuwa amemkatia kidogo huyo muandhishi wa habari kuiandika hiyo habari ili kutujuza kuwa anaown a Hummer!! ushamba mtupu.

 
aaache uongo Hummer hazizalishwi tena, sijui anamdanganya nani?, toka May 24, 2010, hummer haizalishi wala kuuzwa tena kwani toka kiwandani.

na je kama kalinunua kwa mtu?....na sababu ya kusitishwa kutengenezwa ni nini?
 
Ujinga gani mnapost hapa JF?? Maisha binafsi ya mtu yanamhusu nani hapa? Ah!!
 
Mzee, Huijui Bongo? hapo usikute huyo bibie atakuwa amemkatia kidogo huyo muandhishi wa habari kuiandika hiyo habari ili kutujuza kuwa anaown a Hummer!! ushamba mtupu.


Watu kwa kuchonga!!!!si keshawaambia la biashara???? Sasa kwa nini asitangaze kama ana hammer na anaikodisha?Akikaaa kimya nani atalikodi???
 
Kwahiyo akinunua Hummer! Ndio Tunafanyaje?
Angenunua Escalede au Cadillac ingekuwa vipi? Nadhani ingekwa zaidi ya matangazo na habari wasanii wa kibongo wanapenda sifa za KIJINGA vitu vidogo tu Matangazo kila mtu ajue Gari kama hiyo sasa hivi Saudia ni Taxi
 
Dotnata anapata wapi pesa zoe hizo hadi kununua hummer asilolihitaji?

Au anawarusha roho wabaya wake wakati hamna kitu, bongo kila kitu is possible.
 
Hii nchi itachukua muda mrefu sana kujengwa kama bado fikra zetu zinaendelea zilivyo sasa...ni fikra za watu wavivu kufikiri, kuongelea mambo yasiyo na tija kabisa kwa jumuiya ya watanzania...labda kwa sababu ni udaku, na inawezekana kabisa nchi yetu sasa hivi ni ya kidakudaku!!!who knows!!!
 
Hapa kuna la kujifunza. Sina tatizo na mtu kuwa na gari, gari ni muhimu sana kiasi kwamba hata kama huna nyumba unaweza ukanunua kwanza gari na nyumba (kulingana na mazingira unayoishi) ikafuata baadae. Ila nina tatizo na gari ya gharama (or any other "toys") kubwa kiasi hicho. Gari kama hiyo inamfaidisha mtu mmoja tu, wakati kwa pesa hiyo hiyo unaweza ukajenga shule ambayo itafanya watu wapate maarifa/elimu, waalimu wapate ajira, na mwekezaji apate faida. Gari kama Hummer haileti pesa, bali inakula pesa ktk mafuta na vipuri. May be I don't know how it feels like to be a star....
 
Hilo Hummer aseme kanunua used..2010 GM walibaki na Hummer 2200 na zote zilishaisha...lakini kwani Hummer Big deal? mbona yamezagaa jamani na used Hummers Na used Hummers Prices ranger zake ni $28000-$61 000 while brand new toka kiwandani ambayo hayapo tena sa ivi price range zake ni $129,399.00 for the open-top; the wagon $140,796.00, H1 Alpha was priced at $150,975.00...in that range so huyu aiswafanywe watoto wadogo
 
Back
Top Bottom